Mpenzi asiyekupenda na kukujali atakufanyia haya ...

FirstLady1

JF-Expert Member
Jul 29, 2009
16,792
5,374
.Kwanza,hataki kuambata na wewe katika matembezi na ikitokea hivyo anakuwa mtu wa masharti, mara akuambie tangulia nakuja au pengine kutembea nawe kwa umbali.

Pili,anapata kigugumizi kukutambulisha kwa rafiki zake na ndugu na inapotokea amebanwa hafikishi ujumbe kwa kiwango timilifu.

Tatu, haoneshi kubana matumizi kwa ajili ya maendeleo, kwake ni kufuja mali na anapokosa kupewa pesa ni mwepesi kulalamika na wakati mwingine kununa kabisa.

Nne, anaahirisha mara kwa mara kukutana na wewe tena bila kukueleza sababu za msingi. Au kukutungia uongo wa dhahiri na kuusisitiza bila kuona aibu.

Tano, anapokuwa akitoa maelezo ya mwanaume/ mwanamke amtakaye sifa zake zinakuwa hazilingani na wewe. Anaweza kukuambia anapenda kuishi na mwanaume /mwanamke mwenye mwili flani au mwenye elimu ya kiwango flani, sifa ambazo wewe huna!

Sita, anajaribu kukuunganisha na wanawake/wanaume wengine, yaani haoni vibaya anaposikia unataka kuanzisha uhusiano na mtu mwingine, badala yake anakutia moyo wa kuendelea na usaliti wako. Hana wivu kabisa.

Saba, hajutii anapokukosea, mwepesi wa kujitenga, kutokuzungumza nawe na mwingi wa kukusukumia makosa hata kama yeye ndiye aliyekukosea.

Nane, msambazaji wa habari za udhaifu wako na mtu asiyekusifia mbele za wenzake. Si balozi mwema kwa familia yake, haishi kukuponda mbele ya wazazi na ndugu zake.

Tisa, mwepesi wa kupokea na si wa kutoa. Mmiliki wa mali zako na mkumbatiaji wa mali zake pia. Msiri wa mipango yake na mtu anayependa kujua zaidi mambo ya kwako kuliko wewe kujua yake.

Kumi, hathamini uwepo wako na anakuchukulia kama mtu wa akiba. Hakumis unapokuwa haupo, hahisi upweke wala hakukumbuki unapokuwa mbali naye.

Kumi na moja, hakutii moyo unaposhindwa na mara nyingine hahuzuniki nawe unapokuwa una shida. Hachukui huzuni yako kama yake, hakufariji na hakusaidii kutatua kilichokwama.

Kumi na mbili, hakupi kipaumbele katika maamuzi, anajiona yeye ndiye wa kwanza na wewe ni mtu wa kufuatia hata unapopinga jambo hasitishi dhamira yake ya kutenda.

Kumi na tatu, hakusisimui katika mambo ya faragha na wakati mwingine hakuhudumii tendo la ndoa mpaka siku amependa mwenyewe. Ni mwingi wa sababu za kuchoka kusingizia ugonjwa na mwenye kuhisi kero ya kucheza nawe mchezo wa kikubwa.

Kumi na nne, hasamehi na mgumu wa kusahau. Kosa la mwaka juzi analijengea hoja leo na anaweza kulichukulia kama sababu ya kutaka muachane.

Kumi na tano, ni mwepesi wa kutoa kauli za kutengana na asiyeogopa kuachwa.

FL
 
hey

wewe first lady haya umewahi kuyapitia au?
honest mimi hayo niliyamfanyia mchumba wangu lakini bado hajakata tamaa ya kutengana na mimi ndo kwanza kanipigia na kuniuliza ndoa lini.
Hiyo kweli hatari
 
hey

wewe first lady haya umewahi kuyapitia au?
honest mimi hayo niliyamfanyia mchumba wangu lakini bado hajakata tamaa ya kutengana na mimi ndo kwanza kanipigia na kuniuliza ndoa lini.
Hiyo kweli hatari

anaonyesha jinsi gani anakupenda na huyo ndo mwanamke wa kuoa, atavumilia kila kitu shida raha , mvua na mawingi hata lije dhoruba la aina gani halimtikisi, huyo mpaka mnatembelea mkongoja utakuwa naye
 
ushauri wako unamfaa sana yaani huyo ndo yule mvumilivu hula mbivu na si mbichi tena
 
hey

wewe first lady haya umewahi kuyapitia au?
honest mimi hayo niliyamfanyia mchumba wangu lakini bado hajakata tamaa ya kutengana na mimi ndo kwanza kanipigia na kuniuliza ndoa lini.
Hiyo kweli hatari

nimeshapitia baadhi ya hayo ingawa si yote
 
copy and paste at work!
All in all thank you!

PJ unadhani mie ni mshauri wa malav dav
ni kwamba mambo haya yapo katika maisha inakubidi uyajue ,,nimesoma kwanza ndo nikakuwekeeni ubaoni ..mwenye chaki na kifutio anaweza fanya masahihiso
 
PJ unadhani mie ni mshauri wa malav dav
ni kwamba mambo haya yapo katika maisha inakubidi uyajue ,,nimesoma kwanza ndo nikakuwekeeni ubaoni ..mwenye chaki na kifutio anaweza fanya masahihiso

Nikutafutie tenda ya kitchen party mamalishe?
 
Aslam aleykhm

Kwakweli mimi ni mgeni kabisa katika nchi hii. Nitajitahidi nifanye utafiti kwani wanasema kama hujafanya utafiti basi huna haki ya kuongea/kusema.

Lakini kwa wanaojua na kutumegea namna hii basi inatusaidis kwa kiasi fulani. Laki ni wengine wanafanya hivyo ili kulipiza kisasi kwa yale walofanyiwa wao.

Salamu
 
jina lako lina maana gani mgeni?
 
Du fist lady uzi wakitambo sana miaka 9 imepita sikuhiz kuna mambo pia yamebadilika ni ngumu kujua mtu anakupenda au hakupendi
 
kama **** yake ananipa bila shida bc fresh tuu, kwanza nkitembea nae ntakosa bahati ya kuonana na watoto wakal zaid ake.
 
Back
Top Bottom