Mchaka Mchaka
JF-Expert Member
- Jul 20, 2010
- 4,516
- 1,404
Akijiuzulu kweli Mizengo Pinda ATAUMBUKA!
Waziri wa Afya Dr Haji Mponda amesema yeye atajiuzulu ili kuokoa roho za watanzania ambao wataathirika na mgomo mpya wa madaktari na si kwa shinikizo! Hayo aliyasema jana usiku kwenye kikao cha dharura cha baraza la mawaziri cha kujadili mgomo mpya wa Madaktari na Manesi! Hata hivyo Mponda ametoa rai kwamba watanzania wawe makini sana na jinsi watu wanavyotumia migogoro kwa maslahi yao binafsi huku wakisababisha maafa makubwa kwa raia wasio na hatia. Na kusema kuwa kama wana taaruma wakiingia kwenye ushabiki wa siasa nchi itaingia kwenye mgogoro mkubwa na kudhoofisha ustawi wa taifa letu!
Kama ndivyo, kimbelembele cha nini! Tunawezaje kukuchukulia wewe kama reliable source bila kutaja au kuweka hata nakala ya gazeti kama umeitoa huko!! Wewe hujiulizi kwa nini threads zingine haziulizwi chanzo na yako inaulizwa na zaidi ya mtu mmoja!!! Wewe bweg e kweli!!
Niandike inasemekana wakati muhusika ndio amesema hivyo? We vipi? Au ndio mmezoea udaku! Kama wewe ni Tomaso basi subiri hadi mwisho umuone Mponda anatangaza kwenye TV kwa macho yako kesho!
Twende mbele turudi nyuma; hivi Dr. Mponda akijiuzulu kuna uhakika gani kwamba sekta ya afya itaboreshwa? Au ni kwamba tu ajiuzulu kuondoa kiwingu? Akija mwingine na sekta ya afya isiiboreke naye ataambiwa ajiuzulu? Watumiaji wa umeme tutamtaka waziri wa nishati ajiuzulu kwa kuwa sekta ya nishati si nzuri; itafuatia waziri wa elimu; kisha kwa kuwa kuna watoto wa mitaani wengi basi waziri wa watoto na jinsia naye atatakiwa ajiuzulu? Nadhani suala si waziri suala ni mfumo.