Elections 2010 Mr. Sugu ashinda kura za maoni ubunge CHADEMA - Mbeya mjini

Not to say kwamba Sugu ni mkata viuno, au hana uwezo, lakini swali la kuulizia uwezo wake ni legit na linahitaji a thorough examination.

Mtazamo wako ni mzuri sana.
Inakuwaje swala la Mr. Sugu lionekane lihusishe uwezo wake? Je ni kwakuwa ametokea upizani?
Mi hata sikuelewi kwa maana inaonekana umaarufu wake umekufanya uhisi ndivyo sivyo....
Hao unaodhani wamekuwa wakigombea kwa kuwa wana uwezo wamefanya nini ktk nchi hii?

Go go go..... Mr. Sugu ...Its your time!
 
Ni akina wale wale tu........Hana tofauti na Ms Banji! Kawatukana watu matusi ya nguoni kisha tumfurahua! Ningesikitika kupata mbunge asiye na morals Kama huyo

Morals my ass. Nani mwenye haki ya kunyooshea vidole maadili ya mwenzake? Kwenye siasa hakuna maadili bana.....
 
Mtazamo wako ni mzuri sana.
Inakuwaje swala la Mr. Sugu lionekane lihusishe uwezo wake? Je ni kwakuwa ametokea upizani?
Mi hata sikuelewi kwa maana inaonekana umaarufu wake umekufanya uhisi ndivyo sivyo....
Hao unaodhani wamekuwa wakigombea kwa kuwa wana uwezo wamefanya nini ktk nchi hii?

Go go go..... Mr. Sugu ...Its your time!

Bora mr Sugu kuliko Kapt. Komba mfuata upepo (Kundi la wasanii)
 
CCM ina hali ngumu leo kuweza kumchagua ni nani ambaye anaweza kuchukua Jimbo hilo, ambalo tayari CHADEMA -Mbeya wametupa karata yao vizuri.

.

Nasikia Kutoka Mbeya kuwa Nkwenzuru ameibuka Kidedea kwenye kura za maoni za CCM
 
Two wrongs do not make a right, kama kuna watu walichaguliwa kwa kukata viuno hili halihalalishi wengine wachaguliwe kwa kukata viuno.

Not to say kwamba Sugu ni mkata viuno, au hana uwezo, lakini swali la kuulizia uwezo wake ni legit na linahitaji a thorough examination.
ni kweli kujua uwezo wake,
lakini mtaupimaje uwezo wake juu ya ugombea wake au mnamaanisha uwezo wa kimuziki?
na kama ni uwezo wa uongozi, hilo nadhani ni jungu tu bila ubishi, kina kikwete uwezo wa kuwa raisi
ulipimwaje, nadhani hakuna mzoefu bila kupitia mwanzo, mtu hazaliwi mzoefu, uzoefu huukuta pahali anapofanyia kazi...................go go Mr.Sugu
 
Morals my ass. Nani mwenye haki ya kunyooshea vidole maadili ya mwenzake? Kwenye siasa hakuna maadili bana.....

yep uko sahihi mkuu NN,
hasa siasa za bongo, maadili adimu kabisa, wana maadili hata wacheza picha za uchi
kuliko wanasiasa za bongo, (nasema hivyo kwa jinsia ya mwili)
 
Angalizo, Ila tu CHADEMA wawe makini maana CCM hawana dogo, wanaweza kutumia 'ruhani' la video ya Anti-virus ya Sugu kuipokonya CHADEMA ubunge kwa njia ya kesi ya pingamizi Mahakamani masaa machache kabla ya hitimisho la kufikisha majina ya wagombea ubunge NEC.
 
amechaguliwa kwa umaarufu wake ama uwezo anao?

Utajuaje uwezo wake kama hujampa nafasi? Hata JK alipogombe urais alichaguliwa kwa umaarufu lakini huko nyuma alikuwa ana harufu mbaya tu (Madini na Fedha). At least Mr. II aliwahi kupiga kelele kuhusu HAKI MILIKI kwa kazi zao ni tuliona matokeo yake pamoja na kwamba COSATA haijafanikiwa kihivyo kama nchi zingine. He can fight.
 
Nimjuavyo Sugu ni zaidi ya wanamuziki waliopo bongo. Kawatoa wengi sana, falsafa yake inajenga, sio mwoga na mawazo yake ni kupigania haki ya wanyonge pale alipo. Kupitia muziki alitoa, "Nipo mikononi mwa Polisi". Ni dhahiri ana upeo fulani, alimkumbuka hata marehemu Michael Sikupya.
Ni msanii wa kwanza kuleta summit hapa bongo, "Hip Hop Summit". Bahati mbaya aliwahubiria watu wasio na upeo wa kutosha.

Go go go go go go go Sugu nakuunga mkono unaweza kuleta mabadiliko
 
Nakubali Mr. II alipaswa kutumia sanaa kurekebisha jamii / kureveal uchafu uliopo katika sehemu mbali mbali lakini sio kwa kutukana watu, angetumia kauli sahihi watu wasingemponda. Kitendo cha yeye kama mwanamuziki mkongwe tena mwenye kuheshimika kutukana hadharani tena kwa kutumia kazi iliyompatia umaarufu ni cha kuhuzunisha sana, si ajabu akatumia kazi zake mbali mbali ikiwemo uongozi, kutukana watu / wabaya wake. Mimi nashauri ajaribu kuclear hilo tatizo la matusi katika wimbo wake, kama wanasiasa wangine wanavyofanya. Uongozi inahusisha uwezo wa mtu kukubali mistakes, hii inaongeza trust kwa wale wanaotegemea kupata uwakilishi bora.
 
WERA! WAREA! HONGERA, NINA FARAJA,
eBO WATAKOMA NA YAOMASIHARA
WAFANYAKAZI WANA UHAKIKA WA MISHAHARA
JIMBO LAKO LAZIMA LISEME AU LISPE KWENYE UFUKARA

VIVA SUGU
 
Back
Top Bottom