Mr. Lukuvi - This is too much bwana!

Anatoa tongotongo, maamuzi kama Lyatonga. Utendaji mzuri ni wa matendo si maneno. Anyway ni agizo zuri lakini halitekelezeki yaani mpaka kesho. Uamisho wa kawaida unachukua miezi kibao haya wa Lukuvi utachukua muda gani?
 
tusiwahukumu viongozi sawa wakati wote...hata nyerere pamoja na kuungwa mkono kwa mengi kuna wakati alikuwa anaharibu...mimi ni katika wale wanaohoji uwezo wa huyu bwana kiutendaji...
lakini kwahili la kuhakikisha wanafunzi wanasomea kwenye wilaya zao lina tija kiasi fulani, na kama ataweza kulisimamia itakuwa ni jambo zuri...kumbuka kila mtu alichangia ujenzi wa shule katika eneo/wilaya yake...lakini bado wizara imekuwa ikiwachagua wanafunzi kujiunga na shule zilizo nje ya wilaya wanazoishi...kuhusu suala usafiri Dar atakuwa amewasaidia sana watoto wetu ambao wanapata tabu sana na mnajua gharama za usafiri zinaendelea kupanda...suala muhimu hapa ni:
-kuboresha mazingira ya shule zote za serikali ikiwa ni pamoja na mitaala na miundo mbinu, ili watoto waliosoma shule za masaki wakikutana na wale wa TMK au gongo la mboto wasitofautiane sana...kila mtu anapenda mtoto wake apate elimu nzuri...
-walimu waboreshewe maslahi yao ili mwalimu akiambiwa akafundishe mbagala asione unyonge...
-idadi ya shule iendane na idadi ya walimu...sio mbagala shule ina mwalimu mmoja wakati ilala walimu wapo waziada...

nazani katika haya yamo yakuzingatia...wakati mwingine kumchukia mtu tuuuu hakusaidii kama aliyemuweka anampenda....yuko wapi Mataka...mtakuja kuwalaumu bure zeutamu kumba hoja mnawapa wenyewe....
Wewe mawazo yako kama Lukuvi na washauri wake; mtoto anayeishi mkwajuni (Kinondoni) na anasoma Tegeta (nayo Kinondoni) umempunguzia shida ya usafiri (? kiasi gani?) ukimlinganisha na anayekaa kariakoo (Ilala) na anasoma kule kule Tegeta (Kinondoni)? Au kwa kuwa ni wilaya ile ile anaweza kupuyanga kwa miguu?
 
Ameanza na hilo la wanafunzi kwasababu dhamira yake inamsuta kwani alishiriki katika wizi wa fedha za mradi wa mabasi ya wanafunzi Dar!! Wasiolijua hilo wawaulize mafisadi nguli wa ccm waliobaki!
 
Ameanza na hilo la wanafunzi kwasababu dhamira yake inamsuta kwani alishiriki katika wizi wa fedha za mradi wa mabasi ya wanafunzi Dar!! Wasiolijua hilo wawaulize mafisadi nguli wa ccm waliobaki!

Fafanua kidogo mkuu, alishiriki vipi? Hivi ule mradi wa DART (Dar Rapid Trasport) bado upo kweli, make nasikia ulikuwa ni wa World Bank na ulikuwa chini ya sykes akiwa Meya wa jiji! Sijamsikia Kimbisa akiongelea hili au ndo ugumu wa kutoa maamuzi kama kuivunja ubungo Plaza ili kupanua barabara????
 
jamani ehee! achane kumsema mkuu!jitihada alizozifanya kufika hapo si ndogo toka ualimu wa upe, kona zote za uwaziri mpaka bosi wa dar kwa wajanja ni jitihada binafsi kwenu mnakotoka kuna watu wa namna hiyo? tuachane wanyalu tutambe na kubopa wetu. mnakumbuka operesheni UPE ilikuwa mwaka mwaka gani? ndiko alikotokeo. Big up sana JK kwa kumchagua Bravo mkuu watu wanamna yake ni wachache sana nchi hii. Tangu aingie Dar hajapata usingizi mara mabomu, mara misaada akimbizane na wachina. kuwaonea huruma watoto wenu inakuwa shida kumbukeni kuwa huyo ni mwalimu wa UPE anajua shida shida za wanafunzi.
 
jamani upeo huo ndo wake ameanzia ualimu wa UPE kwa wanaokumbuka UPE ilikuwa ni wanafunzi waliofeli std seven 7 walipewa mafunzo ya miezi na kukabidhiwa darasa kwa hilo William kajitahidi. halafu jamaa huwa hataki ushauri kwa watendaji wake hajiamini kisa elimu. mwachani apumzike tangu aingie mji kasoro bahari hajapumzika ,mabomu , wachina na umachinga sasa ameamua kuwaonea huruma wanafunzi kutokana na fani aliyosomea JK alikosea kumpa hicho cheo!
 
Kwa mtindo huu wana JF tunakuwa vichaka.Kabla ya kuhoji lazima kujua aliongelea shule zipi.Na uamuzi huu utawasaidia nani hao hao wanaohama kila mwezi au mwaka hawawezi kuwalipia nauli wanapo kwenda shule kwa kubadilisha mabasi matatu.Mimi nimehama karibu wilaya zote na niliwaombea watoto wangu uhamisho.Inaelekea kuna watu wanajifanya watetezi wa wananchi ili hali hawajui mazingira magumu wanayoishi nayo.kuhusu tatizo la usafiri liko nje ya uwezo wa mkoa kama alivyosema waziri mkuu ,
 
Kwa mtindo huu wana JF tunakuwa vichaka.Kabla ya kuhoji lazima kujua aliongelea shule zipi.Na uamuzi huu utawasaidia nani hao hao wanaohama kila mwezi au mwaka hawawezi kuwalipia nauli wanapo kwenda shule kwa kubadilisha mabasi matatu.Mimi nimehama karibu wilaya zote na niliwaombea watoto wangu uhamisho.Inaelekea kuna watu wanajifanya watetezi wa wananchi ili hali hawajui mazingira magumu wanayoishi nayo.kuhusu tatizo la usafiri liko nje ya uwezo wa mkoa kama alivyosema waziri mkuu ,

SaidSabke,
Mkuu ninakupongeza kwa kuwaweka sawa hawa wenzetu wengine waliotangulia kuchangia. Ni vizuri tukaelewa kuwa huu mpango haumwangalii mtu mmoja mmoja unaangalia population as a whole. Kama tutaonglea matakwa ya mtu binafsi basi tukumbuke kutakuwa na mawazo zaidi ya milioni moja na ni lazima tuchukue wazo moja.
Nadhani wote tunaelewa kuwa wanafunzi wa mkoa wa Dar wanakabiliwa na tatizo la usafiri, tumekuwa tukishuhudia jinsi wanavyopata taabu ikiwa ni pamoja na kuchelewa kufika shuleni / majumbani.
Tatizo hili linalowapata wanafunzi ni lazima lishughulikiwe kwa namna yeyote ile. Kupata ufumbuzi si lazima tujaze magari barabarani (barabara pia hazitoshi foleni ni nyingi) kwani suala la uchelewaji litakuwa halijapatiwa ufumbuzi, tutaendelea kulalamika kuwa magari yapo lakini watoto hawafiki shule au majumbani kwa wakati kwa sababu ya foleni.
Mimi nadhani ni muhimu kuwa na njia mbadala ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafunzi walio wengi wanasoma maeneo karibu na mahali wanapoishi ili iwe rahisi kwao kwenda na kurudi nyumbani.
Kwa mfano katika nchi zilizoendelea, hawarusu watoto kusoma nje ya shule zilizo katika neighbourhood zao. Uandikishaji wa watoto katika shule unazingatia mahali pa ukazi. Mkazi nje ya neighbourhood hawezi kuandikishwa katika shule za eneo hilo. Hali hii imekuwa pia ni rahisi kutoa huduma za usafiri ndani ya eneo husika kwani inajulikana kabisa katika eneo hilo ni wanafunzi wangapi ndiyo wanahitaji usafiri kwa maana ya kuwa wamepanga watoto wanaoshi umbali fulani watakuwa entitled kupatiwa usafiri.
Ni kawaida ya binadamu kupinga mabadiliko lakini wakishaona faida zake wataweza kuelewa ni kwanini mabadiliko yalikuwa ni muhimu.
Kwa kumalizia Mh Lukuvi yupo sahihi kabisa katika ku-deal na tatizo la wanafunzi.

Angalizo: Mara zote utaratibu huu wa kuwataka watoto wasome katika maeneo yao ni kwa zile shule za public na haziwahusu wale wanaosoma katika private school kwani tayari huwa na utaratibu wao wa usafiri.
 
du!!!kama mkuu wa kaya kapatikana!!does he real use brain kufikiri au anatumia moyo kufikiri nn cha kulopoka!!
 
jamani upeo huo ndo wake ameanzia ualimu wa UPE kwa wanaokumbuka UPE ilikuwa ni wanafunzi waliofeli std seven 7 walipewa mafunzo ya miezi na kukabidhiwa darasa kwa hilo William kajitahidi. halafu jamaa huwa hataki ushauri kwa watendaji wake hajiamini kisa elimu. mwachani apumzike tangu aingie mji kasoro bahari hajapumzika ,mabomu , wachina na umachinga sasa ameamua kuwaonea huruma wanafunzi kutokana na fani aliyosomea JK alikosea kumpa hicho cheo!

Mkuu una maana Ualimu Pasipo Elimu ( UPE) nini?
 
Mwenye kuelewa ule mradi wa mabasi yaendayo kasi (Dar Rapid Transport- DART)jamani, atumwagia hapa jamvini.
 
Ndiyo matatizo ya sheria zinapotungwa na kila mtu hata pale ambapo anakuwa ndiyo kwanza katoka ******, bila kujali kama sheria inamruhusu kufanya hivyo au la. Cha kusikitisha zaidi ni pale ambapo raia, na viongozi wengine wote kukaa kimya kama vile hakuna cha ajabu!
 
Back
Top Bottom