Mpendazoe aanika walioanzisha CCJ

Aisee sikujua kama Mpendazoe sio mtu makini kwa kiwango hiki, uchungu mwingi moyoni uliotokana na kuruka melini mapema na kisha kupotezwa na mawimbi umempunguzia busara na ufahamu.

Pole sana mpendazoe, ni ajabu sana kwa Chadema kuanza kuwataja wasaliti wa wapinzania wao CCM,eti ili CCM iwajue wale wanaowasaliti ndani yao...inatia shaka sana hii , sasa nauona kwa mbali ule ushirika usio mtakatifu kati ya mapacha watatu na chadema kama ulivyotangazwa na Nape.

Hii sio news kwa CCM, wanachotakiwa kufanya akina Sitta ni kutojibu in detail kuhusu CCJ bali kuutangazia tu umma kwa urefu kuhusu ushirika wa Chadema na Mafisadi katika kufanya lolote litakalowanusuru Mafisadi, na kisha kwinshee..
Ha ha haaa katibu mwenezi wa CCJ Nape ha haa haaaa
 
NDUGU WANAJF,
Haya maneno ya Mpendazoe yamenigusa sana kulingana na bunge lililopita jinsi lilivyopambana kuweka mambo mengi hadharani.Watanzania walikuwa wanalia siku nyingi lakini kilio chao kilikuwa hakipati wasemaji, mungu akawafungulia wachache ambao waliweza kujiweka wazi bila unafiki, bila kujificha. Mh Samweli Sitta hatasahaulika katika historia ya Tanzania kutokana na mapambano aliyopambana nayo kipindi chake cha uspika.

Sasa amefichwa kwenye shimo ambalo hasikiki tena na ameamua kuuficha ujasiri wake ambao ulikuwa ni ufunguo tuliokuwa tunauhitaji. Tunawaomba tena Mh Sitta na Mwakiembe wafikirie tena nguvu zao za upambanaji tunazihitaji bado. Umma wawatanzania na watoto wawatanzania wanawasubiri kwa hamu wasikie mpo na chama chao cha CHADEMA nguvu ya umma ili kuongeza nguvu na kusahihisha yale yote yaliyotokea yaweze kuwa katika mwelekeo unaoeleweka.

Sasa Mh Sitta umerudi tena kuwaunga mkono wale wote walitufikisha hapa, waliofanya mikataba mibovu, wanaotumia rasilimali zetu bila kujali wazawa, utendaji kazi wa watu wengine kutokuwa na mafanikio katika jamii husika nk . Umeamua kujificha na kuacha taifa lako likiendelea kushambuliwa na mchwa je ni haki? Je,Mh Sitta utasaidia vipi hili taifa lisiendelee kuzama, kushambuliwa na mchwa wakati tunajua ulishaanza na wao kwa kujua kuwa wako kinyime na wamefanya makosa waliamua kukushambulia na kukunyima pumzi kwa kuona ukweli wako.

Gazeti la nipashe linasema hivi
Alimtaka Waziri Sitta kujiondoa ndani ya CCM na kusema iwapo hatafanya hivyo, ataaminika kuwa anapigania maslahi yake na si ya taifa.

SITTA AJIBU
Waziri Sitta alipoulizwa kuhusu madai ya Mpendazoe alisema: "Sipendi kuzungumzia siasa za mtu mmoja mmoja badala ya kuzungumzia maendeleo. …waanzilishi wa CCJ wapo kwa msajili."
Aliongeza kwamba: "Kuingia au kutoka kwenye chama chochote cha siasa ni hiyari, lakini kama unavyojua, leo unaweza kuambiwa hata unataka kujiunga CUF au chama kingine lakini utakakokuwa ndiko kutaeleza msimamo wako."
Alisema uhakika wa tuhuma zilizotolewa na Mpendazoe unaweza kupatikana kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na si vinginevyo.
 
Wakati ule alibembelezwa awataje akagoma,kwa sasa ni wrong time.Ni sawa na hadithi za kufikirika.Mi namuona sawa tu huyo Nape.Je CCJ ingeandikishwa angekua CDM?
Suala si kama ccj ingeandikishwa, bali je waliotajwa walishiriki? Ukweli ndio unatakiwa ujulikane. Tusubiri reaction ya waliotajwa.
 
Suala si kama ccj ingeandikishwa, bali je waliotajwa walishiriki? Ukweli ndio unatakiwa ujulikane. Tusubiri reaction ya waliotajwa.

SITTA AJIBU

Waziri Sitta alipoulizwa kuhusu madai ya Mpendazoe alisema: "Sipendi kuzungumzia siasa za mtu mmoja mmoja badala ya kuzungumzia maendeleo. …waanzilishi wa CCJ wapo kwa msajili."
Aliongeza kwamba: "Kuingia au kutoka kwenye chama chochote cha siasa ni hiyari, lakini kama unavyojua, leo unaweza kuambiwa hata unataka kujiunga CUF au chama kingine lakini utakakokuwa ndiko kutaeleza msimamo wako."
Alisema uhakika wa tuhuma zilizotolewa na Mpendazoe unaweza kupatikana kwa Msajili wa Vyama vya Siasa na si vinginevyo.

MWAKYEMBE ANENA

Dk. Mwakyembe alipoulizwa kuhusu tuhuma hizo alikanusha madai hayo na kusema kuwa Mpendazoe aliwahi kumfuata yeye binafsi pamoja na wabunge wengine wengi wa CCM ili wamuunge mkono katika kutimiza ndoto yake ya kuanzisha chama cha siasa.
Alisema Mpendazoe walijuana kama mbunge mwenzake, na aliwafuata wabunge wengi wa CCM kutaka wamuunge mkono ili kutimiza ndoto yake, kitu ambacho si kosa la jinai.

Dk. Mwakyembe alifafanua kuwa Mpendazoe aliwafuata wabunge wengi wenye mvuto, kwani ni kawaida katika uwanja wa siasa wenye mvuto wa kisiasa kutafutwa na vyama vya siasa.
"Wanasiasa wenye mvuto hufuatwa na vyama tofauti vya siasa ili wajiunge navyo, " alisema ndivyo alivyofanya Mpendazoe na kuongeza kuwa:
"Mpendazoe alishindwa kuwashawishi wabunge hao ndiyo maana wakampuuza."
"Sisi tumeamua kubaki ndani ya chama tawala kuendesha mapambano dhidi ya ufisadi. Tutaendelea na mapambano tukiwa humu ndani na tunafanikiwa sana," alisema Dk. Mwakyembe.

Dk. Mwakyembe alisema alifuatwa na vyama vingi vikiwemo NCCR- Mageuzi na Chadema lakini akasema: "Akili ya mwingine changanya na yako."
Aliongeza kuwa tatizo la Mpendazoe ni kwamba ana papara wakati siasa hazitaki hivyo na wala siasa sio mdundiko ambao kila anayeusikia husindikiza kwa macho na kwa miguu.

MAKONDA ANG'AKA

Naye Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM wilaya Moshi Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Kilimanjaro, Paul Makonda akizungumzia tuhuma hizo alikanusha madai hayo ya Mpendazoe.
Makonda akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu, alisema kauli ya Mpendazoe ni jitihada za mafisadi kutaka kuteka ajenda ya kupambana na ufisadi hapa nchini na ndani ya CCM. Alisema yote hayo yameibuka dhidi yake baada ya kuonekana mstari wa mbele kupambana na ufisadi ndani ya CCM.

Aliongeza kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa anayo majina ya watu walioanzisha chama hicho na kuongeza kuwa ana uhakika hayumo katika orodha hiyo. Alimkejeli Mpendazoe na kusema kuwa hapo alipofika kisiasa anaweza kusema kitu chochote ili mradi ajikuze, lakini hana hoja zozote za msingi. Nape alikwisha kukanusha kuhisika na kuanzishwa CCJ. Naye Mbunge wa Lupa (CCM),

VICTO MWAMBALASWA

Victor Mwambalaswa, alipoulizwa kuhusiana na madai hayo ya Mpendazoe, alithibitisha kuwa alifuatwa na mwanasiasa huyo ili ajiunge na CCJ lakini alikataa. Alisema mwanasiasa yoyote mwenye mvuto kwa wapiga kura anafuatwa na vyama vya siasa unapokaribia uchaguzi, lakini kukubali ama kukataa kujiunga navyo ni hiari yake.

Alisema kauli ya Mpendazoe ni ya barabarani lakini ukweli ni kwamba kwa Msajili wa Vyama vya Siasa jina lake halipo kama miongoni mwa waasisi wa CCJ mwaka 2010.
 
Aisee sikujua kama Mpendazoe sio mtu makini kwa kiwango hiki, uchungu mwingi moyoni uliotokana na kuruka melini mapema na kisha kupotezwa na mawimbi umempunguzia busara na ufahamu.

Pole sana mpendazoe, ni ajabu sana kwa Chadema kuanza kuwataja wasaliti wa wapinzania wao CCM,eti ili CCM iwajue wale wanaowasaliti ndani yao...inatia shaka sana hii , sasa nauona kwa mbali ule ushirika usio mtakatifu kati ya mapacha watatu na chadema kama ulivyotangazwa na Nape.

Hii sio news kwa CCM, wanachotakiwa kufanya akina Sitta ni kutojibu in detail kuhusu CCJ bali kuutangazia umma kwa urefu kuhusu ushirika wa Chadema na Mafisadi katika kufanya lolote litakalosaidia kuwanusuru Mafisadi, mahakama ya umma itaamua in favour of either Wapiganaji au Chadema+Watuhumiwa wa ufisadi, usinipe jibu!!

Hili Neno Mahakama ya Uma kwa Mara ya Kwanza nilimsikia Mpiganaji Dr. Slaa (PhD)

Ha ha haa Ukiona CCM inakimbilia Kwa Uma Kuishitaki CHADEMA na wakati Ina Dola, Ina Polisi, Ina Mahakama ujue CCM inakufa Mzee. Kama CCM wana Uthibitisho wa Ufisadi wa Slaa Naishauri itumie Mahakama zake na Polisi wake Kumshitaki.

Ukiona CCM inakimbilia kwenye Mahakama za Uma ujue Kuna Matatizo

CCM ikisema CHADEAMA wamekwepa Kodi Maana yake CCM wanasema TRA ni MAFISADI ha ha haa
 
Baada ya Kada mwandamizi wa CDM Fred Mpendazoea kuanika siri za vigogo wa CCM Zinazowahusisha na mipango ya kuwahi kukigeuka chama chao na kuanzisiha ccj, jana Fred Mpendazoea aliwataja wahariri na waandishi wa habari ambao walikuwa ni waasisi wakuu wa CCJ,waandishi waliotajwa na Mpendazoea na vyombo vya habari wanavyotoka ni Ramadhani Semtawa(Mwananchi) ,Muhingo Rweymamu(Habari Corporation), Mayage S Mayage (Habari Corporation) .
Amesisitiza kuwa ndio walikuwa waasisi wakuu wa CCJ
 
Picha linaendelea.......................
 
Mpendazoe kaishiwa , kutueleza waanzilishi wa CCJ itatusaidia au itamsaidia nini? yeye ajipange uchaguzi ujao ili apate ubunge asije akafa na njaa
 
Kusema kweli Mpendazoe angewataja kina Nape na Sitta napema isingekuwa na political significance. Sasa ni wakati muafaka kutokana na siasa zilizopo hasa ndani ya CCM. Mbinu ya Chadema ni kuwavuruga zaidi CCM maana sasa kina Lowasa nao wamepata silaha ya kuwarudi kina Sitta na Mwakyembe. UVCCM nao wapepata silaha dhidi ya Nape amabaye tayari alishaanza kuwakoga na cheo kipya. Sasa JK anaweza "kujivua" kambi zote zinazopingana CCM bila kunyoshewa kidole na yeyote. Vita ya panzi ni furaha ya kunguru. Mpendazoe oyee!
 
Aisee sikujua kama Mpendazoe sio mtu makini kwa kiwango hiki, uchungu mwingi moyoni uliotokana na kuruka melini mapema na kisha kupotezwa na mawimbi umempunguzia busara na ufahamu.

Pole sana mpendazoe, ni ajabu sana kwa Chadema kuanza kuwataja wasaliti wa wapinzania wao CCM,eti ili CCM iwajue wale wanaowasaliti ndani yao...inatia shaka sana hii , sasa nauona kwa mbali ule ushirika usio mtakatifu kati ya mapacha watatu na chadema kama ulivyotangazwa na Nape.

Hii sio news kwa CCM, wanachotakiwa kufanya akina Sitta ni kutojibu in detail kuhusu CCJ bali kuutangazia umma kwa urefu kuhusu ushirika wa Chadema na Mafisadi katika kufanya lolote litakalosaidia kuwanusuru Mafisadi, mahakama ya umma itaamua in favour of either Wapiganaji au Chadema+Watuhumiwa wa ufisadi, usinipe jibu!!

Kwa hiyo mpiganaji ni nani?
 
Tena as team mazungumzo yawe ni jinsi ya kuidhibiti cdm na other national interest unafikiri watawaza na kutenda as a team tena? Maana hapa walipo hakuna unafiki tena lazima kundi moja linyanyue mikono juu na lingine lisamehe! Hayo yanawezekana?
Naona kama ndoto ya lowassa kusafishwa inatakaa kutimia maana tayari akina sittaa wameduimbukizwa kwenye dimbwi la matope. Ngoja tuone hiyoo muvi
 
Nataka kuiwauliza wanajamii juu ya huyu Mpendazoe, alikuwa mbunge wa CCM, akahama na kuanzisha CCJ, akahama na kukimbilia CHADEMA mnadhani ni mtu safi huyu wana CDM?

Kama alikuwa msiri wakati anahama CCM na kuanzisha CHADEMA ,akawafichia siri wenzake , wakampa mapesa aanzishe vurugu ndani ya CCM, je mnazani hawezi kufanya hayo hayo akiwa ndani ya CHADEMA?
 
Nataka kuiwauliza wanajamii juu ya huyu mpendazoe! Alikuwa mbunge wa ccm, akahama na kuanzisha ccj, akahama na kukimbilia chadema mnadhani ni mtu safi huyu wana cdm? Kama alikuwa msiri wakati anahama ccm na kuanzisha chadema,akawafichia siri wenzake ,wakampa mapesa aanzishe vurugu ndani ya ccm je mnazani hawezi kufanya hayo hayo akiwa ndani ya chadem?

RIP na Upupu wako,unapotaka kumumng'oa adui huwezi weka mambo bayana na hata sababu ya kutosajiliwa CCJ ilikuwa ni zengwe na worry ya CCM dhidi ya CCJ na Mpendazoe anasema lengo ilikuwa waje waungane na CDM ilikuing'oa CCM sasa unaposema alikuwa msiri na hata akiona CDM kama mambo hayaendi sawa anaweza kuanzisha movement za mabadiliok kupitia chama kingine amabcho ki-mtazamo wake kitakuwa na malengo sawa na anavyoamini na hii ni kwa mtu yeyote makini sio Mpendazoe tu!
 
Nataka kuiwauliza wanajamii juu ya huyu mpendazoe! Alikuwa mbunge wa ccm, akahama na kuanzisha ccj, akahama na kukimbilia chadema mnadhani ni mtu safi huyu wana cdm? Kama alikuwa msiri wakati anahama ccm na kuanzisha chadema,akawafichia siri wenzake ,wakampa mapesa aanzishe vurugu ndani ya ccm je mnazani hawezi kufanya hayo hayo akiwa ndani ya chadem?

Ur talking the obvious! Huwezi Kuwa mbunifu na wewe hata kidogo?

chadem bado kusajiliwa.

Kwa kifupi wewe ni mfukaji wa pumba. Hukuwa na sababu ya kuanzisha thread ....ungekuja hapa na kuchangia.....

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/136552-mpendazoe-aanika-walioanzisha-ccj.html

Mada ile ile sababu ya ulemavu wa akili umejikuta unarudia kitu kilichopo

Mind blindliness hii
 
Ahaaaaaaaaaaaaaaaaa dah!!nikweli sasa kww nini anabwabwaja kama mtoto ikiwa mambo iko hadharani namna hii?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom