Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,903
- 30,243
Bwana Mohamed Said
Utafiti wako una mapungufu mengi sana katika dunia hii wapo wapotoshaji na wanaotafuta ukweli; wapo watafiti wanaodai HIV na AIDS havina uhusiano wapo wanaodai Malnutrition inasababisha AIDS; hao wote wanajiita ni watafiti sawa na wewe; nimekuuliza kwanini hukumuhoji Dr. Kyaruzi alipodai aliingoza TAA badala ya kuja na majibu mbadala umerukia mambo mengine wewe ndiye mwenye mashaka na historia ya Taifa hili nilitumai ukiwa kama unavyojinadi mtafiti ungemtafuta Dr. Kyaruzi ili akufafanulie ni lini aliiongoza TAA; historia tunayoingelea ni takribani miaka 60; unafurahisha sana kuitwa yaani kuitwa scholar umeona ni jambo kubwa sana, wapo watu wanaitana masheikh huku hata elimu ya dini hawana wakati ni dhihaka za kidunia; na hasa unapoongelea kwenye watu wenye elimu duni au wasiojua. Utafiti wako ni wa kupinga kauli za wafu; mtafiti mwenye kutaka kujua ukweli huwakabili wahusika na kupata kauli thabiti; kama ambavyo uliweza kwenda kwa Sykes na ukasoma makaburasha; na kama unavyodai familia ilikunyima baadhi ya makaratasi (rejea matoleo yako ya nyuma) huo ni uthibitisho wa wazi utafiti ulishakuwa na mapungufu; Dr. Kyaruzi(R.I.P) amefariki juzi leo umekuja kuhoji kauli zake; sasa tumwamini nani yeye aliyeshiriki kwenye siasa wakati wa TAA au wewe uliyehadithiwa? Bwana Mohamed watifiti wa aina yako wapo wengi sana ni sawa na wale wanaodai Holocaust haikutokea!
Chama
Gongo la Mboto DSM
Ndugu yangu Chama,
Mbona hili la upungufu katika utafiti wangu nishalikubali?
Kazi yoyote ya binadamu haikosi upungufu.
Ikiwa ni hivyo hapana haja ya sisi kurejea tena na tena katika upungufu wa utafiti wangu au wa mwandishi mwingine.
Kuhusu kumhoji Dk. Kyaruzi si yeye peke yake ambae sikumhoji wako wengi sana sikujaaliwa kukutananao lakini nimekufahamisha kuwa nilimuomba mjukuu wake ambae ni mwandishi amfanyie mahojiano na aandike maisha ya babu yake kama Aisha Daisy Sykes alivyomuhoji baba yake Abdulwahid Sykes na tukapata kazi ambayo hadi leo tunaitumia: "Kleist Sykes: The Townsman." Kutoka kalamu ya Daisy ndipo tulipokujajua African Association iliasisiwa vipi na mengineyo katika siasa za Tanganyika kati ya 1900 hadi 1950.
Tuingie katika "Makabursha ya Sykes" ambayo nilinyimwa.
Ukweli ni huu.
Nimesoma majalada yote ya Sykes isipokuwa shajara (diaries) za Abdulwahid Sykes. Hizi sikupewa na nadhani ni kwa kuwa shajara ni kitu cha ndani mwa mtu na waliona majalada yale yalitosha kwa utafiti wangu.
Bado nashikilia kuwa shajara za Abdulwahid ni muhimu sana katika kuelewa nini kilikuwa kikipitika kati ya 1950 hadi 1954 alipokuja kuasisi TANU.
Labda kuna usilolijua ndiyo maana umekuja na neno "kuhadithiwa" hivyo sistahili kuaminiwa.
Si lazima uishuhudie historia ili uiandike.
Fanya utafiti katika hilo au waulize wajuzi watakufahamisha.
Ukiachilia mbali kuhadithiwa kwanza nikufahamishe kuwa mie mwenyewe nimeishi katika kipindi hicho lau kama nilikuwa mtoto na babu yangu Salum Abdallah alikuwa katika wanachama wa mwanzo wa African Association na TANU.
Kwa ajili hii basi familia yangu ina mpigania uhuru.
Sasa katika hali kama hii mie si muhadithiwa bali niliishi katika kipindi kile na watu waliosukuma gurudumu la historia ya uhuru wa Tanganyika. Kuhadithiwa kwangu hakuwezi kuwa sawa na yule ambae hata Sheikh Hassan bin Ameir hakujaaliwa kumtia machoni.
Tuje katika holocaust.
Napenda nikueleze kuwa katika moja ya fani zangu ni historia ya Vita Kuu ya Pili na holocaust yake khasa kipande cha Auschwitz.
Ikiwa utachukua kisa hiki cha kukataa matanuri ya janga ya Auschwitz hapa mfano huu umekuenea wewe.
Wewe ndiye unaeshughulishwa na kukataa na kuuogopa ukweli.
Sie mie.
Mimi naujua ukweli wa historia ya uhuru wa Tanganyika.
Nimeandika vitabu vitatu katika somo hilo na nimealikwa kutoa mihadhara kwingi sana ndani na nje ya Tanzania.
Marekani, Ulaya na Afrika.
Ama kuwa "scholar" siwezi kukasirika kuitwa hivyo na wala sijaomba niitwe hivyo.