Mpendazoe kuunguruma leo Morogoro

elimukwanza

Senior Member
Dec 27, 2010
168
23
Leo Mh Mpendazoe atakuwa akihutubia wakazi wa mji wa Morogoro katika viwanja vya Kihonda maghorofani na kesho atakuwa viwanja vya nane nane,kutokana na mtoa habari wetu pamoja na kutafuta wanachama ataeleza mpango mzima wa chama mfu cha CCJ

Nawasilisha
 
Nipo mkutanoni' watu sio wengi sanaaa, mpendazoe hajapanda kuna vijana wa chadema wanaendelea kutoa hoja mbalimbali.
 
Huyu jamaa anasumbuka bure kaishakosa ubunge lakini nani anataka mambo ya wa CCJ.
Mbendazoe kwani uwezi kuishi mpaka uwe mbunge?
 
Huyu jamaa anasumbuka bure kaishakosa ubunge lakini nani anataka mambo ya wa CCJ.
Mbendazoe kwani uwezi kuishi mpaka uwe mbunge?

Acha kuvuka mipaka wewe! HAKUNA MTU AMBAYE ANAWEZA KUMCHAGULIA MTU MWINGINE MANENO YA KUONGEA. Wewe unataka kumchagulia mpendazoe cha kuongea?
 
Mwenyeki wa Chadema ndio anaongea sasa hivi' anadai kuna diwani kata ya Kihonda ambaye ndiye naibu Mayor ameshindwa kusimama kuitisha uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa mitano tangu 2009 kinyume cha sheria.Huyu mama amebaki kuwatishia wananchi na juzi amegombana na mama mmoja Gengeni.
 
......Ametoa siku 60 uchaguzi uitishwe kinyume chake atandaa maandamano ya kumtoa huyo diwani.
 
.... Sasa mpendazoe amepanda jukwaani' anasema amani ni tunda la haki,kama kuna usawa amani itakuwepo tu,utii wa sheria bila haki ni UTUMWA.
 
Mwenyeki wa Chadema ndio anaongea sasa hivi' anadai kuna diwani kata ya Kihonda ambaye ndiye naibu Mayor ameshindwa kusimama kuitisha uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa mitano tangu 2009 kinyume cha sheria.Huyu mama amebaki kuwatishia wananchi na juzi amegombana na mama mmoja Gengeni.
Mbowe yuko huko...
 
Anaeleza kwanin alitoka ccm' ....kwa sababu ukipigania haki kwa watu wote ndani ya ccm unakuwa adui,ccm inawajali wananchi wakati wa uchuguzi tu ni chama ambacho kinanyonga haki ya watanzania.
 
Leo Mh Mpendazoe atakuwa akihutubia wakazi wa mji wa Morogoro katika viwanja vya Kihonda maghorofani na kesho atakuwa viwanja vya nane nane,kutokana na mtoa habari wetu pamoja na kutafuta wanachama ataeleza mpango mzima wa chama mfu cha CCJ

Nawasilisha

Ajitahidi kuwa mbunifu kwa kutoa "single" zingine zitakazouza, hiyo ishachuja..
 
Sababu nyingine ni 'uongozi kufanywa biashara ndani ya ccm na eti ccm ina wenyewe!
 
...anasema zana ya kujivua gamba' Kama wanaoitwa mafisadi wametajwa tu na wanatakiwa waondoke mbona K.i.k.w.e.t.e ametajwa meremeta,EPA n.k hajatoka?
 
...Chiligati alisema"kama unatajwatajwa tu kwenye ufisadi inabidi ujiondoe" Mbona kikwete ametajwa na haondoki kwenye epa,kagoda,n.k? Kumbe zana ya kujivua gamba ni usanii.
 
...Anazungumzia mkanganyiko ndani ya baraza la mawaziri huyu anasifia bajeti ya nishati na madini,wengine wanaenda Mbeya kuiponda hiyo bajeti,huyu anasema dowans walipwe waziri mwingine anasema wasilipwe...
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom