Mpya: Ufisadi mkubwa ndani ya DARUSO

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Hii ni dhahiri kuwa kuna ufujaji mkubwa wa pesa za wanachuo wa UDSM, Kampasi ya Mlimani kupitia taasisi yao ya uwakilishi, DARUSO.
Bajeti ya DARUSO iliyokuwa Mil. 78 imekuwa supplied na mil. 26 toka Utawala wa Chuo. Baada ya Viongozi wa Colleges kuchukua 25% ya fedha iliyopo kama katiba inavyosema, kikabaki kiwango ambacho kila taasisi ingepewa 22% ya bajeti yao yote.
Cha ajabu, wadau muhimu walioshiriki katika mchakato wa kuandaa bajeti hawakushirikishwa katika mchakato wa ugawaji wa fedha hiyo ambayo ilikuwa haitoshi, shughuli ikafanywa na Waziri wa Fedha na Cabinet peke yao.
pili, yakaidhinishwa malipo ya Tsh. 700'000 kwa mtu anayedaiwa kuwa ametengeneza tovuti ya DARUSO, tovuti yenyewe ni daruso.udsm.ac.tz ambayo imekuwako tangu enzi za Kipara, na sio tovuti bali ni 'link' kwenye tovuti ya chuo na hakukuwa na mpango wa tovuti kwenye vitabu vya bajeti vya DARUSO.
Mpaka sasa, BUNGE la DARUSO limelazimika kufanya shughuli zake kwa nakisi kutokana na madudu ya Baraza la Mawaziri.
Nitawajuza zaidi kadiri nitakavyopata taarifa.
 
Piga shule mkuu achana na mambo ya DARUSO hao jamaa ni noma, jiandae na UE laki 7 kitu gani mkuu,
 
Kabla wakae wakataze mtindo mpya ya kupokea boom kupitia wahasibu wa chuo wanafanya ufisadi.
 
Kazi ipo...kumbe haya mambo yanaanzia chini.Ndio maana kina EL wanaonekan mashujaa.

yeah!
Ufisadi nilioutaja hapo juu unahusu bajeti ya DARUSO mwaka 2011/2012, bado kuna pesa ilitoka utawala kwa ajili ya DARUSO Gala mwezi wa kumi. Ikafisadiwa mpaka Waziri Mkuu wa DARUSO akanunua gari ya kutembelea, tena nimesikia kuna msaada wa fedha na vifaa ulitoka CRDB Bank PLC, huo hata habari zake hawazisemi.
 
Piga shule mkuu achana na mambo ya DARUSO hao jamaa ni noma, jiandae na UE laki 7 kitu gani mkuu,

hiyo pesa ni michango ya mifuko yetu mkuu, yet yakitokea ya kutokea hao DARUSO hawaplay them part...
Kuna kila sababu ya kukemea haya. Mimi mwenyewe ni kiongozi wa DARUSO, kama kuna mtu alikuwa wa mwisho kuulizia posho yake kwa Mhe. Spika, ni mimi. Kwa maisha ya sasa hivi, kuliko kupata milioni ya magumashi kwa kuumiza wengine, ni aheri upige kimya kwa kuwa hutaifanyia kitu, na madhambi umevuna!
 
Kabla wakae wakataze mtindo mpya ya kupokea boom kupitia wahasibu wa chuo wanafanya ufisadi.

nimesikia hilo la boom dirishani, ila nakumbuka ni mwaka wa kwanza ndio waliopokelea mu-dirisha, hawa wa mbeleni waliwekewa kwa akaunti zao kama kawaida.
BTW: Huo ufisadi ni upi unaofanywa na wahasibu,
would ya gim'me a clue?
 
hapa nimepita tuu, kumbe DARUSO kuna ulajiee,

upite salama mkuu.
Kimsingi kama una sound mind, kufanya ufisadi wa zile pesa ndogo kwa gharama ya dignity yako kwa umma wa wana-UDSM sio ishu bali ni umaskini wa mawazo. Afu hawajui kuwa kuna maisha baada ya DARUSO, sasa ivi wanajifanya wana kibri sana, ila wakitoka pale na kukonda wanakonda.
One must think carefully before fisading vile vihela mshenzi.
 
Back
Top Bottom