TANZIA Abeli Motika (Mr. EBBO) Afariki Dunia

Mchaka Mchaka

JF-Expert Member
Jul 20, 2010
4,516
1,404
unnamed.jpg

Msaniii wa muziki wa kizazi kipya (bongo Flava) Abeli Motika alimaarufu kwa jina la Mr .Ebbo mwenye umri wa miaka 37 amefariki dunia mkoani hapa.

Msanii huyo amefariki dunia juzi saa nne usiku katika hospitali ya dream seminari inayomilikiw ana kanisa katoliki lililopo Usa river Wilalyani Arumeru mkoani hapa.

Baba wa marehemu wa msanii huyo Olais Loshila Motika alisema kuwa marehemu Mr. Ebbo alifariki dunia jana usiku kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya damu.

Alisema kuwa marehemu alisumbuliwa na ugonjwa huo kwa zaidi ya miezi tisa ambapo kabla ya kuumwa alikuwa anaishi mkoani Tanga na alipozidiwa aliletwa mkoani hapa kwa ajili ya matibabu na aliwahi kutibiwa katika hospitali nyingi ikiwemo Mounti meru, KCMC pamoja na hospitali ya kanisa ya seliani.

Aidha alibainisha kuwa marehemu Mr. Ebbo ameacha mjane na watoto watatu na anatarajiwa kuzikwa December tano katika makaburi ya nyumbani kwao Masai Camp Olorieni ndani ya manispaa ya mkoa wa Arusha.

Loshika alisema kuwa wamepokea msimba huu kwa masikitiko makubwa sana kwani marehemu alikuwa anategemewa na familia hiyo pamoja alijuwa ni kioo cha jamii hivyo familia hiyo imepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa na mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.

HISTORIA FUPI YA MR. EBBO

Jina kamili ni Abel Loshilaa Motika a.k.a Mr Ebbo, azaliwa tarehe 26 may 1974 jijini Arusha. Elimu ya msingi aliianza mwaka 1982 katika shule ya msingi kijenge baadae mwaka 1984 aliamia tanga na kuendelea na masomo katika shule ya msingi nguvumali. Nakumaliza elimu ya msingi mwaka 1988.

Alijiunga na elimu ya sekondari katika shule iitwayo jumuiya sec school. iliyopo jijini Tanga. Alimaliza elimu ya sekondari mwaka 1992. Na kwa kipindi hicho chote wakati yuko shuleni alikuwa akiimba kwaya kanisani. Kwenye kanisa la kisosora (Lutheran church) ambapo ilimsaidia sana kujifunza muziki.

Alirudi Arusha mwaka 1993 na kubahatika kupata kazi kwenye night club ambapo alitumia mishahara yake kurekodi nyimbo ambazo hazikumpa mafanikio yeyote isipokuwa zilimuweka katika ramani ya muziki. Baada ya hapo alifanya kazi ya kuandaa matangazo ya biashara na vipindi vya redio kwenye studio iliyojulikana kama Supreme recording studios iliyopo mjini Arusha. kipindi hicho kilijulikana kama “Mambo gani haya” Alirekodi nyimbo kadhaa ambazo hazikumpa mafanikio yoyote kwa mara nyingine na hali hiyo ikamkatisha tamaa kabisa.

Baadae mwaka 1995 Alipata kazi ya kuuza nguo kwenye duka la JJ BLACK lililopo jijini Arusha. Mwaka 1999 Aliamua kurudi jijini Tanga na akafanikiwa kufunga ndoa na kubahatika kupata watoto wawili Ashley na baadaye Alicia. Alianza kazi ya uwakala wa kuuza magazeti mwaka 2000.

Kazi ambayo pia haikumletea mafanikio yeyote makubwa kama alivyokuwa anatarajia, baadaye mwaka 2001 akaanzisha biashara ya kuuza mchele kwa jumla ambayo pia haikuwa na mafanikio aliyoyatarajia. kipindi hicho chote alipokuwa Tanga alifahamiana na Wasanii wa Muziki wa Bongo Fleva,Professor J na Wagosi wa kaya, na wao pia walijua kuwa Mr. Ebbo ni Msanii asilia. Baadae alijiunga na chuo cha kozi za computer jijini Tanga.

Wagosi waliporekodi wimbo wao wa Tanga kunani ,Mr Ebbo alihamasika kurudi tena kwenye Muziki na ndipo alipoandika wimbo wa kwanza wa "Mimi Mmasai mwaka 2002". Wimbo huo ukatambulisha Album yake ya kwanza kisha wimbo wa “ Fahari yako “ Baadaye mwaka 2003 akafungua studio (MOTIKA RECORDS) Ambayo ilifanikiwa kuwatambulisha wasanii kama, Danny Msimamo, Dr Leader, Mo-Kweli, na wengineo wengi , wote hawa aliwaproduce yeye mwenyewe. kama producer wa MOTIKA RECORDS.

Mwaka 2003 akarekodi Album yake ya pili iliyojulikana kwa jina la Bado Ijasungumiswa. Mwaka 2004 akarekodi Album yake ya tatu iliyoitwa Kazi gani. Mwaka 2005 akarekodi Album ya nne iliyoitwa Alibamu. Mwaka 2006 akarekodi Album ya tano inayoitwa Kamongo ambayo ndio albamu ya mwisho kwa uhai wake.
 
Oh! Mungu ampe pumziko la milele na kuifariji familia yake wakati huu mgumu
 
Ni kwa mujibu wa Radio one kumepambazuka leo asubuhi.
Habari zilizonifikia mda huu ni kwamba mwanamziki maarufu Mr ebbo aliyefahamika sana kwa nyimbo ya Mi Mmasai bwana na Kamongo umemfanya nini pegere. Amefariki usiku wa kuamkia leo, chanzo cha kututoka bado hakijafahamika.

~tHe aLpHA~
 
Back
Top Bottom