Mpendazoe akamatwa kwa kutishia bastola Shinyanga

mkuu signatute yako sio ya kujifariji zaidi?

signature yake inafaa kutumika katika harakati hizi za ukombozi wa kweli wa nchi hii iliyojaa maziwa na asali tuliyopewa na mwenyenzi mungu, lakini cha ajabu watu wake wanataabika utadhani wapangaji ndani ya nchi yao.
freedom is coming sooner than later, nahisi kama kuna uchaguzi mdogo wa urais hivi

Duh! Kumbe tukio lenyewe lilikua ni mwaka jana????...! Hii thready mbona imekaa kimalaria sugu?

Michosho,

Mpendazoe huyuhuyu Alishashikwa Dar kwa kesi ya gari akaachiwa, sasa wamebaki kutafuta makosa tu.

Yule aliyempiga OCD mbona hashikwi? Anaenda mbali zaidi na kuvunja ofisi ya umma na anapeta tuuuuuu

Where are we going.

Mwema wake up, hujasikia alarm ya kilio cha wavuja jasho?

Michosho,

Mpendazoe huyuhuyu Alishashikwa Dar kwa kesi ya gari akaachiwa, sasa wamebaki kutafuta makosa tu.

Yule aliyempiga OCD mbona hashikwi? Anaenda mbali zaidi na kuvunja ofisi ya umma na anapeta tuuuuuu

Where are we going.

Mwema wake up, hujasikia alarm ya kilio cha wavuja jasho?

Yaani kweli Tanzania zaidi ya uijuavyo!!!!!!!!

polisi wa shinyanga wana akili kama ya kondoo, mbona Robert Kisena alimpiga mateke OCD wa Maswa na hakuchukuliwa hatua yoyote?[/QUOTE

ALIDHAMINIWA NA MTOTO WA MZEE...
Incfact alimpiga mtama kituoni na mkuu wa makosa ya jinai alipoenda alisema wanafanya uchunguzi kujua kosa lilitendekaje na mwishowe wakamwachia aliepigwa mtama aamue kama atashtaki ama la! Hii ndo TZ bana

Acha kuropoka unatuaibisha, aliyekamatwa ni Fredy Mpendazoe siyo Freman Mbowe.Uwe unasoma thread kwa makini dogo.
Hengo wewe ndio usome thread kwa makini! Mwenzako kafanya comparison ya kukamatwa kwa Mpendazoe na kukamatwa kwa Freeman kwamba jeshi la polisi lina double std, rudia kumsoma kwa makini utamwelewa

Acha kuropoka unatuaibisha, aliyekamatwa ni Fredy Mpendazoe siyo Freman Mbowe.Uwe unasoma thread kwa makini dogo.

Nataka tu nikope maneno ya wanamagamba kwamba, jipime mwenyewe kutokana na comments chache tu hapa chini, tafakari kisha uchukue hatua!!

Mkuu unaonaje ukitulia ukasoma mawazo ya wenzako ukaelewa kuliko kukurupuka?
Amesema hivi, Kesi ya Mbowe ilikuwa Arusha lakini Mbowe alikamatwa Dar na kupelekwa kwa ndege Arusha.
Mpendazoe alifunguliwa kesi Shinyanga anaishi Dar lakini polisi walishindwa kumkamata, sasa kama mazingira ya Mbowe na Mpendazoe yanafanana inamaana Polisi wa Dar na Shinyanga hawawasiliani?
Ni hayo tu

msamehe bure, konyagi za tandale zinamatatizo yake.

Mkuu hata mm nimeshangaa sana hilo, kwani dsm hakuna jeshi la polisi?it simz huyo kamanda wa polisi Shinyanga ni kilaza na kusema hvyo amejiaibisha!

Hengo wewe ndio usome thread kwa makini! Mwenzako kafanya comparison ya kukamatwa kwa Mpendazoe na kukamatwa kwa Freeman kwamba jeshi la polisi lina double std, rudia kumsoma kwa makini utamwelewa

Kwamba mahaka ya arusha ilipotoa arrest warranty kwa freeman mbowe, polisi kanda maalum ya dsm walihakikisha wanamkamata mara moja na kumsafirisha kwa ndege ya jeshi chini ya ulinzi mkali hadi arusha.

Kkwamba mpendazoe amekuwa akitafutwa na jeshi hilo hilo la polisi kwa kuwa anaishi dsm pale pale walipomkamatia mbowe na kumpeleka arusha, kwa maana kwamba polisi shinyanga na polisi dsm hawana mawasiliano na hawana ushirikiano.

labda Shy na Dar ni nchi 2 tofauti.

Mpendazoe usikate tamaa saa ya ukombozi inakaribia.Polisi wanaotumiwa sasa kuna siku watagoma kutumiwa kuwaonea watanzania.

it's plain to see that all of these accusations are politically motivated,today CDM mps are setting the HOUSE on fire,kesho unaambiwa lema mwizi wa magari(car jarking),mpendazoe akamatwa shy,kesho utasikia lisu kakamatwa kwa kutema mate mjini singida,..dunia nzima inajua ccm are behind all this...no retreat no surrender...i smell blood.

JESHI la polisi mkoa wa Shinyanga leo asubuhi limemkamata na kumhoji kwa muda saa kadhaa kada wa Chadema, Fred Mpendazoe kufuatia tuhuma za kutishia kwa bastola pamoja na kumfanyia shambulizi katibu wa UVCCM kata ya Maganzo, Abdulkadiri Mohammed mwaka jana.
Kukamatwa kwa mpendazoe kumekuja siku tatu akiwa katika ziara yake ya kwanza mkoani humo tokea alipokihama chama cha Mapinduzi (CCM) na kuachia ubunge kwa kujiunga na chama cha CCJ na baadaye kukimbilia Chadema.

Mpendazoe amekamatwa wakati akiwa katika ziara ya Kichama kuimarisha Chadema katika mkoa wa Shinyanga ambapo tokea majuzi amekuwa akifanya mikutano kadhaa ya hadhara katika maeneo ya Maganzo, Kishapu, Mhunze na Shinyanga mjini.
Kukamatwa kwake kunatokana na kosa ambalo alidaiwa kutenda Oktoba mwaka jana la kumtishia bastora na kumshambulia kwa maneno Katibu wa UVCCM, kesi ambayo Mpendazoe alidai kuwa ilikwisha siku nyingi.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Diwani Athuman akielezea uamuzi wa jeshi lake alisema Mpendazoe alikamatwa kwa ajili ya kuhijiwa leo kwa tuhuma zilizokuwa zikimkabili na kisha kuachiwa huru.
“Tulikuwa tukimtafuta toka mwaka jana mwezi Oktoba, lakini kutokana na makazi yake kuwa jijini Dar tulitumia nafasi hii baada ya kuja hapa Shinyanga kumtia mbaloni kwa suala lake, na baada ya kumuhoji tulimwachia” Alisema Kamanda Athuman na kuongeza kuwa kesi hiyo ilitokana na masuala ya siasa.

Kamanda huyo akifafanua zaidi alieleza kuwa katika mahojiano yao na Mpendazoe alidai kesi hiyo imeshafutwa ambapo Kamanda wa polisi alisema kuwa kwa sasa wapo katika jitihada za kumtafuta mlalamikaji huyo ili aweze kuthibitisha kama kweli walifikia hatua ya kufuta kesi hiyo ili waweze kulifikisha suala hilo kwenye ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali kwa ajili ya hatua zaidi.
“Siku za kariburi sisi polisi tulisikia wameelewana, lakini habari hizo hazikuwa zimetufikia rasmi hapo ofisini ndio tukaamua kumwita na yeye akasema ni kweli, lakini hatutaishia hapo ni lazima pia tumwite mlalamikaji ili atuthibitishie ili tuweze kulifikisha kwa mwanasheria kwa hatua zaidi, yeye atajua kama kuna kesi ya kujibu au la” Alisema.

Hata hivyo akizungumzia kukamatwa kwake, Mpendazoe alielezea kusikitishwa na kitendo hicho cha Polisi kumkamata kwa kesi ambayo anatambua kuwa ilikwisha malizika kutokana na yeye na mlalamikaji kufikia makubaliano.
“Mimi pamoja na mlalamikaji tulikubaliana kumaliza jambo hili nje ya hamakama, na tukaandika makubaliano yetu na mkuu wa upelelezi wa mkoa (RCO) toka mwezi Machi mwaka huu, sasa nashanga leo ninakamatwa,” alifafanua Mpendazoe.
Pole Mpendazoe, hapo kwenye red mhhhhh!!

Back
Top Bottom