Mpaka sasa bado wananchi tunalipia gharama za uchaguzi za ccm 2010 kwenye sukari

Sangarara

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
13,100
5,649
Kwamba Upandaji wa sukari ghafla baada tu ya uchaguzi mkuu 2010 ambao umeng'ang'ania kuwa juu mpaka sasa unasababishwa na fidia za michango ya wafanyabiasha kwa chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ni taarifa ambazo zimekuwa zinikinyima usingizi kwa muda sasa.

Vyanzo vyangu vya habari kuanzia TRA Customs Department mpaka Wizara ya Viwanda na Biashara, kwa muda sasa, na kwa uhakika vimekuwa vikirudia maelezo yale yale kwamba wafanyabiashara wa kihindi ambao wanapewa vibari vya kuingiza sukari kutoka nje ya nchi ni wale waliokifadhili chama cha Mapinduzi kwenye uchaguzi huo.

Kwamba vibari hivi hutolewa kwa makubaliano ya kutotozwa import duty, lakini wafanyabiashara hawa huuza sukari kwa bei ambazo zime factor in importy duties ili kufidia michango yao.

Kwa nini nchi nzima tuchangie matumizi haya? au ina maana mpaka sasa hawajamaliza deni lao? au ndio tunalipia na riba?
 
Kama utakumbuka mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari, alisema wakati wa kampeni kuwa akichaguliwa kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki atashusha bei ya sukari...vipi bei imeshuka.
 
Kama utakumbuka mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari, alisema wakati wa kampeni kuwa akichaguliwa kuwa mbunge wa Arumeru Mashariki atashusha bei ya sukari...vipi bei imeshuka.
Sikumbuki kama alisema kitu kama hicho, lakini wewe na mimi tunajua kwamba haiwezi kushuka, na mbaya zaidi haishuki kwa sababu tunalipia madeni, na madeni yenyewe ya kimadili dili.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom