Madela Wa- Madilu
JF-Expert Member
- Mar 24, 2007
- 3,062
- 731
View attachment 1323
sijaelewa umekusudia kuua kivipi?
hawa wanafunzi wanafanya mitihani. na rangi ya njano level nyengine na hao wengine.
kurahisisha usimamizi wamewekwa pamoja, tatizo liko wapi?
kwani form four na form six si inakaribiana na hivyo wengi kwenye hall?
Nakubalina kabisa huu ni mpango wa siri wa SISIEMU wa kujenga Taifa la Wajinga.
Nani kakwambia wanafanya mtihani?
Sawa, kama wanafanya mtihani so what? Ndiyo wakae chini?
"kwani form four na form six si inakaribiana na hivyo wengi kwenye hall?" Hii sentensi haina maana yeyote.
Wana JF.
Kama mtu huwezi elewa kinachoendelea kwa kuiangalia picha hiyo, basi ni vigumu sana kuelewa kwamba Tanzania si nchi ya Viwanda.
Pia kwa mtaji huo ni vugumu kuelewa tofauti ya mshona Viatu(kilabata), mpinga rangi viatu na mtaalamu wa kufua chuma cha pua wa kule Korea ya kusini au Japan.
Pia kushindwa kuisoma na kuitafsiri picha hiyo ni dalili moja wapo kwamba somo kwamba Tanzania ni iko Dunia ya tatu katika mizania za maendeleo na nchi kama Sweden Japan na Amerika ziko dunia ya kwanza.
Ni masikitiko makubwa kabisa kuona mtu anaweza kunena maneno makuu katika imani ya dini kampeni za kisiasa na hata katika mkusanyiko wa harusi,lakini mtu huyo huyo hawezi kutambua dalili muhimu za udumavu wa elimu.
Mungu alitupa akili, lakini utashi wa kuzitumia akili katika namna nzuri alituachia wenyewe.
Kwa uhodari wa kutumia shoka wengine huamua kukata vichwa vya watu.
Kwa uhodari mahesabu wengine huamua kupika mahesabu na kuiba.
Kwa uhodari wa tiba na utatifi wengine huamua kuanzisha magonjwa mapya.
Kwa uhodari wa kuongea na kushawishi wengine huamua kuupeleka umma wote kwenye matatizo mkubwa ya kiuchumi.
Bado ni utashi wa bin adam kutumia akili aliyo pewa na Mungu katika mwelekeo ulio sahihi.
Katika nchi iliyopata uhuru zaidi ya miaka 47 iliyopita, mwanafunzi katika darasa la shule yeyote ile katika kijiji chochote kile hastahili kukaa chini wakati akifundishwa au akifanya mtihani au akisubiri mwalimu aingie darasani.
Miaka 47 ni mingi ya kutosha kupanga mipango sahihi ya elimu na kuacha upuuzi na utani kama huu tuuonao katika picha.
Juzi hapa tumeambiwa na Mzembe mmoja kwamba Tanzania INAPAA.
Leo hii shule iliyopo umbali wa chini ya Maili 5 kutoka Ofisi na nyumbani kwa Juha yule kuna Wanafunzi Jalo wamekaa chini darasani wakifundishwa.
Eti inapaa!
Kumradhi, nashindwa kuelewa maana ya kupaa ni nini?
MH yule pengine alifikia hatua ya kusema Inapaa kwa sababu yeye binafsi ametoka mbali na hakutegemea hata siku moja kufikia hapo alipo fikia.
Fikiria,Kutoka kufunga Lubega hadi kuvaa suti pande mbili na mjusi juu na zile suti za nipishe nijambe. Kubadili magari kama nguo za ndani, kumechisha gari na nguo nk.
MH huyu kweli aliona ni maendeleo makubwa yanayo patikana mawinguni tu kwa hiyo ni lazima Tanzania inapaa, asitambue kwamba yeye pekee anapaa akizungukwa na nzi wa kizungu.
Kama hatuwezi kuelewa matatizo ya elimu nchini Tanzania au tunaelewa na kuyapuuzia kwa sababu wadogo zatu wanasoma Bunge Primary school kuliko na madawati ya ziada, basi ni lazima tuelewe kwamba majadiriano juu ya mambo mengine yote yaliyo baki ni mazungumzo baada ya habari. Safari nyingine tukifungua enternet ni bora tulog kule whitehouse.com
Elimu ni Ufunguo wa maarifa yote duniani.
Ndiyo maana wenzetu wote wa dunia ya kwanza hawana mchezo wala ujinga katika masuala ya Elimu.
Wenzetu elimu wanaiangalia yote kwa ujumla wake, kuanzia kindergarten mpaka University.
Kuanzia kusoma Historia za utafiti wa zamani mpaka kufanya utafiti mpya hapa duniani na katika anga za juu.
Nina shangaa kuona mtu na akili zake timamu anashindwa kuelewa tatizo lililo wazi kabisa la watoto wa shule kukaa chini wakati wa kusoma.
Pengine mtu mwingine anaona tendo la wanafunzi kukaa chini wakiwa masomoni ni kawaida, hasa akizingatia jadi yake au utamaduni wa imani yake au vyote.
Lakini kwa utamaduni na imani hiyohiyo hata sijaona imani hiyo ya kukaa chini ikihamishiwa ikulu au kwenye Bunge.Kwenye maofisi yote kila mmoja nahusu utamaduni wa kukaa juu ya vipande vya miti kaa kima.
Ninashangaa kwa nini mtu mwenye akili timamu anashindwa kuelewa kwamba kuna jambo kubwa lisilo la kawaida linaendelea katika mfumo wa siasa na uchumi wa Tanzania endapo miaka 47 baada ya Uhuru watoto wa shule bado wana kaa chini sakafuni.
Tena si watoto wa shule za msingi tu, hata Univeristy of DSM wanafunzi wana kaa chini na wakati huo huo MH Kikwete anapita kila nchi kwa mbwembwe kuomba fedha za kujengea chuo kingine wakati tulicho nacho darasa moja lina watu 1000 katika chumba maalumu kwa wanafunzi 150.
Siyo tu wana kaa chini wengine wanachungulia madirishani wakiwa nje ya chumba cha darasa.
Tumeita mshauri toka Japan aje atushauri namna ya kuukata kama wao wajapan.
Ushauri wa mjapan huyu ukifanyiwa kazi watu wa kuja kuutekeleza kwa vitendo ni hao jamaa waliokaa chini. Sijui ni kwa kiwango gani watu waliosoma katika mazingira hayo ya kukaa chini watakuwa tayari kuyafanyia kazi maagizo ya huyu mjapan.
Kuna watu wanaandika maneno hapa mpaka unawahurumia, na hata kukufanya uamini kwamba pengine mawazo waliyo yaandika hayakutoka kwenye bongo zao ila yalitoka kwenye misuli ya mikono yao.
Sijui ni uwezo wa kufikiri umegonga Glass Ceiling au ni ushabiki wa kisiasa uliovuka mipaka?
Sijui ujasiri wa kutetea na kuona fahari kwamba wanafunzi katika picha wamekaa chini kinyume na madai ya viongozi wa chama na serikali unatoka wapi?
Hata ukiwa na Roho mbaya kuliko ibilisi mwenyewe, katika damu yako walau kutakuwa na chembe za ubinadamu.
Kukauka kisabuni na kushindwa kuona udhaifu wa chama tawala na serikali yake wa kushindwa kuimarisha elimu sambamba na mahitaji ya watanzania ni ugumu unao karibiana na uhaini.
Mtu asiyeona umuhimu wa shule kuwa na vyumba vya madarasa vya kutosha na kuhakikisha watoto wote wana madawati ya kukalia ni vema mtu huyu akubali kwamba kwake yeye fedha mfukoni ni bora kuliko elimu.
Laiti mtu huyo angejua kwamba Masheikh wa Saudia ndiyo wenye fedha nyingi kuliko lakini walio kwenda shule ya kutakata ndiyo wanao iongoza dunia tena wanaiongoza kibabe!