MPANGO wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia (REDET)

MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,565
836
Na Edson Kamukara

MPANGO wa Utafiti na Elimu ya Demokrasia (REDET) umesema kupanda kwa gharama za maisha, huduma mbaya za jamii, rushwa, viongozi wabovu, ufisadi, ukosefu wa ajira, kudorora kwa kilimo na mikataba mibovu ndiyo mambo yanayokwamisha utendaji wa Rais Jakaya Kikwete.

Hata hivyo utafiti huo ulibainisha kuwa Watanzania wengi waliohojiwa wanaonekana kuwa na imani na Rais Kikwete kuliko Baraza lake la Mawaziri na chama chake cha CCM.

Mtafiti Mkuu wa REDET, Dkt. Bernadeta Kiliani na Makamu Mwenyekiti wa mpango huo, Dkt. Benson Bana waliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam jana kuwa matokeo hayo ya utafiti wa Novemba 2008 yalijumuisha mikoa yote ya Tanzania kwa kuchagua wilaya moja kila mkoa na watu 50.

Dkt. Kiliani alisema kati ya waliohojiwa asilimia 39.5 walisema wanaridhika sana na utendaji wa Rais Kikwete, asilimia 39.0 wanaridhika kiasi huku asilimia 19.3 wakisema hawaridhiki na utendaji.

Alisema takwimu hizo zikilinganishwa na utafiti wa Oktoba 2006 na Oktoba 2007 kutathimini uongozi wa Rais Kikwete tangu aingie madarakani ni kwamba asilimia ya wanaosema wanaridhika sana na utendaji wake inapungua kutoka 67 mwaka 2006 hadi 44 mwaka 2007 kufikia 39.5.

Utafiti huo unabainisha kuwa sababu zilizotolewa na watu ambao hawaridhiki na utendaji wa Rais ni kushindwa kwake kuboresha maisha, kuchagua viongozi wasiofaa, kushindwa kupambana na rushwa na utafiti ulifanywa kipindi vigogo wakipelekwa kortini kwa tuhuma za wizi wa fedha za EPA.

Dkt. Kiliani alisema wahojiwa wengi waliotoa tathmini yao ya utendaji kazi wa Serikali na baadhi ya taasisi zake, kiwango cha kuridhika sana kilikuwa chini ya asilimia 40 kwa kila asasi iliyokuwa kwenye orodha.

Katika orodha hiyo Bunge liliibuka kidedea kwa asilimia (32.7), Serikali za mitaa (29), jeshi la polisi (24.3), Mahakama(22), Baraza la mawaziri(18) na Taasisi ya Kupambana na Kudhibiti Rushwa (TAKUKURU) ikiburuza mkia kwa kuambulia asilimia 13.4 tu.

Alibainisha kuwa watu wengi bado hawaridhiki na jinsi Serikali ya Rais Kikwete inavyoshughulikia matatizo kama migomo ya wanafunzi vyuo vikuu, migomo ya walimu, suala la EPA na sakata la OIC.

Katika suala la imani kwa viongozi wa Serikali, Rais Kikwete aliongoza kwa kuwa na asilimia 50.3 akifuatiwa na Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda 54.6, Makamu wa Rais Dkt. Ali Shein 48.5, Mkuu wa Mkoa husika 36.3 na Mbunge kwenya jimbo 32.2 .

Kuhusu utendaji wa Rais Amani Karume na Serikali yake Visiwani Zanzibar utafiti unasema kuwa ingawa katika matokeo ya mwaka 2006/2007 alionekana kushuka, katika matokeo ya 2008 amepanda kidogo kutoka asilimia 35.5 hadi 44.
 
Back
Top Bottom