Mpuuzeni Selemani Kova, hajielewi yeye ni kada wa CCM au ni mtumishi wa umma

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Mpuuzeni Selemani Kova, hajielewi yeye ni kada wa ccm au ni mtumishi wa umma mwenye kufuata miiko ya utumishi.

Kwamjibu wa sheria ya utumishi wa Umma, Seleman Kova ameshastaafu kazi ndani ya jeshi la polisi na nafasi yake imechukuliwa na Kamanda Tosi(si Tosi mmjuae).

Kova alistaafu siku moja na IGP Said Mwema, "LAKINI", Kova na Kikwete wakakubalia kuwa Kova aendelee kuwepo ndani ya jiji la Dar mpaka uchaguzi upite, kwa kile kilichodaiwa "hakuna mtu mwenye uwezo zaidi yake wa kupambana na wapinzani" hivi ninavyowajuza, nikuwa Selemani Kova hana la kupoteza ndani ya jeshi la polisi, yupo tayari kufanya lolote ilimradi amfurahishe mteule wake, na uwepo wake Jeshi la polisi utakoma 25/10/2015 saa tano na dakika hamsini na tisa usiku (23:59).

Kova kwasasa hapati ushirikiano ndani ya jeshi, maafisa wa chini yake wamemtenga, amekuwa mropokaji zaidi ya Nape, wenzake wanamwita afisa habari wa Lumumba, mfano jana Kova alitoa agizo kwa RPC wa Ilala kuwa "apige" mabomu ya nguvu msafara wa Mgombea wa Ukawa Mh Lowasa uliokuwa Kariakoo, lakini kwa hekima na busara za RPC huyu wa Ilala, alifika nakuwaomba kwa heshima na hekima viongozi wa msafara ule wasitishe ziara ndani ya soko la kariakoo, na kutoa sababu ambazo kimsingi zimepokewa vema na timu nzima na kusitisha ziara,

Lakini Kova kama sehemu yakumjulisha bosi wake huku akikasirika amri yake ya kipuuzi kupuuzwa, amekurupuka na nakuitisha mkutano na waandishi wa habari kisha kutoa amri ambazo hata hajui anasimamia sheria ipi.

Tumsamehe na kumpuuza mstaafu huyu wa jeshi la polisi aliyeng'ang'ania kiti cha jeshi kwa mbeleko ya kisiasa kwani uwepo wake utakoma siku ya uchaguzi na baada ya hapo mkono wa sheria utachukua mkondo wake dhidi yake!
 
Back
Top Bottom