Mr Kuchekacheka na maisha ya watanzania

mwandiga

JF-Expert Member
Dec 5, 2011
1,506
661
Namshangaa sana rais kikwete a.k.a Mr kuchekacheka kwa jinsi anavyofanya masihara na maisha ya watanzania. Kwa kweli maisha yanazidi kuwa magumu sana na kila kukicha ni afadhali ya jana, sukari inazalishwa hapa tz tena kuna viwanda kibao lakini kila siku bei inapanda. Leo nimenunua kilo kwa shilingi 3,000/-
Umeme ndio huo unapaa kama Tai vile
Kwa ujumla vitu vyote vimepanda bei huku wale wafanyakazi wa serikali mishahara iko pale pale, lakini jamaa anachekacheka tu hasemi lolote la maana bali tumethubutu tumeweza na tunasonga mbele.
Walimu walimaliza vyuo mwezi wa sita mwaka jana hadi leo hawajui wataajiriwa lini kisa fedha hakuna lakini maadhimisho ya miaka 50 mabilioni yametumika. Shame upon this country na viongozi wake. Tanzania ni nchi yenye utajiri mkubwa sana lakini huyu bwana anawachekea wazungu wanaoiba huu utajiri wetu. Utadhani sio mtanzania vile, yupo kimya kwa mambo ya msingi ambapo ndio wakati aliopaswa kuonyesha msimamo wa nchi na maamuzi magumu ili kuwakomboa watu wake (watz )
Mafuta yanapanda bei kila siku huku wauzaji wakifanya maamuzi wanayoyaona yanafaida kwao huku jk amekaa kimya tu. Akija kuongea anacheka tu na kuongea upupu. Watanzania tutafika????
Greater thinkers changieni.
Mods chonde chonde msiitoe hii topic kwani nyie pia hii hali ya taifa kwa namna moja au nyingine inawaumiza na hamuipendi, solutions nzuri zinaweza tolewa hapa na Baba riz akazichukua
 
Sikubaliani nawe uliposema shame upon this country kwani tatizo sio country ni uongozi wakiongozwa na mtawala jk.
Ila ni wakati wako pia wakuhamasisha watanzania walokuzunguka kuhusu maamuzi sahihi 2015,kwani meng yashasemwa lakini hatuoni mabadiliko so 2015 tusirudie makosa yakuuza kura chagua Cdm ilikupunguza matatizo ulotaja.
 
mpaka kufikia 2015 hapa katikati watanzania tutapitia magumu mengi sana na maisha yatzidi kuwa magumu, hiyo inatokana na sisi watazania kutotaka kubadirika.People wake up tusifanye makosa ambayo tumekuwa tukifanya miaka yote iliyopita ikifika mwaka 2015.Ni wakati wetu wa kufanya maamuzi magumu sasa kwaajili yetu na vizazi vyety vijavyo!!
 
Ugumu wa maisha upo kila kona ya dunia hii.
Hujasikia yanayoendelea nchi nyingine?
Dunia nzima uchumi unayumba mkuu.
Kenya na uganda bei ya sukari ni kubwa kuloko hapa.
Walimu umesikia mtapangiwa kazi mwisho wa mwezi huu.
Fanya kazi acha kulalama mtoto wa kiume.
OTIS
 
****** kaza uzi,wananchi legelege ndo huzaa serikali legelege,****** ndo Rais anae reflect tabia halisi za wa TZ,kupenda sherehe sana,masihara kwenye mambo ya msingi,uongo,unafki na usani wa kitapelitapeli,Uongozi hauwezi kubadilika isipobadilika jamii yenyewe,je Jamii ya kibongo imebadilika??
 
....daima na mileleeee! Aminaaa!
 
mpaka kufikia 2015 hapa katikati watanzania tutapitia magumu mengi sana na maisha yatzidi kuwa magumu, hiyo inatokana na sisi watazania kutotaka kubadirika.People wake up tusifanye makosa ambayo tumekuwa tukifanya miaka yote iliyopita ikifika mwaka 2015.Ni wakati wetu wa kufanya maamuzi magumu sasa kwaajili yetu na vizazi vyety vijavyo!!

Hamna haja ya kusubiri mpk 2015!! TUKINUKISHE tu hata leo hii .......
 
Ugumu wa maisha upo kila kona ya dunia hii.
Hujasikia yanayoendelea nchi nyingine?
Dunia nzima uchumi unayumba mkuu.
Kenya na uganda bei ya sukari ni kubwa kuloko hapa.
Walimu umesikia mtapangiwa kazi mwisho wa mwezi huu.
Fanya kazi acha kulalama mtoto wa kiume.
OTIS
Sio nalalama nasema ukweli na ukweli utabakia kuwa ukweli no matter what. Hauwezi kuifananisha Uganda na Tanzania hata Burundi tu iko juu kuliko Tanzania japo ilikuwa na vita. Ajira za walimu umeziona zimetangazwa au umesikia (hearsay) Viongozi wa Tanzania wakiongozwa na JK ndio wamesababisha tuwe hapa tulipo.
Nifanye kazi hiyo kazi iko wapi? Kila siku nazunguka na vyeti naambiwa sina uzoefu wakati fresh graduates wakike wanapata kazi. Kama wewe uliingia hapo ulipo kwa kimemo sio wote wamejaaliwa hivyo. Ss watoto wa kapuku hatuna hiyo nafasi na tazama siku inakuja hicho kimemo kitalipuka na hautakuwa na jeuri ya kusema ACHA KULALAMIKA FANYA KAZI
 
Teh teh teh teh kama ningekuwa na uwezo ningeomba mchele na unga ufike kilo sh 5000.
Sukari ifike hata sh 7000
umeme ndiyo iwe kama anasa upande hata kwa 300%.
Iliwananch wanayo ing'ang'ania ccm wastuke tatizo vikanga,kofia,t-shirt na mashati huwa vinawadanganya nakufanya maamuzi ya kiupupu sasa life likiwa la stage hiyo ndiyo itakuwa poa tuone kama hizo kofia,t-shirt,masharti kanga na pombe za kienyeji zitawasaidia.
Tushafanya kosa na kurudia mara nyingi now ni mda wa kuchange.
 
Back
Top Bottom