Mponda agoma kujiuzulu

OSOKONI

JF-Expert Member
Oct 20, 2011
10,965
5,336
Kukimbilia kujiuzulu siyo suluhu sana ya tatizo. Kwasababu kama ni hivyo, watu wanaweza kuharibu mambo kwa maksudi wakitegemea watajiuzulu na kukaa pembeni."

Alieleza kwamba hadi jana jioni, hakuwa na uamuzi wowote kuhusu hilo na alikuwa akiendelea na majukumu yake kama kawaida huku akisisitiza;

"Unajua mtu anaweza kufikiria zaidi kujiuzulu kama atakuwa amefanya au amesababisha kitu na yeye mwenyewe nafsi yake ikathibitisha hilo. "

Alisema binafsi, ameguswa na mgomo huo wa madaktari ambao umeathiri huduma za afya nchini, huku baadhi ya watu wakipata madhara zaidi ya maradhi.

Lakini, alipoulizwa kwamba kutokana na hali hiyo, haoni kwamba alipaswa kuwajibika kwa kujiuzulu kama sehemu ya kuumizwa na madhara yaliyowapata Watanzania kutokana na Wizara yake alijibu; "Naomba ni reserve(nihifadhi) kauli yangu katika hilo. Lakini, nani wanataka nijiuzulu, ni wewe (mwandishi) au nani? Maana sijasikia hilo unalosema. Nikisikia nitaamua."

Alifafanua kwamba kuwajibika wakati mwingine baadhi ya watu wamekuwa wakitafsiri dhana hiyo tofauti .

"Kwa mfano, mimi nimeguswa sana na mgomo wa madaktari, nawapenda sana Watanzania, sasa hapo kuna tofauti kidogo."

Dk Mponda alisema ndiyo maana alikuwa akifanya jitihada zote kuhakikisha anakutana na madaktari hao kuhakikisha mgomo huo unamalizika, lakini bahati mbaya juhudi hizo hazikufanikiwa haraka.

"Kwakweli nimeguswa sana na mgomo huo wa madaktari, ndiyo maana nimekuwa nikifanya kila jitihada kuhakikisha unamalizika, lakini bahati mbaya hilo halikutokea. Kwa hiyo, nimeumia sana," alisisitiza Dk Mponda, baada ya kuulizwa tena kwamba kama ameguswa ni kwanini asiwabijike kwa kujiuzulu hata kama hakutenda kosa.

Alisema anatambua umuhimu na dhana ya uwajibikaji, lakini akasisitiza kuwa "Siwezi kusema zaidi kwa sasa. Wakati ukifika nitaweza kuzungumza."
 
Hivi Dr.Mponda alishindana na nani kwenye jimbo lake la uchaguzi?au hakuwa na mpinzani?Huyu Dr bora angebaki kufanya kazi kwenye taaluma yake tu
 
Ni kweli Dkt. Mponda sio Medical Dkt. yeye ni fundi michundo ya kutengeneza majembe, matololi kule Mbeya kwa kile kilichokuwa kiwanda cha Zana zaKILIMO au ZZK kiwanda ambacho alichangia kwa kiasi kikubwa kufilisika kwake na kufa kabisa na huu udhaifu wake wa kushauri viongozi wake vibaya ameendelea na kumdanganya Pinda hadi kumpandisha hasira ya uwapa ultimutum madaktari. MPONDA TAFADHALI JIUZULU au ndio kusema kuwa huna uchungu na wananchi wako waliokupigia kura. Inabidi uwajibike Mzee usione aibu
 
Huyo lazima aondoke hata kama si kwa kujiuzuru ni kwa kuhamishwa wizara,kamwe serikali haiwezi kufanya kosa kwa kumuacha hapo,ukweli ni kuwa huu mgomo umewanyima usingizi hao wakubwa nadhani leo wamelala,kinachofanyika hapo ni kuonyesha kuwa uchunguzi ndiyo utakuwa umewaondoa na si shinikizo la madaktari,na hata hao wengine katibu mkuu na mganga mkuu wa serikali wamesimamishwa si kufukuzwa ila ndiyo mwendo wenyewe huo,wanaondoka,kuwaweka katika wizara yoyote kunaweza kuibua mgogoro na watumishi waliopo.
 
mambo ya kuhamishana wizara hatuyataki ndo yanayofanya mawaziri wafanye watakavyo wakijua watahamishwa wizara, wanatakiwa wakifanya madudu watimuliwe
 
Osokoni....mbona inasemekana Mponda aliwasilisha barua ya kuomba kujiuzulu kwa raisi ila rais akakataa?alichomwambia wewe ujui siasa acha uoga..... source Gazeti la rai la jana.
 
Hivi Dr.Mponda alishindana na nani kwenye jimbo lake la uchaguzi?au hakuwa na mpinzani?Huyu Dr bora angebaki kufanya kazi kwenye taaluma yake tu

Dr Mponda (kwa msaada wa Selina Kombani wa Ulanga Mashariki) si ndio alichakachua kura Ulanga Magharibi dhidi ya Professor Mlambiti wa SUA (CHADEMA). Marehemu Regia alikuwa anatoa updates wakati ule wa matokeo ya uchaguzi kuwa wanampiga bao Professor, naye akaenda huko kujaribu zuia ikashindikana, Professor akasusa Mponda akamwambia kama wasusa sie twala!

2015 Mlambiti atabeba jimbo lile..
 
Osokoni....mbona inasemekana Mponda aliwasilisha barua ya kuomba kujiuzulu kwa raisi ila rais akakataa?alichomwambia wewe ujui siasa acha uoga..... source Gazeti la rai la jana.
Kweli kabisa mkuu ndio kamkatalia. Jamaa alikuwa ameshafunga mabegi tayari kuondoka. Tatizo mkuu wetu hataki mtu awajibike. Mponda komaa uondoke..post kubwa sana kwako huiwezi
 
Dhana ya uwajibikaji bado haieleweki kwa viongozi kutokana na kung'ang'ania siasa kama ajir namba moja.
 
Back
Top Bottom