MPENZIO U MKUTAPO KACHANJWA CHALE NYINGI MGONGONI,KIFUANI,MAPAJANI,nk.

Mtanganyika1

Member
Sep 13, 2011
56
5
Habari zenu wana JF
Siku zote jambo hili limekuwa likinipa maswali mengi, pale niwaonapo dada zangu unakuta amechanjwa chale nyingi mwilini hasahasa wengi nakutana nao kwenye daladala, nimekuwa nikihisi kwamba hivi ni kinadada tu ndo wanapenda kuchanja chale? au tu kwa sababu wao wanaacha sehemu za mwili wazi mara nyingi zaidi ya wanaume kumbe nao ni mabingwa wakuchanja chale?

Sina shaka kwamba wengine wanachanja chale kwa mema kwa kujitibu, kinga nk. lakini mimi binasifisi mtu ambaye nikimuona anachale mwilini ambazo zitanipa maswali huona kama ni watu wanao jishirikisha na Ushirikina tu na mara nyingi kama ni binti nilikuwa na fuatilia awe mpenzi wangu nafsi hunisuta kwamba hapo sisalama hata kidogo. Je wewe hupata hisia gani?MIE NAOGOPA.
 
Hayo ni yako BINAFISI. . .
Wengine wamechanjwa hata hawana ufahamu.
 
Labda atakuwa alikuwa na ugonjwa kipanda uso au ugonjwa wa chembe cha moyo huyo.................LOL
 
Wengi wao wamechanjwa wakiwa watoto!

Ni kweli ukifuatila wengi walichanjwa utotoni katika maeneo ambayo huduma za afya hazikuwepo, hivyo jamii hiyo ikawa inategemea waganga wa tiba za jadi ambazo suala la kuchanjwa halikwepeki,

Ila ili kujiridhisha km mhusika anajihusisha na ushirikina au lah unaweza kumwuliza hizo chale alizipataje, majibu yakiwa hayaridhishi unaanzia hapo kumwacha au kutafuta ukweli km unampenda.
 
Kumbe tupo wengi tunaoamini hivyo. Chale kwangu ni USHIRIKINA, finish..
 
waafrica tuko watu wa ajabu mno....

ukikuta wahindi wanavaa hirizi...tunaelewa ni utamaduni wao..

ukikuta wachina na wajapan wamejichora chora tunaelewa ni utamaduni wao...

lakini ukikuta mwafrica mwenzio kafanya mambo ya tamaduni zake ni 'mshirikina'...

utasema na wewe huna ya kwako ya 'tamaduni za kwenu'.....
 
inawezekana mara nyingi unakutana na wamakonde...acha kuwafikiria watu vibaya
 
Yale yale ya wanaume kutumia muda mwingi kutazama wanawake. Chale si uchawi na wengi huchanja kwa lengo la kutibu maradhi fulani yaliyowatesa hasa utotoni na ni sehemu ya tamaduni za kiafrika.
 
Haina haja ya kuchunguza sana kwani ukimchunguza sana bata hutomla kamwe. :eyebrows:
 
laabda wamerithishwa vibuyu na bibi zao, watakua wanganga wa kienyeji badae lol.
 
Back
Top Bottom