MPINDUA GENGE

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
MPINDUA GENGE.

1)Roho ilipokusuta,mwenyewe ulijachia.
Leo weleta utata,kiti kuking'ang'ania.
Uliunguza mbatata,ile ulotupikia
Ewe mpindua genge,ni nani alokutuma

2)msomi ulie soma,elimuyo yapotea.
Tungelijua mapema,wala tusingeachia.
Kiti kwako chawa nyama,mbona unakirudia.
Ewe mpindua genge,ni nani alokutuma.

3)mbwa alie kung'ata,leo anakutetea.
Tamaa ukoipata,ufisi watuletea.
Ulipoteza karata,bora ungeijutia.
Ewe mpindua genge,ni nani alokutuma.

4)bora ungelitulia,heshima kujijengea.
Kipya ungejiundia,busara kuongezea.
Hiko kilichotokea,daima ni kujutia.
Ewe mpindua genge,ni nani alokutuma.

5)asie kuwa na haya,mzuri kuvurugia.
Kwa uliotenda haya,hakuna kunyamazia.
Siungeenda ulaya,huko kupata tulia.
Ewe mpindua genge,ni nani alokutuma.

Shairi=MPINDUA GENGE
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160.
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi .
 
Back
Top Bottom