Mpango wa kuhujumu M4C na CHADEMA huu hapa - chukueni hatua..

Leo tarehe 29.08.2012 niko hapa maeneo ya Lumumba Kariakoo , kuna rafiki yangu alinialika mlo wa mchana katika moja ya migahawa ya hapa Lumumba na kuwa kwangu hapa niomekutana na tukio ambalo nimeamua niliweke hadharani kabla halijatokea kwani naamini kabisa kuwa lengo la mpango huu ni kuendelea kutugawa taifa kwa misingi ya Ukabila jambo ambalo sikubaliani nalo kama ambavyo ninapinga kugawa watanzania kwa misingi ya udini .

Mwigulu Nchemba , juzi jumatatu amechapisha tisheti zenye maandishi ya M4C – na ameweka maana kwenye hizo tisheti ambazo bado hazijaanza kugawanywa kuwa ni Movement 4 Chagga na ameweka maandishi makubwa kuwa changia Movement 4 Chagga (M4C), Zipo na zitaanza kugawanywa muda wowote .

Zoezi hili linaendena sambamba na operation ya Mwigulu ya kwenda Igunga eti kuelezea nini kilitokea mahakamani kwa wana Igunga , ziara hii imepangwa kuanza siku ya Jumamosi kwani alikuwa anasubiria FUSSO waliyonunua kwa shilingi milioni arobaini na tisa (49,000,000) na kuitengeneza kama za CDM ikamilike na walinunua vifaa Mlimani City tayari tangu wiki iliyopita.

Lengo la kuweka hapa ni kuwajulisha CDM wajue kuwa kuna mipango hiyo tayari imepangwa na inaendelea kutekelezwa , chukueni hatua .Aidha kuna vijana wenu watatu majina leo nayahifadhi wanafanya vikao vingi sana na Mwigulu na wa mwisho alipofika kwake wiki iliyopita alipewa shilingi laki nane , mara ya kwanza alipewa shilingi milioni tatu na huyu ametangaza rasmi kuwa atajiunga na CCM wakati wowote – fuatilieni waliogombea Bavicha na kushindwa na hata mmoja aliweza kushinda ila anawahujumu nyie CDM.

Sikubaliani na mipango ya kuligawa taifa kwa misingi ya Udini na Ukabila hivyo nitaipinga sana hata kama mtanijua LIWALO NA LIWE.

NI MIMI MPIGA FILIMBI-

Tunashukuru, hizo taarifa ni za kweli wala sizitilii shaka, maana CCM wameshachanganyikiwa na wameshajua nchi wameshaipoteza, kwahiyo wanatumia mbinu zozote kujihami!
 
Mwizi wa jina la mtu mwingine ndio anataka kujaribu kuleta hujuma kwenye chama cha ukombozi?!

I have plan B.
Nina mjadala kuhusu mwigulu alivyo iba na kutumia jina la mtu mwingine baada ya kufeli darasa la saba, kabla hajafika Igunga over the week end nitakuwa nimesha attach na kumtumia mpiganaji mmoja azi print na kutoa photocopy azigawe kwa kila mpita njia na nyingine abandike kwenye nguzo za umeme. Hiyo itafanyika usiku huu nitaambatanisha na sehemu ya hii hoja.

Mwigulu ni laini kama maini.
 
mpango uliowazi nii wa kuwatumia ma RPC kila mkoa ili janga kubwa litokee na m4c ipigwe marufuku!msajili wa vyama yumo
 
acha awapeleke nguo za kuva ndugu zake badala yakuchangia mambo ya maana anaendelea na sera za chumvi wakati wa kuomba kura
 
Hii Kama atafanya Hivyo itakuwa ni personal attack kwa Kabila Fulani ndani ya Ardhi ya Tanzania!! Pia ikumbukwe huyu Mwegulu alikuwa na Kimada wake Pale Kariakoo ambapo alimnunulia Vifaa Kutoka China worth 50,000,000/- Labda huyu dada amemliza ndio maana anaendekeza Chuki kwa kabila fulani!! Hivi Magamba Hawawezi kuona Huyu Bwana anatumbukiza Chama na Taifa Kwenye Shimo kwa maslahi Binafsi na Chuki? (Inasadikika Huyo dada alikuwa wa Kabila la Kichaga)
 
Amini nawaambieni watanzania wa sasa sio hao anaofikiria Mwigulu


Hataweza hakika na anajisumbua bure tu.
 
Huyu naibu waziri nae ni CHADEMA?

IMG_0945.JPG
 
Duhh! Mwigulu, mchumi wa daraja la kwanza, anakurupuka na cheap propaganda kiasi hiki? Kweli CCM wameshikwa pabaya, kama mfa maji vile!!
 
Hii dhambi ya ubaguzi sidhani kama itambakiza mtu kwa muda mfupi inaweza ikawa ni njia rahisi ya kupata umaarufu wa kisiasa kwa wenye akili zilizolala lakini huko mbeleni itatugharimu sana na sijui kwann chama tawala wameshindwa kuliona hili badala yake wanalitumia kama mtaji/mbinu ya kisiasa kwani kuwa mchaga/mnyiramba/msukuma et al ni kosa?Mh.Lameck Mkumbo(first class economist) hebu fikiri upya mbinu zako mpya za siasa kwani unakotaka kutupeleka siko mbona kuna vitu vingi sana vya msingi unaweza kuvifanya na ukaonekana ni wa tofauti katika maisha yako ya siasa hebu tujifunze kuishi katika maisha yenye changamoto na hakuna taifa lililoendelea bila kupata changamoto na kuzifanyia kazi hizo changamoto,vyama vya siasa si zaidi ya nchi yetu haya mambo ya ubaguzi ambayo wenzetu wa S.A wameishi wakiyapinga cc ndio tunataka kuyaleta sasa hivi uko wapi umoja unao hubiriwa kwenye majukwaa ya siasa leo hii tunaanza kuangaliana kwa makabila yetu na dini zetu?
 
usifananishe RC na mashekhe ubwabwa wanaojifungia msikitini kukwepa sensa...ficha upumbavu wako.!

Vipi mameno hayo angekuwa amesema Mwislamu? Msiwatendee wenzenu yale msiyoyapenda kutendewa..................hebu pata maumivu anayopata mwachadema mwenzio Muislamu>>>??????
 
Mwizi wa jina la mtu mwingine ndio anataka kujaribu kuleta hujuma kwenye chama cha ukombozi?!

I have plan B.
Nina mjadala kuhusu mwigulu alivyo iba na kutumia jina la mtu mwingine baada ya kufeli darasa la saba, kabla hajafika Igunga over the week end nitakuwa nimesha attach na kumtumia mpiganaji mmoja azi print na kutoa photocopy azigawe kwa kila mpita njia na nyingine abandike kwenye nguzo za umeme. Hiyo itafanyika usiku huu nitaambatanisha na sehemu ya hii hoja.

Mwigulu ni laini kama maini.
HIYO NIMEAFIKI NJIA YA KUMDHOOFISHA ADUI NI KUMPIGA GOOOOOOD lazima kilaza mwigulu akome
 
Vipi mameno hayo angekuwa amesema Mwislamu? Msiwatendee wenzenu yale msiyoyapenda kutendewa..................hebu pata maumivu anayopata mwachadema mwenzio Muislamu>>>??????

wewe mateso gani na nani anapata sijui akili yako ina kutu we vipi HAKUNA MWANACHADEMA ANAEONEWA WEWE
 
WAKUU IVI suala la mwigulu na yule dada kukamatwa na kura za wizi kwenye chupa ya chai hapa town limeishia wapi?
 
ni mbinu nyingine ya kuelekea kufeli kwao.sidhani kama ccm wataweza kubadili hisia za vijana wengi wa sasa kuwa ni chama bomu.
 
Back
Top Bottom