Mpwa wangu anatafuta mume wa kuzaa naye!

Ni mtoto wa kaka yangu, na amezaliwa na kukulia Dar, mimi sikuwa karibu naye na ni msiri sana. Nimekuwa nikizungumza naye mara kwa mara lakini sio muwazi na hiyo ilitokana na yeye kujiwekea mipaka.

Amesoma hapa nchini na nje ya nchi katika moja ya nchi za Scandinavia na sasa ni mwajiriwa serikalini. Sina uhakika sana umri wake lakini naamini ana zaidi ya miaka 40. Hivi karibuni nilishikwa na udadisi na katika mazungumzo na shemeji yangu,(mama yake) alinijulisha kwamba hata yeye na kaka yangu wanashangaa binti yao kutoolewa au hata kupata mtoto. Anakiri kwamba hawajawahi kumuona na mwanaume na hana mashoga wanaofika hapo nyumbani.

Nilimdadisi iwapo waliwahi kumuuliza kuhusu kuolewa, shemeji akanijibu kwamba waliwahi kumuuliza na akajibu kwa kifupi kwamba hajapata mume na kipata atawajulisha. Lakini tangu siku hiyo akawa hana raha na akawaambia wadogo zake kwamba wazazi wamememchoka na sasa wanamnyanyasa. (anao wadogo zake wawili wa kike ambao wameshaolewa na kuzaa)

Nilitoa wazo kwamba wamshauri japo apate mtoto, ushauri ambao aliukubali kwa mikono miwili, lakini ni nani wa kuzaa naye?

Nimeshauri hatua ya kwanza ahame hapo nyumbani akapange mbali na nyumbani ili awe huru na hapo atakuwa na fursa ya kupata mwanaume japo wa kuzaa naye. Amekubali na sasa anatafuta nyumba ya kupanga.

Lakini yuko worried kama atapata mwanaume mwaminifu ambaye sio mume wa mtu japo wa kuzaa naye tu basi. Ila swali lake aliuliza iwapo hapa nchini kuna uwezekano wa kufanyiwa IFV badala ya njia ya kujamiiana. Hilo sina uhakika nalo na ndio maana nimekuja hapa kutafuta ushauri..
King'asti , BADILI TABIA , gfsonwin , Yummy , nyumba kubwa , Nehondo , MwanajamiiOne , marrykate , AshaDii , NATA , FirstLady1 , TaiJike , na wengineo ambao sijawataja, naomba msaada wenu ili nimsaidie mpwa wangu

She can find lunatics around Kariakoo or city centre and the right time could be the late evening!!
 
mkuu umri tena wa kazi gani yeye si anataka kuzalishwa...afu kibongo hakuna IVF,deal hapa ni kujamiana tu.je nikizaa nae ntakuwa na uhuru wa kuwatembelea wanangu au ndo itakuwa basi,wakikuwa wanaambiwa baba enu alikufa mkiwa wadogo,kama ni hivyo kumzalisha tu na watoto wawe wake anatoa shingapi?mi na mbegu za pacha....nipe deal,ukimwi lazima kupima.
sawa lakini kwa njia gani, ya kujamiiana au ya IVF?
Je uko tayari kupima? (UKIMWI)
Je una umri gani?
Niko serious mkuu
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Nimesoma nimekuelewa mkubwa, ila swala linakuja kwamba atahitaji kuzaa na mwanaume wa age yoyote.,kama ndiyo.. mimi kijana na nipo tayar at any time t na nipo tayar kupima na nipo free, japo nipo kikaz singida ila kwa sasa nipo tanga ambapo ni nyumbani... Bac muulize kama yupo tayar nitamsaidia.
 
Back
Top Bottom