Mpinzani wa Prof Mwakyusa - RUNGWE aachiwa!..

tenende

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
6,511
500
Aliyekuwa Mgombea Ubunge wa jimbo la RUNGWE MAGHARIBI na mpinzani mkuu wa Prof Mwakyusa kwa tiketi ya CHADEMA, NDG YUSUFU ASUKILE, hatimaye yuko nje!..

Mgombea huyu aliwekewa pingamizi na Mwakyusa kwa madai kuwa ni mwanajeshi, na kumfanya afanye kazi ya kuwanadi madiwani wake, muda wote wa kampeni 2010.

Yusufu mwenyewe anasema aliacha jeshi kabla ya kujiunga na chuo, miaka mitatu kabla ya mwaka 2010 kwa kufuata taratibu zote.

Wiki chache baada ya kuuawa DIWANI wa kata ya Kiwira na mwenyekiti wa CCM RUNGWE, ndg MWANKENJA, YUSUFU aliwekwa ndani akiunganishwa na watuhumiwa wa mauaji hayo.

Mwaka 2011 hadi agosti 2012 amekuwa akisota ndani mpaka juzi alipotoka.Taarifa za ndani - ccm zinasema lengo lilikuwa kumzuia YUSUFU asifanikiwe kumbana Mwakyusa mahakamani kutokana na kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu uliopita.

HUU UBABE WA CCM KUBAMBIKIZIA KESI na KUWAWEKEA MAPINGAMIZI YA KIBABE KATIKA UCHAGUZI UTAISHA LINI?. NI LINI JAMAA hawa wataacha kuonea wanyonge?.
 
Pole sana kamanda waukweli hayo ni majaribu moja wapo ya kukukomaza kisiasa, 2015 Rungwe yako kijana wetu.
Na ikibidi tafuta ushauri wa kisiasa kwa Prof. Safari na Lisu ili kama kuna uwezekano wa kwenda mahakamani.
Huu mziki wa haraki YUSUPH aliuanza tukiwa chuo cha IAA na naimani hata rudi nyuma, Peeooplees pooower!
 
siasa za Tanzania ni ngumu sana! Yaani madaraka yanafanya mtu amtumbukize mtu kwenye matatizo makubwa kama kesi ya mauaji!
 
CCM mwisho wao 2015 watake wasitake. "Nguvu Tunayo.... Ari Tunayo na Sababu Tunayo" ya kuwaondoa madarakani.
 
Aiseee baba yangu akuna kiongozi wa ukweli asie kuwa na historia angalia mandela aliwekwa ndani mkuu haya yote yatakwisha 2015

nimesikitika mpaka mbege yote imekata kichwani
 
kama kuna mtu aliuawa lazima suspect wakamatwe awe ccm or chadema...hiyo sio siasa
 
Natamani hata lile gonjwa limlipue huyu mnafiki mwandosya!
Pole sana kamanda Yusuph usi hofu
2015 sio mbali huyu mgonjwa nina uhakika hata kuwa na afya ya kukimbizana na wewe!...
 
hadi maprofesa nao wanacheza rafu?

Kama ni kweli prof kahusika na njama hizo chafu basi si ajabu kuwa kuugua kwake prof hakuna mkono wa mwanadamu bali Mungu. Hakurogwa wala kuwekewa simu. Kajiumiza mwenyewe kwa matendo yake. Mungu hamfichi mnafiki na dhalimu!
 
Natamani hata lile gonjwa limlipue huyu mnafiki mwandosya!
Pole sana kamanda Yusuph usi hofu
2015 sio mbali huyu mgonjwa nina uhakika hata kuwa na afya ya kukimbizana na wewe!...
 
Natamani hata lile gonjwa limlipue huyu mnafiki mwandosya!
Pole sana kamanda Yusuph usi hofu
2015 sio mbali huyu mgonjwa nina uhakika hata kuwa na afya ya kukimbizana na wewe!...
wee nawe sijui upo bar au ndio kudandia gari kwa mbele? thread inasema mpinzani wa prof mwakyusa kaachiwa huru, sasa mambo ya mwandosya yanatoka wapi? au ni wewe ulimpa sumu?
 
Yusufu namkubali sana toka enzi za mbeso pale iaa,. Daa mi najitolea kungana nae kwenye kampeni 2015,. Karibu mtaa yusufu nafikiri sasa utakua kamanda wa ukweli
 
siasa za Tanzania ni ngumu sana! Yaani madaraka yanafanya mtu amtumbukize mtu kwenye matatizo makubwa kama kesi ya mauaji!

Hata mimi yalinikuta kama hayo 2005 tena ngazi ya udiwani ktk Wilaya ya Mbarali. CCM ni zaidi ya GUANTANAMO BAY TORTURING CHAMBER ya wapinzani wake
 
Aliyekuwa Mgombea Ubunge wa jimbo la RUNGWE MAGHARIBI na mpinzani mkuu wa Prof Mwakyusa kwa tiketi ya CHADEMA, NDG YUSUFU ASUKILE, hatimaye yuko nje!..

Mgombea huyu aliwekewa pingamizi na Mwakyusa kwa madai kuwa ni mwanajeshi, na kumfanya afanye kazi ya kuwanadi madiwani wake, muda wote wa kampeni 2010.

Yusufu mwenyewe anasema aliacha jeshi kabla ya kujiunga na chuo, miaka mitatu kabla ya mwaka 2010 kwa kufuata taratibu zote.

Wiki chache baada ya kuuawa DIWANI wa kata ya Kiwira na mwenyekiti wa CCM RUNGWE, ndg MWANKENJA, YUSUFU aliwekwa ndani akiunganishwa na watuhumiwa wa mauaji hayo.

Mwaka 2011 hadi agosti 2012 amekuwa akisota ndani mpaka juzi alipotoka.Taarifa za ndani - ccm zinasema lengo lilikuwa kumzuia YUSUFU asifanikiwe kumbana Mwakyusa mahakamani kutokana na kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu uliopita.

HUU UBABE WA CCM KUBAMBIKIZIA KESI na KUWAWEKEA MAPINGAMIZI YA KIBABE KATIKA UCHAGUZI UTAISHA LINI?. NI LINI JAMAA hawa wataacha kuonea wanyonge?.
Mtoa mada ni MWONGO NA MNAFIKI.
Na Mungu si Asamani, kikombe cha mautimlichomnyesha marehemu John Mwankenja hakika hamtakikwepa.
Tumesikia vifijo vyenu katka kusherekea "kushinda" tuhuma za mauaji ya John.
Mtadanganya mahakama lakini si wananchi.
 
Back
Top Bottom