Moyo wangu haupendi tena mwanaume nifanyeje?

Heloo

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
4,391
3,402
Wadau naomba mnishauri,nifanye nini?baada ya kuwa kwenye uhusiano na mpenzi
kwa miaka mitano na baadae kuamua kumwacha kwa jili ya ulevi wake wa kupitiliza
nahisi au najikuta simwamini na wala simpendi mtu yoyote tena,ikumbukwe kuwa
nina umri wa miaka 30,na pia sio kwamba siku zote sikujua kama choice yangu ni
mbaya bali niliamini angebadirika na kuwa mpenzi bora,lakini kadri siku zilivyokuwa
zinakwenda ndivyo na ulevi alivyokuwa anazidisha kurudi kwake peku,kuumia kwa ulevi.
Mbali na ulevi,hakuwa mtu wa mapenzi nikimaanisha kunijali,mfano,yeye alikuwa anafanyia
kazi mkoa mwingine mimi mwingine,mwaka unaweza katika asije kwangu kunitembelea
na akija ujue kaja Dar kwa shida za kiofisi,pia vitu kama zawadi ni ndoto toka kwake kinyume
na mimi,sasa kwa kawaida unaweza ukasema jamaa hakuwaanakupenda lakini si kweli
mbali na mapungufu hayo nilijihakikishia ananipenda kwa mambo fulani niliyokuwa napele
leza kama je ana mpenzi mwingine,au ananiongeleaje kwa watu?au je mahusiano yake
kwa mpenzi wa zamani yalikuwaje,nikagundua kwamba jamaa Tatizo ni Ulevi tu wa kutia umaikini
Sasa ni mwaka niliamua kumwacha,na kweli nikafanikiwa kumtoa moyoni,tatizo akitokea mpenzi
mwingine moyo haukubali,nitafanyaje?au nijilazimishe?au nina tatizo la saikologia?lpz help
 
.
Heloo.. niPM
 
usijilazimishe anza urafiki wa kawaida na mtu mwingine ambaye ni mwanaume na utamsahau yule na utampata mwingine wa kumpenda toka moyoni lakini usijilazimishe kabisa.
 
Inshort wewe bado hujapata kabisa mpenzi wa kuitwa MPENZI chini ya hili jua.
Habari yako nzima sijaona vigezo vya wewe kujinakshi kua una mpenzi.
Huyo uliyekua nae ni boshen flan hivi , watoto wa mjini wanaita zugeshen.
Hata visifa vya kusema nimwite mkata kiu pia hanavyo!
Now start afresh, sasa ndiyo tafuta mwanaume, kupotea njia siyo ujinga bali ndiyo kuijua njia.
Tafuta kitu mang'anyu ule nchi.
This country bwanaa!
 
Asikudanganye Mtu .. Hakunaga mwanaume bora.. Utayempata lazima awe Na kasoro, cha kufanya wewe jipange kukabili kasoro hiyo.. Mara nyingi matatizo makubwa ya wanaume ni mawili, AMA mlevi au mpenda wanawake.. Unaweza kupata mjitu hauonji pombe hata kidogo ila masaa kumi Yuko bize Na cm anatengeneza desh..desh.. Hata ukumfumania ni mwepesiiii wa kuomba excuse ila baadae Kama kawa anaendelea.. But akiwa chapombe unaweza kumdhibiti baadae akawa mwanaume bora sana..
 
Wadau naomba mnishauri,nifanye nini?baada ya kuwa kwenye uhusiano na mpenzi
kwa miaka mitano na baadae kuamua kumwacha kwa jili ya ulevi wake wa kupitiliza
nahisi au najikuta simwamini na wala simpendi mtu yoyote tena,ikumbukwe kuwa
nina umri wa miaka 30,na pia sio kwamba siku zote sikujua kama choice yangu ni
mbaya bali niliamini angebadirika na kuwa mpenzi bora,lakini kadri siku zilivyokuwa
zinakwenda ndivyo na ulevi alivyokuwa anazidisha kurudi kwake peku,kuumia kwa ulevi.
Mbali na ulevi,hakuwa mtu wa mapenzi nikimaanisha kunijali,mfano,yeye alikuwa anafanyia
kazi mkoa mwingine mimi mwingine,mwaka unaweza katika asije kwangu kunitembelea
na akija ujue kaja Dar kwa shida za kiofisi,pia vitu kama zawadi ni ndoto toka kwake kinyume
na mimi,sasa kwa kawaida unaweza ukasema jamaa hakuwaanakupenda lakini si kweli
mbali na mapungufu hayo nilijihakikishia ananipenda kwa mambo fulani niliyokuwa napele
leza kama je ana mpenzi mwingine,au ananiongeleaje kwa watu?au je mahusiano yake
kwa mpenzi wa zamani yalikuwaje,nikagundua kwamba jamaa Tatizo ni Ulevi tu wa kutia umaikini
Sasa ni mwaka niliamua kumwacha,na kweli nikafanikiwa kumtoa moyoni,tatizo akitokea mpenzi
mwingine moyo haukubali,nitafanyaje?au nijilazimishe?au nina tatizo la saikologia?lpz help
Kama anakunywa pombe, hata kama si mlevi, hilo linaweza kukusababishia hali hiyo kwasababu pombe inatrigger those unwanted memories.

Kwa mfano kama ulikuwa raped, halafu mtu huyo aliyekurape alikuwa anavuta cigar, basi ukija kukutana na mwanamume anayevuta cigar, unaweza usimfeel kutokana na hizo memories.
 
Habari yako dada, Aya! taratibu taratibu . . . . Kiukweli nimefurahi kuamuakutoa yalio moyo mwako hasa kwa watu makini kama wanaJF hii ni hatua kubwa ya kupata suluhu la tatizo lako. Unachotakiwa kujua ni kwamba haupo peke yako wenye tatizo hili, wanaJF tupoupande wako wakati wote. Nikiaanza na majibu ya tatizo lako hebu tuanze nakuangalia tatizo lilipoanzia, mwanaume uliyempata alikua na tabia gani zilizo kuudhi, hamna ubishi kuwa haukuonja ladha halisi ya kiini cha mapenzi 'li-note' hilo. Hapo ndipo palipo kushinda hivyo tatizo ni tabia, miaka mi5 inatosha kujenga mawazo tofauti/hasi juu ya wanaume hili ni moja. Tuvute pumzi kidogo . . . . . . naam kitaalamu umeathiriwa kisaikolojia ila amini tatizo litakwisha. Kwanza jaribu kuorothesha sifa mbaya zilizokukera za mpenzi wako wa zamani kwenye karatasi moja kadiri uwezavyo, kichwa cha habari andika MTAZAMO WANGU JUU YA WANAUME. Kisha chukua karasi jingine andika tabia/jinsi unavyo taka mpenzi wako awe, kichwa cha habari andika MTAZAMO SAHIHI. Choma moto karatasi ya kwanza, pili isome karatasi ya pili ihifadhi. Isome mara kwa mara . . . . anza maisha mapya waki mtazamo juu ya wanaume. Jiweke jinsi mwanaume wa sampuli unayotaka uwenaye wanavyo taka. Sali na kuomba mungu akujalie upate bwana anayekujali, kukuheshimu na kukupenda kwa dhati . . . natumaini ikifuata haya utapata suluhisho la tatizo lako kwa uwezo wa MUNGU. NOTE: MEN ARE NOTE SAME. kama utahitaji maelezo zaid ni PM ukaniuliza maswali kwa ufafanuzi zaidi. Asante!
 
Pole sana, hakuna mwanadamu aliyekamilika, jifunze kuishi na mapungufu ya wengine. Acha kuumiza kichwa na mambo ya mapenzi, kinachotakiwa kufanya ni kutafuta pesa tu na siyo mapenzi, kwani ukipata mapenzi unayotaka halafu huna pesa si ndio balaa. Ukiwa na pesa mapenzi yatakuja yenyewe, yasipokuja SODA ZA KOPO zipo, unanunua unakunywa, ukimaliza unatupa. Raha sana.
 
Soda ya kopo tena? Duh......mshikaji!!!! (am wondering.... till when??)
 
MAPENZI NA PESA WAPI NA WAPI! , ingawa mitizamo inatofautiana ila mtizamo wa falsafa hizi za kuunganisha mapenzi pesa ni kwa walio vunja mioyo yao kukosa confidenc 2, na kumanage wawa pendao na kuamua kuvunja kikombe cha asali nakutaka kuunganisha kwa nguvu ya gundi ya karatasi.
 
Ok, chukulia wewe ni demu, halafu ombaomba anakutongoza na anamapenzi ya dhaaati kwako, UTAKUBALI???
 
Soda ya kopo tena? Duh......mshikaji!!!! (am wondering.... till when??)

Till u broke. Soda ya kopo safi sana, haina stress, inakupa muda mwingi kutafuta pesa na siku zote haina siri moyoni. Yani raha sana.
 
Ukiona hiyo hali ujue bado unampenda sana, hiyo kusema umemtoa moyoni unajipa tu moyo kwamba ume move on
kwa kifupi bado hujafanikiwa kumsahau
 
Pole sana, hakuna mwanadamu aliyekamilika, jifunze kuishi na mapungufu ya wengine. Acha kuumiza kichwa na mambo ya mapenzi, kinachotakiwa kufanya ni kutafuta pesa tu na siyo mapenzi, kwani ukipata mapenzi unayotaka halafu huna pesa si ndio balaa. Ukiwa na pesa mapenzi yatakuja yenyewe, yasipokuja SODA ZA KOPO zipo, unanunua unakunywa, ukimaliza unatupa. Raha sana.

ushauri gani huu?
 
Back
Top Bottom