MPASUKO mkubwa CCM, Juhudi za Kimataifa zinahitajika kukinusuru!

CCM lazima wataleta vita hapa Tanzania, nchi wameshindwa kuendesha kutoka madarakani hawataki wananchi hawawataki kwa hiyo wanachofanya ni kuharibiana. Vita njenje
 
ingekuwa inahusu chama kingine watu wengi wangeuliza source ya hbr lkn kwa vile ni ccm watu wanashangilia hatakama hbr yenyewe ni ya kutungwa.
Kweli ushabiki mwingine ni too much!
 
tuweni na amani na tumshukuru Mungu kwa hilo kuliko lingine,

CCM ≠ Tanzania
CCM ≠ Ngao ya Taifa
CCM ≠ Mama au baba wa Taifa
CCM = Mvurugo ni Kawaida yao
 
Yericko Nyerere

R U GUESSING OR SERIOUS Unaposema Juhudi za Kimataifa? What is CCM again? first PLO haiwezi kusuluhisha

Sababu ilikuwa inamsaport IDD AMIN kwenye VITA na Tanzania na pia walipeleka Wanajeshi...

ANC Umeona Haina Uhusiano na Tanzania toka Oliver Tambo aondoke... Waliopo Sasa hawana Connection

FRELIMO labda lakini watamuita LOWASSA na SITTA na kuwaambia pendaneni? kuna utajiri wa GAS?

Frelimo wenyewe sio Socialist RAIS wao ni billionea kwahiyo sijui itikadi gani itawasaidia CCM...

NDOTO NDOTO....

Mkuu labda nikusaidie, PLO ndio hutoa mafunzo ya kijasusi (green guard) ndani ya ccm,

FRELIMO ni mdau mkubwa na waasili wa ccm tangu chama hich cha Samora Macela kilipokuwa kikidai Uhuru toka kwa Mreno na hivi majuzi kilipokuwa kikipambana na RENAMO

ANC hiyo ndio muhimili wa usaidizi kwa ccm, na mtu muhimu sana kwa ustawi wa kijani, ANC imekuwa ikisaidia kutoa mafunzo kwa ccm ya kuendesha siasa za kileo hasa za KUCHAKACHU matokeo ya chaguzi!

Kwaujumla hapo vyama nilivyovitaja ni ROHO ya kidiplomasia ya ccm achilia mbali chama Yujing Tao wa CHINA
 
Last edited by a moderator:
Huo msaada wa hivyo vyama vingine ni wa aina gani?watakuja kuwaamulia ccm nani awe mgombea urais?
 
Mkuu,

Hoja nyepesi sana hiyo, haiwezi kusababisha mpasuko unaousema. CCM inajipanga sasa hivi, ndo maana wapinzani kwa nje mnakikuza hata kidogo kinachotokea chamani. poleni sana

sitilii shaka mipango yenu ya kukinusuru chama, mi ninachokiona ni uroho wa madaraka ndio unao watawala. Utamwaga ugali mwenzako anamwaga mboga!
 
Mleta mada ametafsiri vibaya uhusiano wa Lowassa na Kikwete. Hayo anayosema yanaweza kuwa si kweli kama tutazingatia yafuatayo:

Mosi, Lowassa aliwahi kusema urafiki wake na Kikwete haukuanzia barabarani na hivyo hauwezi kuvunjwa na vyombo vya habari. Kikwete hakukanusha kuthibitisha kuwa ni kweli.

Pili, Lowassa alibeba dhambi zake na za Kikwete na hivyo Kikwete kulamizika kumlipa malipo ya ustaafu wakati alitimuliwa na kashfa yao ya Richmond.

Tatu, Kikwete alifanikisha dili lake na Lowassa kwa kuruhusu Richmond iuzwe kwa Dowans na Dowans iuze mikangafu yake kwa Tanzania.

Nne Lowassa na Kikwete ni wana-CCM chama kinachosifika kwa unafiki na ugeugeu.
Tano, Lowassa hawezi kulazimishwa na usalama wa taifa maana iko chini ya swahiba na pacha wake Jakaya Kikwete.

Sita ikichukuliwa kuwa Kikwete na Lowassa ni wasanii wa kawaida, wanachofanya ni kupima upepo na kuwachanganya wadanganyika.
 
Ukweli husemwa:


Mpasuko mkubwa?. Ndiyo inawezekana.

Juhudi za kimataifa?. Mmh, Hapo umechemsha na tukubali kutokubaliana.

Watakaoifuta CCM katika uso wa utawala ni sisi wananchi na siyo wanachama wa CCM.

Makundi katika chama chochote cha siasa huwa yapo tu pamoja na chama kuwa na wanachama wenye itikadi moja.

CCM ni chama kikongwe hapa Afrika na kimeweza kukabiliana na changamoto nyingi toka kilipoanzishwa na katika changamoto hizo kimeweza kupata uzoefu wa kukabiliana nazo.

Ikumbukwe kuwa, haijatokea kwa chama kilichoko madarakani kusambalatiswa na wanachama wake bali ni wanachama 'wakorofi' kusambalatishwa na Chama ama kwa kuvuliwa uanachama au kuwekwa kiti moto. Mifano ni mingi tu na mfano wa karibuni ni pale ANC ilipomtupilia mbali Thabo Mbeki katika Chama.

Nafikili umegusia nguvu ya CCM katika wanachama wake pale uliposema Lowasa alilazimishwa na usalama wa Taifa kwenda kwenye tafrija ya ugawaji wa ng'ombe na akatii amri.

Tusikae hapa na kujipa moyo kama CCM inasambalatika kama hakutapatikana wa kukinusuru kutoka nje. Hii inakuwa kama maneno ya kwenye kahawa katika usindikizaji wa masaa.
 
chaguo la kikwete ni membe,wakina sita na mwakyembe wanakundi lao,lowasa ana nguvu sababu ya busara zake pesa zake ni mwanzilishi wa wanamtandao hivi wakuu wa wilaya wapya ancontact nao wote kutumia intelijensia dhaifu na bwana rostam anatumia pesa za saudia kuwamaliza akina membe na sita patamu hapo big up lowasa myalia sana wapambe wa bwana dhaifu.
 
Kama jungu Nyerere umelipika. hivi Kampeni za Urais zinaanza kabla hata ya kuwachagua viongozi wapya wa CC na NEC, kwanini usisubiri Mkutano Mkuu wa Taifa CCM mwezi ujao watakaochaguliwa ndio watakaompitisha Mgombea Urais hapo 2015 kwa sasa ni Majungu kusema Lowassa, Membe au yoyote kabla ya wanachama wenyewe kuwapitisha, hivi vihabari vya nje ni sawa na kelele za mlango haziwezi mkosesha usingizi mwenye Nyumba
 
Mipasuko yote ni upepo tu!!

MPASUKO wa dhati na Tunaougojea kwa manufaa ya Taifa Letu na wenye meno ya kumyoosha hata Joyece Banda wa Malawi ni Huu!

Kuna CCM mbili tu zenye kueleweka.

1. CCM AZIMIO LA ARUSHA CCM AA .....(CONSERVATIVE CCM) NA
2. CCM AZIMIO LA ZANZIBAR CCM AZ ... (THE LIBERAL CCM)

Huu ndio mpasuko wenye tija.

ukiwaona wanatunishiana msuli huku wote ni waumini wa CCM YA ZANZIBAR jua hao hawana lolote ni wasinii kama azimio la zanzibar lilivyo la kisanii.

ukiwona wanapingana na CCM YA ARUSHA ... JUA KUWA BILA CCM YA ARUSHA KUZALIWA TENA ccm itakuw aimekwisha kabisa.

ANGALIZO.


1.
CCM YA ARUSHA IKIFUFUKA ... NA KUJIPAMBANISHA NA CHADEMA ... CHADEMA ITABIBI WAFANYE KAZI YA ZIADA KUBWAGA.

2. CCM YA ZANZIBAR IKISHINDA ... NA KUPAMAMBANISHWA NA CHADEMA ... HAIKIKA CHADEMA INACHUKUA NCHI KIRAHISI.

3. CCM YA ARUSHA NDIO ILIMTIMUA ID AMNI NA NDIO YENYE UWEZO WA KUMSHIKISHA BI JOCE BANDA WA MALAWI ADABU NA KUITAMBUA TANZANIA KUWA SIO YA KUCHEZEA.
.




 
Azimio Jipya,

Yanaukweli kabisa hayo uliyoyasema mkuu!

Tatizo moja ccm wao wanalishwa na mapokeo na kuamini kuwa wanatakiwa kwenda kisasa hata kwa kuumiza nyoyo za wanachama!

Kwa mukthada huo, makundi hayo hasa lile la CCM AA ni vigumu kuamka kwakuwa ili lisimama linahitaji huruma na fadhira za CCM AZ, hasa ikitajwa na kuaminika kuwa CCM AZ ndio iliyoshika uchumi wa CCM asili!
 
Last edited by a moderator:
Me hilo halininyimi usingizi,,,,,sinufaiki na chama chochote kwa namna yeyote,,,,,,,,

Kiufupi nchi hii walipotaka ifike imefika, nchi haitawaliki, watanzania wamefundishwa kulalamika kwa kila jambo, hata lile ambalo ni majukumu yao ya msingi, watanzania hatufanyi kazi, tumekalia siasa uchwara tu! hazina tija hata kidogo, viongozi wa kisiasa leo anasema hili kesho anakana hakusema au hakuwa na maana inayosemwa ili mradi mambo ni vululuvululu...." kuwa kiongozi mwadilifu Tanzania sasa imekuwa mtihani!
 
Back
Top Bottom