Mponda: Nitajiuzulu kuepusha vifo na si shinikizo la madaktari!

Mizizi

JF-Expert Member
Mar 8, 2008
1,275
391
Waziri wa Afya Dr Haji Mponda amesema yeye atajiuzulu ili kuokoa roho za watanzania ambao wataathirika na mgomo mpya wa madaktari na si kwa shinikizo!

Hayo aliyasema jana usiku kwenye kikao cha dharura cha baraza la mawaziri cha kujadili mgomo mpya wa Madaktari na Manesi!

Hata hivyo Mponda ametoa rai kwamba watanzania wawe makini sana na jinsi watu wanavyotumia migogoro kwa maslahi yao binafsi huku wakisababisha maafa makubwa kwa raia wasio na hatia, Na kusema kuwa kama wana taaluma wakiingia kwenye ushabiki wa siasa nchi itaingia kwenye mgogoro mkubwa na kudhoofisha ustawi wa taifa letu!
 
Hivyo vitaarifa kutoka kwenye vikao vya kahawa havina mvuto kwa watu makini. Ungeandika 'inasemekana', nani angekuuliza chanzo? Pwambafu!!

Niandike inasemekana wakati muhusika ndio amesema hivyo? We vipi? Au ndio mmezoea udaku! Kama wewe ni Tomaso basi subiri hadi mwisho umuone Mponda anatangaza kwenye TV kwa macho yako kesho!
 
Niandike inasemekana wakati muhusika ndio amesema hivyo? We vipi? Au ndio mmezoea udaku! Kama wewe ni Tomaso basi subiri hadi mwisho umuone Mponda anatangaza kwenye TV kwa macho yako kesho!
We mzizi hii ni serious issue unaleta utani basi wewe ndo waziri eee au ulikuwepo kwenye kikao. Ngeleja kakutuma utupe taarifa
 
Jiendee mwanangu. Hapa hakuna cha huruma kwa watu maana kama ingekuwapo ungechukua hatua kabla ya mgomo uliosababisha vifo. Usomi na huruma gani hivyo mwanangu? Nenda tu historia ni hakimu kama kweli unayosema yanatoka moyoni na si usanii wa chama chako na bosi wako.
 
KATUNI(648).jpg
 
Akiwa anaenda amuombe pia Blandina Nyoni na L Nkya wamsindikize!suala la uwajibikaji kwa wabongo bado ni GENI sana!grrrrrr
 
Kwa kifupi nitampongeza sana no matter what he did wrong before ..akiamua yy kujiuzuru na kumpatia taarifa rais ...maana anaweza kukatariwa kisiasa asijiuzulu ...but that should be personal too kamayy anaona ataokoa maisha ya watu basi ni vema kuliko repuation za chama au serikali....

Inaonekana hawa jamaa Dr hawatarudi nyuma..serikali dont get twisted
 
Niandike inasemekana wakati muhusika ndio amesema hivyo? We vipi? Au ndio mmezoea udaku! Kama wewe ni Tomaso basi subiri hadi mwisho umuone Mponda anatangaza kwenye TV kwa macho yako kesho!

TV ipi wakati nazenyewe sasa hivi zimejaa magamba habari muhimu hawazitangazi
 
Back
Top Bottom