Hekima Ufunuo
JF-Expert Member
- May 28, 2009
- 220
- 11
Uchaguzi wa Mwaka huu hautaleta mabadiliko makubwa kwenye ngazi ya Raisi na hata Wabunge na Madiwani pamoja na kwamba hapa JF panaonyesha kuwa watu wanamwamko mkubwa wa mabadiliko.
Nikiangalia utafiti wa kura ambao unaendeshwe na JF, inaonyesha kuwa mwaka huu utakuwa na mabadiliko makubwa katika ushindi kwa wapiganaji na wapenda mabadiliko (Upinzani). Nikichukua ushindi huu wa hapa JF nikaupeleka kwa wapiga kura, matokeo yanakuja tofauti.
Inaniuma sana kwamba kuna miaka mingine mitano ya kuendelea kushuhudia malumbano yasiyokuwa na tija kwa Taifa huku watu wakijineemesha wenyewe na familia zao. Foleni ikiendele kuwa jambo la kawaida kwa wakazi wa DSM, Mwanza, Arusha. Wizi wa rasilimali za bahari ukiendelea kama kawaida. MIsitu na utalii vikiendelea kudorora kwa kutonufaisha taifa na wenye akili zao kunufaika pasipo na wa kuwadhibiti. Wakinamama wakijifungu kwenye lango la hospitali na wengine kulala chini au mzungu wa nne bila wa kuwaonea huruma wala kuleta majibu. Sukari na unga vikiendelea kupanda bei pasipo na wa kuhangaika navyo kama bidhaa muhimu kwa jamii. Dola ikiendelea kutumika katika taifa lenye uhuru wa miaka hamsini wakati lina sarafu yake ya shilingi. Aridhi ikichukuliwa na wageni pasipo na wa kuhoji. Elimu ikiendelea kudorora kwa kufikisha kidato cha nne watoto ambao hawajui kusoma wala kuandika. (inakuwaje mtoto asiyejua kusoma wala kuandika anafaulu darasa la saba?) Ufisadi ukiendelea kulitesa taifa kama vile halina uongozi. Majambazi yakiendelea kuuwa watu pasipo na wa kuwatisha ama kusimamia sheria (Jhwani Mwaikusa ni mfano tu wa Watanzania wengi wanaokufa kwa ujambazi) Pensheni kwa wazee ikiendelea kuwa ndoto kwao baada ya kutaabika kwa mika mingi ya utumishi. (kima cha chini cha pensheni kwa mstaafu ni 52,000?=, Kinatosha nini kwa nchi ambayo sukari kilo ni shilingi 2,000?=?) na mengine mengi.
Haya yote yatafikia tamati siku "WANAOTAABIKA WATAKAPOLIONA TATIZO"
Mpaka sasa wanaoliona tatizo siyo wanaotaabika, wanaoweza kuingia JF Wanaliona Tatizo lakini hawataabiki. Kilo ya sukari kuuzwa sh. 2,000/= kwake ni tatizo lakini lenye majibu. Mke au mume wake hawezi kulala sakafuni muhimbili wakati wa kujifungua au anapoumwa kwa sababu anaweza kulipia fast truck na akapewa kitanda. Nauli za Daladala kupanda ni tatizo lakini kwa mwana JF anao uwezo wa kukabiliana na hilo tatizo. Wale ambao haya ni matatizo kwao kwa kutokuwa na uwezo wa kukabiliana nayo HAWAJAYAONA hivyo wanataabika tu bila msaada.
Kura ya JF siyo hali halisi kule kwa wapiga kura ambao hawalioni tatizo.
Kuwafanya walione tatizo, tufanyeje????????
Respect