Mpendazoe kuunguruma leo Morogoro

Ndofu unasumbuka bure Mpendazoe hana mvuto ndio maana hata CDM wamemtosa.
Vipi kile kitabu chake kinauzika au ndio watu wasokotea tumbaku
 
Anawaambia polisi wakati mwingine wawambie mabosi wao mabomu yamegoma kulipuka ili wasiwadhuru wananchi wanaodai haki. ANAKUMBUSHIA MANENO YA SHAABANI ROBERT "unaweza kuchovya hatia ndani ya dhahabu lakini mkuki imara wa haki hauvunjiki" maana yake hata ccm wakitumia polisi na kuhadaa wananchi kwa maandamano ya chadema bado mapambano ya kudai HAKI yatashinda.
 
..anasema siasa ni vita isiyomwaga damu ndio maana tanzania iliruhusu mfumo wa vyama vingi,hivyo serikali isizuie maandamano kwa nguvu.
 
Swala la katiba: katiba ya sasa inamatatizo mbakubwa,inamapungufu inabidi ibadilishwe...katiba imempa mamlaka makubwa mno raisi, haimzuii kuchagua hata shemeji yake kuchukua nafasi kubwa ya nchi.
 
Katiba mpya inabidi impunguzie rais madaraka yake na akishindwa kuongoza aondolewe,mfano Jaji anateuliwa na raisi anaapishwa na raisi vyp raisi akiwa na kesi atamhukumu vyp?!
 
Kama katiba inasema raisi ndiye mwenye ardhi hv akiamua kuchukua ardhi yenye rutuba kwa mtu flani na ikiwa nayenyang'anya vibali vya ardhi ameteuliwa na rais itashindikana vyp kwa rais kuipora ardhi ile? Katiba ipunguze madara kwa raisi.Katiba lazima ishirikishe wana nchi anatoa mfano wa mchina "mchina anasema ukiniambia jambo flani ntalisahau ila ukinishirikisha jambo hilo sitalisahau"
 
Anamalizia kwa kuwashukuru watu wa Morogoro kwa kura walizoipa Chadema,anawataka vijana na watu wote washiriki kwenye siasa kwani kila kizazi kina zama yake' kina Nyerere walileta uhuru kizazi hiki kihakikishe kinatengeneza Tanzania tunayoitaka!
 
Huyu bwana ndo ana ugomvi na Makongoro Mahanga? kama ni ndiyo basi nimesha dokezwa kwamba Mahanga kaonekana Morogoro leo hii. Wasije kuwa wanatafutana mitaani kabla ya kukutana mahakamani au huko Ukonga.
 
Mwisho anaomba vijana waongoze mabadiriko na anamtaka kikwete aamue na aseme nchi imemshinda! Asanteni sana wakuu.
 
asante ndofu kwa taarifa,makamanda wametapakaa kuwaelimisha wananchi. Bravo mpendazoe umeamua kuwatumikia maskini.
 
Nyie mnaopinga afanyacho Mpendazoe basi nanyi hampaswi kueleweshwa zaidi kwa kua nyie ni sehem ya Magamba,anafanya kazi nzuri ya kutoa elimu ya Uraia.
 
safi kamanda kwakutujuza ya huko ,na hongera sana mpendazoe kwakuwaelimisha wananchi
 
Msijali wakuu tupo pamoja' nipo hapa Morogoro kwa ajiri ya field work, nilivyopata taarifa za kuwepo kamanda Mpendazoe nilijongea ili angalau mpate mambo ya msingi aliyoyasema kamanda wetu. HAKIKA CHADEMA ITAENEA PANDE ZOTE ZA TANZANIA KWA JUHUDI ZETU,HAKUNA KUOGOPA VIVA CHADEMA! Kwa haraka haraka tumevuna wanachama wapya wasiopungua 20! Kesho atakuwa maeneo ya nanenane hapa Moro.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom