Mpango maalum wa CCM kuhusu madiwani wa CHADEMA

hii thred iko too low sana. na wote wanaochangia wako low pia

mkuu una maanisha nini kusema post iko low,inawezekana kidogo uwezo wako uko low,kwangu mimi naona hii topic inalipa sana kwa sababu ni kweli

Kwa matukio haya CCM uongozi umewashinda ni upole tu wa Watanzania utakao wafikisha 2015.Huwe kufanya kazi ya kupambana na wapinzani badala ya kushughulikia matatizo ya wananchi.

Kwa vile uzi huu umeanzia kwenye assumptions ,na mimi nataka ku assume hivi -

Serikali wakidhani wanawakomoa cdm watawashawishi waende mahakamani na watashinikiza washinde kesi na kubaki na udiwani usio na chama.

Conclusion:
Hoja ya mgombea binafsi bila chama itakuwa imeshinda na huo utakuwa ni ushindi wa wananchi na si ccm,kwani wengi
watakimbia chama chao kwa vile kuna watu maarufu kuliko chama.

Ukinyang'anywa Uraia hakuna mahakama yoyote duniani inayoweza kukusaidia. taratibu na kanuzi za uraia wa nchi ni sheria ambazo hakuna mahakama inaweza kupindisha kinyume. Hivyo kama Chadema wamewanyang'anya madiwani UANACHAMA hakuna mahama ambayo inaweza kurudisha uanachama wao na kama sii wanachama wa chama cha siasa - KIkatiba hairuhusiwi!.

Kwa hiyo utaona kwamba Mahakama haiwezi kuwalazimisha Chadema kurudisha uanachama wa hawa madiwani na itaweza tu kusikiliza kesi zao ikiwa bado wana uanachama hivyo kufuata sheria ya kikatiba. Madiwani sio mber wa Chadema hivyo wanapoteza hadhi zote za chama.

Unajua watu wengine huwa ni wavivu wa kufuatilia mambo na kujifunza. Nakei na Mwita25 jaribuni kidogo kuzishghulisha akili zenu kwa kila mnayoyasema kulihusisha na matukio yanyofanana. Style walioifanya CDM kuwawajibisha hawa madiwani wajimga ni kama ile ambayo magamba walitaka kuitumia kwa Sitta. Walijua ile ndo ingekuwa mwisho wake, na uspika ungekuwa ndio kwaheri.

Sioni ni kwa kiasi gani mmezitumia akili zenu kudhani kuwa cdm wamekosea. Hao jamaa madiwani wapumbavu ndio ntolee. Wao walijua pia ndio maana walisema watakata rufaa ngazi za juu za cdm. Na magamba wakiwachukua hawa madiwani, itakuwa ni kwa wakati huu tu ambapo wanweza wakawa mtaji, 2015 hawana chao ndani ya magamba hawa. Tunajua kilichowakumba kina Kaburu, Lamwai na wengineo ambao kwa sasa ni kama wafu tu kwenye siasa.

Wanajutia, walijuta na watajuta milele.

Nimechungulia tu, napita mazeee! teteteteteteteeeeeeeeeeeee, Nakei na Mwita25 nyie ni vilaza kweli! teteteeeeeeeeee!

Mkuu nilikuwa naheshimu sana comments zako, kumbe sikujua kama kulikuwa na kaupumbavu kanakusumbua. CHADEMA hawakuwafukuza madiwani ili washinde umeya, wala kushinda viti vya udiwani tena. CHADEMA wamewafukuza madiwani kwakukiuka maamuzi halali ya kamati kuu kwa makusudi. Kwa sababu hiyo, ni heri wamewafukuza ili nidhamu ikabaki kwenye chama. Suala kushinda lipo kwa wapiga kura. Kufungua kesi mahakamani ni haki yao kama wanaona wameonewa, la msingi ni kwamba tumewafukuza kwenye chama makini. Hata hivyo itakuwa ngumu kushinda kesi, kwani hawakufukuzwa kwa kuingia muafaka, bali kukiuka kanuni. Hatuna haja ya umeya, tuna haja ya haki na usawa.

Watu kama Mwita wanahitaji elimu ya uraia ili waepuke kuongozwa na hisia. Ulichokisema ni sahihi kabisa kuwa suala si muafaka wala umeya bali suala ni kanuni. Mara nyingi negligence imetuponza Watanzania kwa kuyachukulia mambo kirahisi hata yanayohitaji seriousness.

Mwita na Nakei wanadhibitisha udhaifu mkubwa wa shule za kata. Infact, wanatuonesha failure nyingine kwa mambo ambayo ccm inajivunia!

Mwita na Nakei wanadhibitisha udhaifu mkubwa wa shule za kata. Infact, wanatuonesha failure nyingine kwa mambo ambayo ccm inajivunia!

Subiri kwanza siku 30 zipite za kumtoa mkurugenzi Wa Arusha ndiyo mjadili leo tuna siku saba.

hii thred iko too low sana. na wote wanaochangia wako low pia

Kwa kusema 'too low sana' unamaanisha nini? Kwanza neno 'too' linafanya kazi sawa na hilo uliloongeza 'sana' hivyo hukuwa na haja ya kurudia maneno kama mimi nisivyo na haja ya kukujibu hapa. Imebidi nifanye hivi ili kukuridhisha wewe unaeamini kwamba wenzio wote humu ni wapuuzi na wewe ni mwerevu zaidi. Huna lolote uliloongeza kwenye hii mada.

MADIWANI: Kila jambo lenye heri halikosi na shari kwa namna yake. Yawezekana kabisa kwa kubaki na hao madiwani wangenufaika ila kwa mtazamo wangu ni wazi kwamba walifanya utafiti wakaona kwamba kwa kubaki nao 'shari' ni jingi kuliko heri(Lesser evil school of thought). Hawawezi kuwa wamekurupuka wale waungwana, Mnyika, Kabwe, Lissu na Slaa si watu wa mzaha mzaha kama baadhi wanavyotaka tuamini. Mimi sio mwana CHADEMA wala sina kadi ya chama chochote sema nikiainisha usemaji wao bungeni na maoni yao juu ya mambo kadha wa kadha hapa nchini, naona kama wapo safi(kinadharia ndio, kwani siasa si nadharia tu). Si peke yao ila mtu kama huyu mama 'Shelukindo' na wengineo wa CCM ni watu ambao wakisema kitu ama kigezo unakua na uhakika kwamba wameshafanya tafiti.

CDM wasiwasi wa nini tena! wakati nyie ndio mmewafukuza hao Madiwani wenu.
Mnategemea wakae tu hivi hivi wakati walichagulia na Wananchi wa Arusha, Madiwani mimi nipo pamoja na nyie nendeni mahakamani mkatafute haki yenu ya Kikatiba!
Mimi binafsi najitolea Mawakili wa nne wa kuwatetea Madiwani wapambanaji

CHADEMA wamejenga taswira nzuri kwa kuwafukuza madiwani walio asi lakini kwa upande wa pili wamejipa mtihani mgumu hapo baadae. Inawezekana imekuwa hivi: Mgome alafu watawafukuza, wakishawafukuza nendeni mahakamani, kesi itacheleweshwa na nyie mtaendelea kuwa madiwani halali, wakati kesi inaendelea CCM wataridhia kurudia uchaguzi wa MEYA, wakati wa kupiga kura madiwani waliofukuzwa watawapigia CCM.

Impossible mission

ukiangalia kiundani bila kuangalia UCDM wale madiwani wameonewa...sababu wao hawafanyi kazi lema anazidi kwenda bungeni..sasa baada ya miaka mitano watawaeleza nini wananchi waliowachagua...Sasa hii CDM kwa watu makini wasio tayari kupelekwa ni vigumu sana either ukubali kuwa kibaraka wa ZITTO au MBOWE wazo binafsi hapa halipo...KAribuni sana wanavyuo kwenye chama cha demokrasia..halafu baada ya kuona hakuna jipya mtanisimulia..Tchao

Kwa hiyo kipi bora, kukaa na msaliti ili mradi muonekane wengi au kuachana naye ili muwe waadilifu wachache?

Na hili ndilo linapelekea Watanzania kubaki nyuma kwani hata Rais Kikwete alichaguliwa kule vijijini kwa kutumia picha na tabasamu lake.

CHADEMA wamejenga taswira nzuri kwa kuwafukuza madiwani walio asi lakini kwa upande wa pili wamejipa mtihani mgumu hapo baadae. Inawezekana imekuwa hivi: Mgome alafu watawafukuza, wakishawafukuza nendeni mahakamani, kesi itacheleweshwa na nyie mtaendelea kuwa madiwani halali, wakati kesi inaendelea CCM wataridhia kurudia uchaguzi wa MEYA, wakati wa kupiga kura madiwani waliofukuzwa watawapigia CCM.

Hapa ndio kila siku naingia wasi wasi na uwezo na utendaji wa Chadema. Hivi kwanini kila wakati mnafikiria negative side.

Je Wanachadema mnakubali kwa dhati kabisa kuwa Tanzania ni muumini wa Rules of law. Na kwa taratibu huo hao madiwani wana haki ya msingi kabisa kama hawakuridhishwa na maamuzi ya CC ya Chadema wana haki kamili kufungua shauri lao mahakamani? Sasa nyie wasi wasi wenu nini kama mlifuata taratibu zote za katiba yenu iliyosajiliwa na nchi katika kuwavua uwanachama.

Hakika siku zote muogopa sheria ni mwalifu, Nanyi nachelea kusema ni waarifu sheria kama mnaziogopa sharia hizo.

CHADEMA wamejenga taswira nzuri kwa kuwafukuza madiwani walio asi lakini kwa upande wa pili wamejipa mtihani mgumu hapo baadae. Inawezekana imekuwa hivi: Mgome alafu watawafukuza, wakishawafukuza nendeni mahakamani, kesi itacheleweshwa na nyie mtaendelea kuwa madiwani halali, wakati kesi inaendelea CCM wataridhia kurudia uchaguzi wa MEYA, wakati wa kupiga kura madiwani waliofukuzwa watawapigia CCM.
Mkweli huwa anasimamia haki kwa mstari ulionyooka, si kama CCM wanavuana magamba na yakifika kiuno wanaishia hapo...

Back
Top Bottom