Mr. Nice Aokoka! Hallelujah!

eRRy

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
1,125
204
Aliyekua muimbaji wa Dansi nchini Lucas Mkenda au Mr. NICE kama anavyojulikana na wengi amempa Yesu maisha yake tangu mwezi wa nane mwaka huu. Anahudhuria ibada, maombezi na tayari amebatizwa. Chanzo cha habari kinasema anaabudu Kawe kwa GeoDavie jijini Dar-es-salaam, tayari ana nyimbo nne za kusifu na kumuabudu Mungu. Amekua akitoa ushuhuda wake kwamba Mungu amemponya na kuyaokoa maisha yake.

mr-nice.jpg

Source:http://strictlygospel.wordpress.com/2009/10/12/mr-nice-ameokoka/
 
Natamani awe ameokoka kweli-kweli lakin wasiwasi wangu anaweza kuwashambulia kondoo wa Bwana kwa staili ya ajabu mmh1
Otherwise Bwana amtangulie.
 
Mbona nimesoma jana tu kwenye magazeti kuwa ameanzisha bendi kama jibu kwa watu wanasambaza taarifa kuwa amefulia!!!!????
 
Hivi GeoDavis anahubiri na watu wanaokoka?? nimjuavyo yeye ana upako wa kuponya hana karama ya kuhubiri wokovu.

enewei nadhani mr. nice atakuwa kiumbe mpya akimaanisha hivyo au la ataota mkia sasa zaidi ya kufulia
 
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=3gBOdYXtuEg"]http://www.youtube.com/watch?v=3gBOdYXtuEg[/ame]
 
Kwanini hakudumisha imani kwa kanisa alilokuwa mwanzo na kumrejea muumba wake??? ... HUyo Kafuata pesa baada ya kufulia mtaani, period!
 
This is good marketing strategy for Mr. Nice, kaona kurudi juu tena haitawezekana,njia pekee iliyobaki ni kupitia "gospel", ila sijuwi kama ile miiko ya kiganga ndo imekwisha na jamaa yupo "free" sasa au vp, maana sifikirii kama gospel inaendana na uchawi.
 
Kila mtu ana maamuzi yake katika maisha..! Hakuna sababu ya kumshtaki mtu kwamba kafulia au la..fedha inaweza kuja na kutoweka kwa mtu yoyote yule.

unapo onyeshea kidole kwa mwenzio kwamba kafulia wakati wewe mambo yako yapo safi na wategemea yatakuwa safi siku zote basi mshukuru mungu au yule anaye kuwezesha.

Tabia za kuponda na kuzungumzia maisha ya watu wengine nadhani haiwezi kutusaidia zaidi ya kutudharaulisha sisi wenyewe.
 
Mambo ya ku 'recession proof his game'. Gospel inapanda chati kadiri world financial calamity inavyozidi. Akili kumkichwa.
 
kile kibwagizo nakisikia kwenye Tangazo la clouds Fm, la nyimbo za injili kumbe kaimbi Mr. Nice!!! imekaa vizuri
 
KILA JUMANNE:huwa anatumbuiza MASAI CLUB pale karibu na mango-garden.halafu jamaa anaongoza kwa kuomba bia mazee!yani akishaingia tu inabidi wadau tujifiche,maanake ni kama luba.

kwa mfanu jumanne iliyopita alikunywa sana konyagi.............

anaebisha tukutane nae kesho club masai
 
sasa si kanisani wanaendaga asubuhi, usiku anakuwa hapao masai, na mimi nilimuona last week hapo Masai. Mbona wa kuokoka kihivyo wapo wengi tu, huwa ninakutana maskani moja na dokta remmy ongala, napiga zake urabu na bangi kisha anafanya na yale mamabo yetu kisha asubuhi anaenda kanisani kuchapa misa.
 
This is good marketing strategy for Mr. Nice, kaona kurudi juu tena haitawezekana,njia pekee iliyobaki ni kupitia "gospel", ila sijuwi kama ile miiko ya kiganga ndo imekwisha na jamaa yupo "free" sasa au vp, maana sifikirii kama gospel inaendana na uchawi.

ina maana MR nice mziki wake ulikuwa unaenda na ushirikina

looh maybe ndo maana kaamua kurudi kundini
 
ina maana MR nice mziki wake ulikuwa unaenda na ushirikina

looh maybe ndo maana kaamua kurudi kundini

Mh! Siamini kama anatumia ushirikina kwenye mashairi kwa hio kuna thread huku pia waandikaji wanatumia ushirikina?
 
Back
Top Bottom