Mpenzi wangu ameamua kuokoka hataki mambo ya zamani -nifanyeje

kaburunye

JF-Expert Member
May 12, 2010
672
74
wadau, mi nilikuwa na mpenzi wangu ambaye kwa sasa kaamua kuokoka na anadai maandiko hayamruhusu kufanya tena upuuzi wa zamani (yaani uasherati). Nimembebeleza na kumwambia kuwa niko tayari kuokoka ili nimpate lakini anasema hata nikiokoka uhusiano wangu na yeye hautaweza kuendelea. Na amenionya nisithubutu kuokoka kwa ajili yake na kama nataka kuokoka niokoke lakini si kwa ajili ya kumpata yeye. Anasisitiza kuwa inabidi amwombe Mungu ampe mme kutoka kwake hivyo mi ndo basi tena.

wadau hebu nisaidieni nifanyeje. Je nimuibukie huko huko church au nifanyeye maana bado nampenda na sitaki kumpoteza. :confused2:
 
Ametambua njia bora ya kutokuwa nawe tena kimapenzii..ni mstaarabuu kiasi ila mbinu yake ndo nzurii
 
Huyo hakukupenda bwana usipoteze muda; Penzi halibadilishwi na wigo wa Imani

Yeye anadai kuwa maandiko hayaruhusu uzinzi na uasherati na anasema akitaka kuolewa atamwomba Mungu ampe mme mwema. Sasa nafikiria sijui niokoke huenda Mungu akamwongoza kwangu tena. Jamani nisaidieni
 
ila namwona kweli siku hizi ni mtu wa church kweli kweli na amekuwa mtu wa tofauti. Kwani ina maana hata walokole wanafanya mambo ya nanihii
hawafanyi nanii,kanisani, ila huyo mpya mlokole mwenzake karibu watafunga ndoa sio wewe kazi yako story tu kuoa hutaki.
 
Unaposema upo tayari kuokoka ili uwe naye ,UNAJUA MAANA YA KUOKOKA?Usifanye kitu usichojua maana yake.Mie naamini kweli kashukiwa na Roho wa Bwana na wewe uendelee na maisha yako.
 
Kakaaaaaaa kapata mtu huyo hasa huko church na anadhihilisha kuwa hakupendi alikuwa anakuchuna tu.Kwa kuwa kama angekua anakupenda angekushawishi muokoke wote kisha muoane sio yeye pekee, so mpotezee utakuja juta mzee nawe muombe Mungu wako atakupatia wa ukweli.
 
Kesha mpata mlokole mwingine kanisani.mbona mgumu wa kuelewa?

Hiyo nyekundu siyo lazima iwe hivyo, Inawezekana aliona mapungufu katika maisha yake na hivyo ameamua kutengeneza na Bwana, miye nimeokoka kama miaka 7 sasa, siku niliyoamua kuokoka wadau wote walikuwa against me,including nyumba ndogo. Lakini that was my decision, kila mtu alisema lake lakini kwa kuwa niliamua mimi mwenyewe bila kuhubiriwa na mtu na ikawa hivyo, NA NDIVYO ILIVYO.
 
Ukiona kobe kainama ujue anatunga sheria...... Need I Say More?
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Au kuna kitu mlikuwa mnafanya kibaya sana mpaka mtoto wa watu kaamua kuokoka na kaona akiwa na wewe lazma mtaendelea na hiyo tabia chafu..............
 
Wokovu wa kweli na mapenzi yenu ni vitu viwili tofauti..
kama umeamua kuokoka na wewe okoka kwa ajiri yako na si kwa ajili yake
kama imepangwa muwe pamoja mtakuwa tu lakini kama sivyo shukuru mungu kwa kila jambo
 
Ushatemwa kaka yangu kiulainiiiii kama ananawa vile..........kwani kabla hajaanz akufanya uasherati hakujua kuwa mungu alikataza in the first place???? Asisingizie kisa kaokoka saa hivi eti uasherati hauna nafasi...............wewe chukua zako time asikupotezee muda mwaya isiwe tabu kabisa. ingawa bado unampenda ila utapata mwingine better than her trust me. in no time utamove on.
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Au kuna kitu mlikuwa mnafanya kibaya sana mpaka mtoto wa watu kaamua kuokoka na kaona akiwa na wewe lazma mtaendelea na hiyo tabia chafu..............

Hahahahahaaaaaaaa jamaaa alikuwa anapenda kula chipsi kuku saa tisa usiku nini?
 
Ushatemwa kaka yangu kiulainiiiii kama ananawa vile..........kwani kabla hajaanz akufanya uasherati hakujua kuwa mungu alikataza in the first place???? Asisingizie kisa kaokoka saa hivi eti uasherati hauna nafasi...............wewe chukua zako time asikupotezee muda mwaya isiwe tabu kabisa. ingawa bado unampenda ila utapata mwingine better than her trust me. in no time utamove on.

JS umepotelea wapi wewe??
 
Wokovu wa kweli na mapenzi yenu ni vitu viwili tofauti..
kama umeamua kuokoka na wewe okoka kwa ajiri yako na si kwa ajili yake
kama imepangwa muwe pamoja mtakuwa tu lakini kama sivyo shukuru mungu kwa kila jambo

Tatizo la huyu anataka ku download na kuoa hataki.Sasa anapoambiwa mambo fulani hakuna tena ndio anapagawa.Mie nampongeza sana huyo dada.
 
Back
Top Bottom