Mpaka Julai kila msanii awe na TIN Namba - Zitto Kabwe

sexologist

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
2,283
976
Ninafatilia kipindi cha bunge... kati ya hoja zilizonivutia ni hoja ya Zito Kabwe kwamba kila msanii awe na TIN namba ili kuweza kulinda kazi zake kwa maslahi yake na taifa kwa ujumla.
 
Yap ni ahadi ambayo hata Mh.Nchimbi aliitoa jana kwa wasanii wote kuwa July mwaka huu ni mwisho wa wasanii kuibiwa kazi zao yaonekana wamejipanga vyema kuandaa mchakato wa kuwasaidia wasanii
 
Martha Mrata anasema ukiangalia idadi ya watu waliokuwepo msibani Kanumba hakutakiwa kuishi katika mazingira kama yale... Hili linasababishwa na kuwa na kipato kidogo japo umaarufu unakuwa ni mkubwa zaidi... Na sababau kuu ya yote haya ni kazi zake yeye kama msanii na wengine kuwa zinaibiwa... Kama isingekuwa hivyo Kanumba angekuwa ana maisha ya juu zaidi ya yale yaliyoonekana... pia angekuwa na Bodgadi...

My take: Tushiriki kulinda kazi za wasanii wetu na tusishiriki kuhujuma kwa kubani... tununue orijino jamani.
 
hujui unakosea unaposema TIN NAMBA?

Ninajua nakosea mkuu... kama unafahamu lugha vizuri hiyo ni totoloji (mrudio) TAX IDENTIFICATION NUMBER... Lakini nimeandika kile nilichosikia mkuu... By the way lets focus on the meseji.
 
Hawa jamaa hawalipi kodi kabisaaaaaaa. Naskia mwaka 2011 pekee Kanumba aliipata zaidi ya milioni 500TZS, ambazo zinazidiwa na alizopata Ray kutokana na kazi yao ya filamu. Hapo ujue kachukua only 10% tu inayobaki wanaiba wahindi na waonesha sinema bubu. Hii serikali goigoi kama kama ingekuwa inataka mapato hapo ndio mahala pake. Kiutaratibu mtu yeyote anatakiwa kulipa kodi hadi 30% ya mapato yake kwa mwaka, sasa unajiuliza kumbe hawa jamaa hata TIN hawana na TRA wapo tu wanawatazama. Bila kuiondoa hii serikali goigoi kamwe hatutaendelea, wao wanadhani mapato ni misaada ya wazungu akina David Cameron kumbe kuna vyanzo kibao hapa vinavyohitaji usimamizi tu.
 
Wewe ni mnafiki huna chochote.., vipi demu wako wa german hajambo..usije ukaniroga mana ulisema hata panya hatobaki.. Kabwela mzitto
 
Ninajua nakosea mkuu... kama unafahamu lugha vizuri hiyo ni totoloji (mrudio) TAX IDENTIFICATION NUMBER... Lakini nimeandika kile nilichosikia mkuu... By the way lets focus on the meseji.

vp wanaosema ATM-machine?
barabara ya morogoro road?
benk ya crdb?
 
Ninafatilia kipindi cha bunge... kati ya hoja zilizonivutia ni hoja ya Zito Kabwe kwamba kila msanii awe na TIN namba ili kuweza kulinda kazi zake kwa maslahi yake na taifa kwa ujumla.

Akasome upya. kama mashine za EFD hazitumiwi na wafanyabiashara wa maduka ya jumla Kkoo waqt wanazo na wanamauzo ya over five hundred milion per day. Zito Zuberi anaongea nini
 
Anayesema CRDB Bank yuko sahihi maana CRDB ni jina tu sio kifupisho cha maneno kadhaa. Kule kwenye cooperative and rural development bank tulishatoka kitambo
 
vp wanaosema ATM-machine?
barabara ya morogoro road?
benk ya crdb?

hapo kwenye bank ya CRDB hakuna kosa, kwani CRDB haina kirefu tena! I mean hakuna maneno halisi ndani ya hizo herufi "CRDB" hiyo B haimaanishi Bank, bali inasomeka hivyohivyo tu!

Source: mimi nimeshiriki kutoa semina zao
 
Lakini ni kweli kila msanii tayari ana TIN yake?!
Maana hii habari ni ya mwaka jana!
 
Slaa katoa amri swala hili lisijadiliwe, lakini Godbless Lema na viongozi wengine wamepuuzia amri hiyo ya Slaa...
 
Slaa katoa amri swala hili lisijadiliwe, lakini Godbless Lema na viongozi wengine wamepuuzia amri hiyo ya Slaa...

Dk. Imani vipi? Mbna kama CHADEMA inakutoa sana povu..!!
Rudi Czech au subiri viti maalum hapo Moro Kusini.
 
Back
Top Bottom