Mpaka wa Horohoro, nini kinaendelea?

matongo manawa

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
336
79
Kuna kila dalili za kuibuka mgogoro wa kidiplomasia Kati yaTz na Kenya kwenye mpaka
wa Horohoro ambapo kuna mradi wa ujenzi wa mradi wa one stop border.

Kila Nchi inajenga mradi huu kwa upande wake lakini cha ajabu wakenya wamechimba fence na kuingia hadi kwenye ardhi ya Tanzania.

Nimepita eneo hilo nikaona wajenzi wanafanya kazi huku nafasi ya Normanland ikiwa nayo inajengwa ukuta kuingia Tz, nilijaribu kuwadodosa wenzangu tuliokuwa tunavuka nao mpaka nao wakasema wanashangaa!!

Sijui serikali yetu inajua???
 
Ndio maana naomba kipindi cha dhaifu kiishe haraka,kuna hatari ya kuvuna aibu kama taifa.
 
Kenya wasihofu kwa vile kwa sasa Tanzania haina serikali yenye kuweza kushughulikia masuala madogo kama hayo. Rais kila siku anazurura sijui kujitibia au kushangaa nani ajua?

Serikali yetu ya sasa ni kwapuakwapua hivyo kugombea kitu ambacho hakiiingizi ten percent siyo kipaumbele chake. Hivyo watanzania mlie na nchi yenu itaendelea kumegwa na kuingiliwa na wakimbizi wa kiuchumi huku nanyi mkiwavumilia. Ajabu mkienda South Africa au Greece mnatolewa kamasi na kutimliwa kama mbwa koko.

Kazi kwenu.
 
Tuna inteligensia na geshi imara sana duniani?Bado tuu hawajaamua(amka), shimbo yupo wapi?
 
Mkuu Wakenya hawawezi kufanya makosa kama hayo, nafikili watakuwa wanajenga nje ya mpaka sio ndani mkuu, sio wajinga wanajuwa fika TANZANIA haiwezi kupuuzia kitu kama hicho. Hapa tutazungumza mengi kuhusu Serikali yetu lakini tukumbuke Jeshi letu na Watanzania kwa jumla sio lelemama.
 
Acha kuota mkuu, unavyoongea kuhusu jeshi lenu utadhani la marekani.
 
Ndio maana naomba kipindi cha dhaifu kiishe haraka,kuna hatari ya kuvuna aibu kama taifa.
kwa kiasi fulani nakuunga mkono.
kuna mambo ya ajabu yanatokea mipakani ambayo hawa jirani zetu walikuwa hawathubutu kuyafanya enzi zile ambazo mgambo (militia) ya Tanzania ilikuwa kubwa kuliko majeshi yao ya miguu kwa ujumla (namaanisha nchi zote nane).
 
Always look on the bright side of life! One stop border itarahisisha sana biashara kati ya nchi za Afrika Mashariki. Long live EA.
 
Kenya wasihofu kwa vile kwa sasa Tanzania haina serikali yenye kuweza kushughulikia masuala madogo kama hayo. Rais kila siku anazurura sijui kujitibia au kushangaa nani ajua?

Serikali yetu ya sasa ni kwapuakwapua hivyo kugombea kitu ambacho hakiiingizi ten percent siyo kipaumbele chake. Hivyo watanzania mlie na nchi yenu itaendelea kumegwa na kuingiliwa na wakimbizi wa kiuchumi huku nanyi mkiwavumilia. Ajabu mkienda South Africa au Greece mnatolewa kamasi na kutimliwa kama mbwa koko.

Kazi kwenu.

South Africa au Greece? Mbona mbali sana huko? Nenda hapohapo Kenya tu na vi-degree uone kama vitakusaidia.
 
Back
Top Bottom