mponda na nkya wanahitaji kuwajibika

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
wakuu salamu sana.
nimejaribu kufuatilia na kujiridhisha sababu za mgomo wa madaktari na kuona kuwa mawaziri hawa walikuwa na nafasi kubwa ya kuzuia mgomo huu.
tatizo la intern doctors doctors kukosa posho zao ni la muda mrefu sana,mwaka 2010 iliundwa kamati inayojumuisha wajumbe mbalimbali akiwemo dr majinge mkurugenzi wa bugando hospitail,dr lembariti kutoka muhas na wajumbe wengine wengine kutoka wizara ya afya ambao walipita hospitali mbalimbali nchini kutambua matatizo ya intern doctors.naamini ujumbe huu uliwasilisha matatizo na mapendekezo ya utatuzi kwa mawaziri hawa.mnamo mwezi wa december tulishuhudia mgogoro kati ya serikali ikiwakilishwa na wazara ya afya na interns ukiibuka.kibaya zaidi wizara ya afya ilishindwa kutatua mgogoro huu kwa umakini badala yake waliendekeza dharau na uongo dhidi ya madaktari hawa.
hii ilipelekea MAT kuingilia kati lakini kwa hulka za wizara ya afya kudharau watendaji wake tukajionea mgomo wa madaktari kuibuka.
naamini waziri mkuu alipewa taarifa potofu iliyopelekea yeye kuibuka na kauli za jazba na hatimaye mgomo mkali kutokea.

lazima tukubali kuwa kuna watanzania wengi wameathirika na mgomo huu,hivyo mwisho wa siku ni lazima mtu awajibike iwe madaktari au mawaziri.

jana mh rais amekutana na madaktari,na baada ya kukutana nao ameelewa kuwa madai yao ni ya msingi na hatimaye ameweza kuwashawishi madaktari warudi kazini.

tamko la madaktari linaonesha kuwa hawakuwa sahihi kumshinikiza rais kuwaondoa hawa mawaziri na sasa wameamua kumuomba rais kuwaondoa ili waweze kufanya kazi vizuri.madaktari hawako tayari kufanya kazi nao,huu ni ujumbe muhimu kwa rais na watanzania kwa ujumla ambao unatakiwa kufanyiwa kazi kwa haraka.
nikitafakari naona watu muhimu wizarani ni katibu mkuu hivyo kuondolewa au kujiondoa kwa mawaziri hawa hakutakuwa na athari kubwa kwa serikali.lakini kuendelea kuwepo kwa mawaziri hawa kutasababisha madhara kwa wagonjwa na serikali.kama madaktari wameheshimu ikulu na wananchi sasa ni wakati wa mawaziri hawa kuheshimu madaktari na wananchi,wanatakiwa wapime na kujiuzulu.rais waruhusu wajiuzulu kwani mgomo huu umepoteza maisha ya watanzania,pia kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea kwa mgomo baridi iwapo hawa wawili wataendelea kushika nyadhifa zao.
muda wa kuwajibika umefika mponda and nkya should go.

nawasilisha.....
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom