Mr II (Sugu) katika kashfa ya wizi wa wimbo wa Mr Blue 'Freedom'

Alichofanya Sugu ni "Mix Tape",hii ipo kote duniani,Legendary kufanya "mixtape" ya wimbo aliyowahi kushiriki ili kuwapa radha mashabiki wake wanaokubali mziki wake.Sugu ana mashabiki wanaopenda Hip hop yake,na mwenyewe kasema baada ya harakati za Siasa aliamua kuwapa watu wake radha ya wimbo katika Audio na Video

Sugu hajaufanya huo wimbo kibiashara au kiushindani,ameufanya wimbo huo just kuwapa burudani watu wake.Ndio maana kwa "uugwana" kaamua kutoa ile mistari ya Mr Blue,pengine "concern" ya Mr Blue ni kuona kwanini Sugu kamuita Roma na kina Prof J yeye akaachwa??

Sugu ana "haki" zake katika Verse alizochana na Mr Blue,ndio maana kachukua zile zake tu,na za Mr Blue kaziacha.Hili ni tatizo kwa Wasanii wa Bongo kukutana vijiweni bila kuwa na "Haki Miliki" za wimbo,kama umeimba na mtu kwa kumshirikisha,na haki miliki ipo kimya,mistari aliyoimba mwenzako kwa kumshirkisha inabaki kuwa yake na wimbo unabaki kuwa wenu.

Mix-Tape ipo sehemu zote duniani....Maana hapa kuna watu wameanza kuingiza UKAWA na CCM bila hata kupata muda wa kujiuliza.Hii kazi ya kumuandama Sugu inaendelea,maana wakati anaandaa nyimbo zake akaja humu Lizaboni kusema Sugu anamiliki magari ya kifahari

Leo Mr Blue anasema "kaibiwa",halafu leo leo saa tatu usiku Clouds Tv Kipindi cha "Take One" Zamaladi mke wa Ruge atamuhoji Mzazi mwenzake na Sugu maswali ambayo najua baada ya kipindi uzi utaletwa hapa.Ndio maana siipendi siasa,kutwa kucha kuviziana

Beka kaimba wimbo wa Adela,na hakuna lolote sbb ilikuwa kama "mixtape" tu.Sugu hajautoa wimbo huo kwa "Commercial purposes" hiyo ni zawadi ya mahadhi yake kwa wale waliokuwa wamemiss miondoko yakeView attachment 342479View attachment 342480
Tofautisha mixtape na cover song...kwa hili sugu habebeki.
Sugu kaiba wimbo wa mr blue. Kwanza huyu jamaa (sugu) ni mnafiki na kigeugeu sana. Harakati zake za vinega/anti-virus ziliishia wapi? Aliwaacha wenzake kijiweni, yeye akala pesa za ruge..leo kachukua wimbo wa mr blue na kusema wake. Hizo harakati unazosemaga unafanya ni zipi?? Harakati za kinafiki tu.
Sugu, you're douche.
 
MAJIBU YA MJ RECORDS NA SUGU...
Kutoka Bongo5.com
Lakini katika kila malalamiko, ni vyema kusikiliza pande zote zinazohusika kwenye jambo husika ili kuupata ukweli. MJ Records walioutayarisha wimbo huo wamezungumza kuelezea mambo yalikuwaje.

Producer mkuu wa studio hiyo, Marco Chali ameiambia Bongo5 kuwa beat ya wimbo huo ilitengenezwa na mdogo wake, Daxo Chali aliyetengeneza chorus yake na alimpa msanii wake Lizzy aliyeingiza.

“Ngoma ilikuwa ipo tayari na ilikuwa inasubiria verse tu kadhaa halafu ilikuwa ni ngoma yake [Daxo]. Kwahiyo jamaa [Blue] akawa ameipenda tukampa akasema atamshirikisha Mr Two,” amesema Marco.

Walipoifanya, Blue aliiamua kuiachia kupitia Mkito peke yake kwa maana kwamba hakuiachia ngoma rasmi. Anasema baada ya muda Sugu alimpigia simu kumuomba kuwa afanye version nyingine ya wimbo huo na aifanyie kabisa na video.

Anadai alimuambia Sugu aongee na Daxo waliyekubali kuufanya tena hadi video ikafanyika huku yeye [Marco] akiwa hajui chochote kilichoendelea baada ya hapo. Na Marco anasema pia hakuhusika kwenye uingizaji wa sauti zote mbili zaidi ya kuzifanyia mixing peke yake.

Marco amesema anadhani wawili hao [Sugu na Blue] waliongea kuhusu hatua hiyo na kwamba wao kama studio hawakuwa na kipingamizi chochote kuhusu kurudiwa kwa wimbo huo kwasababu walitaka wimbo ufike mahali.

Hata hivyo Marco amedai kuwa wote wawili [Sugu na Blue] hawakulipia wimbo huo na kwamba MJ Records iliwapa kwasababu ya ‘love’ tu. Marco anasema anashangaa kuona Mr Blue sasa hivi anatoa malalamiko hayo.

“Ni kwasababu mimi nilipenda tu kutoa studio bure kwanini usijitahidi ukapeleka hiyo nyimbo ikafika sehemu ikafahamika, at least pia akili za watu zilizotumika watu wazione. Na ndio hicho kitu naona ni kizuri, yeye kwa mfano angefanya hata video, sidhani kama Sugu angerudia huo wimbo,” ameongeza Marco.

“Na yeye aliposema kwamba anataka afanye video, namaanisha kwamba walishaongea na Blue kwamba yeye afanye video. Halafu Daxo wasije kumweka tena kwenye matatizo akaonekana kwamba ni producer mzinguaji ni vitu ambavyo havitamsababishia biashara na dogo mwenyewe ndio anataka kutoka. Na anajua wazi kuwa ni watu wazima wameongea kule,” amesisitiza Marco.

Naye Sugu amedaiwa kujibu malalamiko ya Blue kwa ujumbe huo chini kwenye WhatsApp.

Sugu-2.jpg
 
Ushauri wa bure: Vijana hamuwezi kupata haki zenu Instagram au Facebook, nendeni kwenye vyombo vinavyosimamia sheria. Inasikitisha vijana wamekosa akili kabisa, juzi tumeona mwingine kaenda kushtaki Instagram eti kabakwa na msanii. Hivi hizi ni akili za wapi?
 
Mbunge wa mbeya mjini na mkongwe wa muziki wa hip hop bongo Sugu a. K. a Mr II hivi karibu aliiachia wimbo wake mpya audio pamoja na video ujulikanao kama FREEDOM' Baada ya kuwa ahidi mashabiki wake kuwa yeye harakati za mziki zinaendelea

Mara baada ya kuachia wimbo huo ndipo MR BLUE alipo kuja juu na kuandika kupitia ukurasa wake wa instagram akiwaomba ushauri mashabiki wake nini afanye ingawa anajua watu watasema anatafuta kiki

Mr Blue amesema kuwa huo wimbo ni wake na alimshirikisha Sugu lakini anashangaa kuona Sugu katoa Verse yake na kuweka verse nyingine kisha kusema ni wimbo wake yeye na kuutolea video bila ridhaa yake

Mr Blue amesema anamlaumu kwa kushindwa kumpa taarifa n kufanya vitu bila kumshirikisha mwenye wimbo, kuthibitisha hilo Mr blue ameweka Audio Youtube na kutaka watu waone na wasikie wimbo walio ufanya na Sugu

MTAZAMO:
Niliamua kwenda Youtube kusikiliza nyimbo zote mbili, ni kweli kuwa Mheshimiwa kazingua yaani hajabadirisha kitu zaidi ya kufuta verse ya Mr Blue na kuongeza nyingine!

Anakosea sana kwa sababu Mr Blue anategemea mziki ili apate chochote yeye anakula kodi za wananchi tena nyingi tuuu bado na mziki anawafanyia dhuruma vijana wanao utegemea, hakika mshika mawili moja humponyoka.

Ni wakati wa Sugu kuamua kuchagua kimojawapo kama ni mziki au Siasa kuliko kubaki anawadhurumu vijana wanao tegemea mziki kuendesha maisha yao!

Nyimbo ya Mr. Blue hii hapa:

Nyimbo ya Sugu hii hapa:

anastahili kupelekwa jela mara moja.. jamaa ni jiziiiii..
 
Kuna Verse Blue kaimba Ukilala Umelaliwa sasa wamemlala yeye analialia yani watu wanasaka noti we umetoka nyimbo unabaki nayo gheto kwako unategemea nini hapo aandike kaumia tu kwanza kitendo cha kufanya Instagram ndo mahali pa kupeleka mashitaka haimsaidii akienda Basata ajiandae kugeuziwa kibao kama hana hati miliki
 
Kwa vyovtote vile Sugu ni mwizi na alitakiwa consent ya Mr Blue kutumia wimbo wake.. !
Mr Blue anasema huu wimbo ni wake wala si wimbo wa wote. ..
Sugu ni mkorofi na anapenda mabeef sana...
Hivi Mkuu si kuna kipindi ulikuwa unasema wewe ni Mwanasheria?
Mbona unachoakiandika hata hakiakisi kama una uelewa wowote kuhusu mambo ya Law?
 
pole yake. wakiambiwa watafute patent sijui copyright mapema wao wanaona haifai. complaining haitamsaidia.
on a positive side, version yake ni bora zaidi ya ile ya sugu. (imao)
 
Hiyo ni kawaida na naamini kuna kificho nyuma ya pazia, nakumbuka kuna kipindi Q-Chief aliurudia wimbo alioshirikishwa na JAFARAI na kukatokea sintofahamu lakini baadaye akadhihirika kulikuwa na neno nyuma ya pazia
 
Ujui lolote kuhusu mixtape usilete ujuaji kwa usilolijua... Kwenye muziki kuna wimbo, kuna remix, kuna cover, kuna mixtape... Beka alifanya cover.. Hii ya Sugu ni nyimbo na anajifanya kui own ilihali aliitwa na Blue kushiriki leo inageukaje ya kwake?

Jamaa una hasira na Sugu kama alikufanya mbaya we una Hakika gani kama aliitwa kushiriki tu ulikuwepo wakati wanafanya mapatano ya kufanya hiyo wimbo au blahblah tu...mwambie Blue atoe nyimbo nyingine tu kama mmiliki wa beat producer kakubalii Sugu afanye wimbo huo basi hamna kesi hapo siku nyingine wajifunze mana ya property rights siyo kutoa mapovu
 
Tofautisha mixtape na cover song...kwa hili sugu habebeki.
Sugu kaiba wimbo wa mr blue. Kwanza huyu jamaa (sugu) ni mnafiki na kigeugeu sana. Harakati zake za vinega/anti-virus ziliishia wapi? Aliwaacha wenzake kijiweni, yeye akala pesa za ruge..leo kachukua wimbo wa mr blue na kusema wake. Hizo harakati unazosemaga unafanya ni zipi?? Harakati za kinafiki tu.
Sugu, you're douche.
Mkuu usipanic sana..wenye wimbo wao wamekuja
MJ Records wazungumzia ukweli kuhusu wimbo Freedom ulioleta mgogoro kati ya Sugu na Mr Blue – Bongo5.com
 
Ujui lolote kuhusu mixtape usilete ujuaji kwa usilolijua... Kwenye muziki kuna wimbo, kuna remix, kuna cover, kuna mixtape... Beka alifanya cover.. Hii ya Sugu ni nyimbo na anajifanya kui own ilihali aliitwa na Blue kushiriki leo inageukaje ya kwake?
Mimi na studio yangu tumeitwa majipu na kutukanwa sana kwenye mitandao ya jamii baada ya Mr. Blue kutoa tamko lake. Hili hapa ni tamko rasmi kutoka kwetu kwa kupitia @bongofive. cc @joseph_sugu_mbilinyi @daxochali Marcochali
 
barafu umejaribu sana kueleza katika mtazamo wa nini ni nini na kwa mujibu wa nini? Hayo si ya msingi, la msingi ni kuwa Mbunge alifanya uhuni, kumess na wimbo huku unamjua mwenyewe bila kumtaarifu.

Lingekuwa jambo la heri tusingefika haa, mbona Baghdad katoa wimbo wa Mtazamo Remix na hakukuwa na matata na Prof. Jizzle, hata kama asingeshirikishwa kwenye kuimba naamini waliongea nje ya sheria na definition za "UrbanDictionary"!

Kinacholalamikiwa ni uungwana, sio kufanya kwa kufuata taratibu za Kizungu za kubabia babia!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom