Mtanzania, Asante kwa mtizamo wako lakini napenda kusema kwamba maelekezo yangu ni sahihi kabisa. Na masuala yote ya immigrationa nowdays yanashughulikiwa na USCIS( zamani INA). Unaweza soma hapa kuhusu masuala yote kuhusu namna mtu anavyoweza kupoteza status yake kama Legal Permanent Reisdent aka Green Card Holder. Natumaini itakupa mwanga kidogo. :Now That You Are A Permanent Resident
Shadow,
Asante kwa link. Nimeiangalia na naona iko clear na inafanana kabisa na kwa nchi za Europe. Wache niweke hapa chini ili kila mtu asome:
You may be found to have abandoned your permanent resident status if you:
-Move to another country intending to live there permanently.
-Remain outside of the US for more than one year without obtaining a reentry permit or returning resident visa.
-However in determining whether your status has been abandoned any length of absence from the US may be considered, even if it is less than one year.
-Remain outside of the US for more than two years after issuance of a reentry permit without obtaining a returning resident visa.
-However in determining whether your status has been abandoned any length of absence from the US may be considered, even if it is less than one year.
-Fail to file income tax returns while living outside of the US for any period.
Declare yourself a "nonimmigrant" on your tax returns.
Kwa mfano kama huyo mama alirudi TZ kimoja na bwanake, automatically alipoteza hiyo green card status. Kama anataka kurudi USA kwa muda mfupi lazima aombe visa. Kama anataka kurudi kuishi kimoja USA angeweza kuomba returning resident visa na kama bado ana uhusiano na USA wanaweza kumrudishia. Uhusiano huo ni pamoja na kuwa na familia kule, nyumba nk.
Kwa watu walio wengi, wanachofanya ni kuendelea kujifanya wanaishi USA kumbe wamerudi kwao na wanatembelea USA mara moja moja. Watu wengi wanafanikiwa kwa kutumia njia hiyo. Ila tatizo lake unaweza kuingia matatizoni kwa kushindwa kulipa kodi au kushindwa kutimiza sheria zingine za nchi. Hapo ndio ukweli hujulikana na jambo dogo hugeuka kubwa.
Kwa mawazo yangu mimi naona huyo mama kwa kujua sheria aliachia hiyo green card bwanake alipopata ubunge. Ukiwa mwanasiasa au familia ya mtu anayetaka kuwa mwanasiasa inabidi uwe mwangalifu sana na haya mambo. Usije ukaishia kuwa kama yule kijana wa Mathayo ambaye aliendelea kupata mshahara kule Botswana hata baada ya kuondoka.
Hata ukiendelea kuwa na green card na mpakani wakagundua umerudi kwenu kimoja, wanaweza kuku deport hapo hapo kwa kukosa visa.
Ushauri ambao watu wengi wenye case kama huyu mama wanapewa kwenye hizi forums za immigration ni kwamba omba visa ili mkukwepa usummbufu mpakani.
Susuviri, kuhusu mahali pa kuombea, inatakiwa iwe pale ambapo unaishi. Kama unaishi hapo kwa muda mfupi ni kweli wanakuambia ukaombee kwenu. Lakini kama una haki ya kuishi hapo kwa muda mrefu, kwa mfano una visa ya kuolewa, una PR, hapo ni main residence yako nk. unaruhusiwa kuombea kwenye nchi hiyo hiyo. Huyo jamaa yako atakuwa alikuwa na visa ya muda mfupi au mwanafunzi na labda alikuwa naomba kwenda USA kwa visa ya muda mrefu, hapo watakuambia nenda kaombee kwenu.
Kwa case ya huyu mama naamini alikuwa na haki ya kuombea Dar au Nairobi. Labda kwasababu ya kuwa Arusha akaona aende Nairobi kwao na confidence kubwa, akakutana na vichaa hao wa ubalozi.
Cases kama hizi jamani ziko nyingi sana na huwa inaudhi sana. Huyu mama angelikuwa na muda angeweza ku appeal na kushinda lakini case yake ndio hivyo, kashindwa kwenda kumuona mtoto wake dakika za mwisho. Inasikitisha sana.
Wacha tusubiri ubalozi watasema nini.