Mpendwa Lulu: Nakutumia waraka huu kwa hayo yaliyokupata!!

Kama utafanikiwa kutoka kwenye janga hili, nakusihi uwe balozi mwema wa kuwashawishi hata wenzako wenye umri kama wako waone faida za kuwa watulivu, na kuishi maisha ya uadilifu na kutii maonyo ya wazazi, viongozi wa dini na jamii kwa ujumla. Maisha ya mahangaiko yana hatari nyingi na balaa nyingi, watu wengi ambao wameshindwa kutulia na kuendesha maisha ya kiistaarabu wamejikuta wakijiingiza kwenye shida na majanga ambayo huenda yasingekuwa na sababu yatokee, hili ni muhimu sana ulizingatie maana ''mtoto wa tajiri akionywa mtoto wa maskini tega sikio" pia unaelewa wazi kuwa "mchuma janga hula na wakwao". Pole sana dada yangu, ningekuandikia mengi ila naona nisikuchoshe upumzike kwani hili nililokukuta kwa vyovyote litakuwa limekuvunja sana moyo na kukutia simanzi, kwa vyovyote vikao vya bunge lisilo rasmi kichwani kwako litakuwa likikuyumbisha kwa maoni na kukutaka utoe miongozo itakayosaidia kuondokana na hii dhahma, jitie moyo, inawezekana wanadamu wasitake kukuelewa ila nakuhakikishia hapo ulipo ukimwita mola wako kwa uaminifu yeye atakuelewa tu na anaweza kabisa kukuepusha na janga hili pole sana Lulu.
Ushauri mzuri sana huu. Kama kuna ndugu yake ambaye ni memba humu JF, basi au-print huu uzi na kumpelekea. utamsaidia kujitizama upya.
 
Huyu Lulu si ndo nilisomaga kwenye magazeti ya Shigongo kuwa yuko busy anasimamia nyumba yake kimara. Na wakaendelea kusema eti anajengewa na mbunge mmoja wa CCM mwenye umbo kuubwa. Kama ni kweli basi mbio za sakafuni uishia ukingoni. Maisha si kutegemea uzuri ndo uwin mabinti zetu hawa inabidi wajue wala si dili kutegemea mwili kusafisha jina mujini.
What goes around comes around, kwa wale wanaojua kanuni ya maumbile wanaweza kukubaliana na mimi kwamba hili janga alilipanda mwenyewe, na sasa anavuna alichopanda. unafikiri kama alikuwa anatembea na waume za watu hiyo si ni moja ya laana!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom