Mr Afande KOVA

Iza

JF-Expert Member
Jan 8, 2009
2,026
611
Wajameni sijaelewa huyu mkuu wa afande hapa Dar daily kideoni,mara amekamata vibaka.. ooh wamachinga...,hivi hakuna msemaji wao kwa kanda hii au ndo kale katabia akistaafu mjengoniiiiiii
 
Wajameni sijaelewa huyu mkuu wa afande hapa Dar daily kideoni,mara amekamata vibaka.. ooh wamachinga...,hivi hakuna msemaji wao kwa kanda hii au ndo kale katabia akistaafu mjengoniiiiiii

Kujifagilia muhimu babaake!
Ampe junior wake atangaze, halafu sifa kwa nani?
Mjini hapa besti, ongea na watu upate viatu!
 
Anajenga jina na kupalilia njia kwa akufanya mazingaombwe kaka kwani mifano halisi tunayo.
Mboma,Mahita,Tibaigana,wote hawa hivi karibuni wametajwa au wamenza kujitokeza kwa ajili ya kugombea ubunge majimboni kwao.Naamini naye yuko njia moja tu.
Kila siku ana kauli zake mbili ya kwanza ni kuwa msako mkali umeanzishwa kuwanansa majambazi/wahalifu hao na hatuoni matokeo na nyingine ni Ulinzi umeimarishwa jijini wakati kila siku tunapigwa na majambazi na mpk vibaka wamehamiha sarrender bridge karibu kabisa na kituo cha polisi huku mkuu ansema ameimarisha ulinzi.
 
Wajameni sijaelewa huyu mkuu wa afande hapa Dar daily kideoni,mara amekamata vibaka.. ooh wamachinga...,hivi hakuna msemaji wao kwa kanda hii au ndo kale katabia akistaafu mjengoniiiiiii
..Biashara matangazo mkuu....akipanda jukwaani siku ile utamsikia...Si mlikuwa mnaniona kwenye tuluninga twenu nakamata vibaka nafaa sana kuwa riwakilishi renu kure mujengoni!!!
 
kwa utaratibu wa polisi cheo chake kinamfanya pia kuwa msemaji wa polisi wa eneo lake

Si Kweli. Mbona IGP yeye ana msemaji wake ACP Msika.

Mbona Kamishna Znz haongei kama KOVA. In fact kipolisi anayetakiwa kuongea ni RPC na sio kamishna.

Kova anapenda sana Sifa na kuongea na vyombo habari.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom