chilumendo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2013
- 2,903
- 3,080
Wanaukumbi kwanza nawasalimu nyinyi nyote mtakaosoma post yangu hii.Nirudi kwenye mada, ninaye mpenzi ambaye tumedumu naye karibu mwezi mmoja na nusu yeye anakaa kwake amepanga nyumba na mimi ninakaa kwangu sasa katika huo muda wa mahusiano kuna muda hua naenda kulala kwake kama mara nne hivi vivyo hivyo naye huwa anakuja kulala kwangu.
Sasa sababu ya kuleta post hii hapa jamvini ili nipate ushauri, ni kwamba kuna siku alilala kwangu wakati wa usiku wa manane nikajihisi nimelalia maji nilivyoshituka kumshitua mpenzi wangu kwamba haya maji yametoka wapi akasema ni yeye amekojoa kwa bahati mbaya. Nilivyombana ni kwanini akojoe kitandani badala ya chooni akasema mkojo ulikuwa umembana sasa akasema ngoja alale kidogo ndoto ikamjia anakojoa nje kumbe ni kitandani.
Nilivyomuuliza kama hali hiyo ilishajitokeza huko nyuma akasema kama miaka mitatu iliyopita tukio hilo lilijitokeza ombi langu kwenu wadau huyu ni mpenzi niliyekuwa nina mpango wa kumchumbia hivi karibuni lakini kwa tabia hii nimevunjika moyo kabisa, nilikuwa naomba ushauri katika jambo hili kama kweli linaweza kujitokeza kwa mtu kukojoa kitandani kwa bahati mbaya au hilo ni tatizo la kudumu.