MPASUKO mkubwa CCM, Juhudi za Kimataifa zinahitajika kukinusuru!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,270
Hali ndani ya ccm imezidi kuwa mbaya na ambayo haijawahi kutokea tangu kuundwa kwa chama hiki tangu mwaka 1977,

WAHAFIDHINA ndani ya ccm wameapa kuwa hawapo tayari kuona ccm ikishindwa Uchaguzi ujao, na wapo tayari kufia miguuni kwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Tz,

Taarifa za ndani na zakuaminika zinasema mpasuko wenye kutishia hata usalama wa nchi yetu,umeanzaa baada ya Lowassa kulazimishwa na wanausalama kuhudhuria UGAWAJI wa ng'ombe pale Monduli ulioratibiwa na kusimamiwa na Rais Jakaya Kikwete!

Kimsingi inasemekana Lowasa alishaapa kutokaa meza moja na JK, hivyo kitendo cha kulazimishwa kuwepo na kuamuliwa kutoa kauli ya kumsifu jk imemkera sana yeye na wanamtandao wake ndani ya ccm na wamepanga kufanya UASI mkubwa ndai ya CHAMA na ikibidi wanasema (nje ya chama)!

Wakati hilo likijiri kambi ya Samweli Sita nayo imechukizwa sana na hatua ya JK kukaribiana na Lowasa kwani wanasema kitendo cha JK kuwa (maadui) kilikuwa kikiwasaidia wao kujijenga kisiasa na kutimiza malengo yao ya Urais 2015

Hawa nao wanatafakari hatua za kuchukua na inatajwa kuna vikao vya siri vimekuwa vikifanyika Tabora na Masaki vikiratibiwa na wanamtandao wa Sitta!

Kundi lingine ni la Waziri Membe,

Kwanza Membe amekasirishwa sana kuona wanaccm wanamchafua huku mwenyekiti jk akiacha tu hizo rafu bila kupuliza kipyenga, amefika mbali na kusema sasa anajibu mapigo,

Wakati kundi la mwishoo ni la vijana, likiongozwa na Januari Makamba, Emanuel Nchimbi, Nape Nauye nk

Hawa wamestushwa sana na mwenyekiti kuwageuka nakuanza kuwa karibu na Lowasa wakati alishawaahidi kuwa sasa ni zamu ya vijana,

Hili nalo linajiapiza kuwa bora chama kife lakini sio kuongozwa na wazee kwakuwa wameongoza kwa miaka 50 lakini nchi inakuwa kwa kurudi nyuma,

Wakati kundi hili likisema kwa manung'uniko, linaonekana kama linasalitiana kwakuwa baadhi yao wameanza kupingana na kudharauliana wao kwa wao, na wengi wakimtupia lawama Januari na Nape kwa wamekuwa wakijipendekeza kwa Mwenyeti badala ya kujenga umoja wao!

Wadadisi wa siasa za ccm wanasema kuwa hali iliyopo haiwezi kutatulika bila juhudi za vyama marafiki vya nje, kama ANC afrika Kusini, PLO cha Palestina, Frelimo cha Msumbiji,nk

Haya ndugu zangu mungu aepushilie mbali Chama hiki kife bila kurusha miguu maana kitatuingiza kwenye matatizo makubwa!
 
Kwisha kazi ccm imefikia tamati hapo hakuna atayeweza tena kukirudisha
 
Sikio la kufa halisikii dawa! Kama falme zilivyoinuka na kuanguka, anguka kuu la ccm limekaribia! Chama kimekiuka miiko, kimewasahau wakulima na wafanyakazi, kimekumbatia mafisadi, na kinazima kila njia ya sauti ya wanyonge kusikika. Huwezi kujenga nyumba imara yenye msingi dhaifu!
 
Me hilo halininyimi usingizi,,,,,sinufaiki na chama chochote kwa namna yeyote,,,,,,,,
 
Inakuwaje mtu analazimishwa kugawa Ng'ombe na akakubali? Halafu huo si mchezo wa siasa tu kama michezo mingine?
 
Hii ni habari njema kwa wapinzani wa ccm! Ni wachache walio makini watakaojighulisha walau kuhoji chanzo cha habari yenyewe achilia mbali kutafuta usahihi wake! Ingawa imekaa kishabiki sana na kikutungwa tungwa!! Sikatai mpasuko ndani ya ccm hilo halina shaka, ila je, ni ya kweli haya? Ikiwa jibu ndiyo basi ni wakati wa watanzania kusahihisha makosa yaliyoligharimu taifa kwa miaka 50. Wacha tuone!!!
:ranger:
 
Mkuu,

Hoja nyepesi sana hiyo, haiwezi kusababisha mpasuko unaousema. CCM inajipanga sasa hivi, ndo maana wapinzani kwa nje mnakikuza hata kidogo kinachotokea chamani. poleni sana
 
Yericko Nyerere

R U GUESSING OR SERIOUS Unaposema Juhudi za Kimataifa? What is CCM again? first PLO haiwezi kusuluhisha

Sababu ilikuwa inamsaport IDD AMIN kwenye VITA na Tanzania na pia walipeleka Wanajeshi...

ANC Umeona Haina Uhusiano na Tanzania toka Oliver Tambo aondoke... Waliopo Sasa hawana Connection

FRELIMO labda lakini watamuita LOWASSA na SITTA na kuwaambia pendaneni? kuna utajiri wa GAS?

Frelimo wenyewe sio Socialist RAIS wao ni billionea kwahiyo sijui itikadi gani itawasaidia CCM...

NDOTO NDOTO....
 
Last edited by a moderator:
Mbona hili umelisahau kwa upande wazanzibar kuhusu mfumo wa muungano mbona watu vidole machoni hawatambuani yaani raha kama nini chama hiki kinakoelekea
 
Siasa ni mchezo mchafu, hivi kwa shughuli ya kugawa ngombe kwa nini asingeenda waziri mkuu au waziri wa mifugo, au Wassira au hata Lukuvi? Hivi ni kwa nini Bwana Mkubwa anaingizwa kwenye mitego ya kiaina hivi?

Kama wanakufa wakafie mbele ya safari, hii Tanzania ni yetu sote sio ya wajanja wachache mafisadi.Hatuwezi kuendelea kuwa waoga kwa ajili ya magamba, mbona wao wanapofisadi nchi sio waoga?

Hata wakija vijana,embe halianguki mbali na mti na mtoto wa nyoka na nyoka, CCM wamepoteza mwelekeo na uhakali wa kuongoza nchi.
 
Heading na Content tofauti kabisa...ebu pitia hotuba ya Lowassa wakati anaongea na waandishi wa habari anakuambia yeye na JK hawakukutana barabarani...nimefungua hii thread nikidhani nakutana na habari ya maana kumbe ni Vapour.
 
Bora cCm kife kabla ya 2015 maana hata raia wamesikika wakisema

''...bora kuishi na vVu kuliko kuongozwa na cCm...''{mwisho wa kunukuu}
 
Liwalo na liwe tena ikifa kaburi lake liwe futi 12 kama tunavyozika wachawi kwetu!The country is in shamble and disorganised with
Widespread lack of patriotism bse of CCM
 
Uzuri wa Lowasa anajua kucheza na mbongo za magamba! Muda si mrefu atawaformat vichwa vyao na watasahau yote yaliyopita maana watayaita yaliyopita si ndwele.
Na watakapo yaita kuwa si ndwele m4c itakuwa imezibua shampeni na kizibo kinadondokea magogoni.
 
Heading na Content tofauti kabisa...ebu pitia hotuba ya Lowassa wakati anaongea na waandishi wa habari anakuambia yeye na JK hawakukutana barabarani...nimefungua hii thread nikidhani nakutana na habari ya maana kumbe ni Vapour.
Walikutana wapi? Au guest house
 
Back
Top Bottom