Moyo unaniuma sijui nifanyeje?

apprentice1997

Senior Member
Jun 8, 2016
107
99
Wakubwa zangu shikamoni,

Niliamua kutulia na msichana mmoja tu nikaamua nitulie nae huyo, kiukweli nampenda sana mpaka nimeamua kuwa mwaminifu kwake. Jana alinielekeza kuwa nimekuwa muwazi sana kwake na yeye ameamua kuniambia ukweli kuwa amekuwa na mahusiano na vijana wengine 3 jumla tupo wa 4. Lakini yeye bado ni bikra na hajawahi kulala na mtu yeyote.

Yeye ni mtu wa dini sana na amekuwa akihudhuria semina wiki hili na akaamua kunieleza ukweli wote na pia anasema anataka kuachana na sisi wote na atulie. Mimi nimetafakari sana Jana hiyo nikaenda kanisani muhubiri akasema ili ufanikiwe ni lazima ujitoe mahali unapodhani ni comfort zone yako nikaguswa nikajua kuwa natakiwa kuachana na mapenzi nae na nisiwe na mwanamke yoyote. Umri wangu ni miaka 19, nimefaulu na mwezi huu naanza kwenda college na yeye bado yupo shule.

Baada ya kutoka church akili yangu ilitulia na kuniambia kuwa ninataka kuwa na amani nae ninatakiwa niachane nae na nikaridhia baada ya mimi na yeye kuonana nikakumbuka mambo mengi sana tuliyopanga pamoja na ninampenda kwa kuwa anajiheshimu na ana hofu ya Mungu. Moyo unaniuma toka hapo ninafikiria mipango yangu na malengo niliyokuwa nae ninaumia sana natamani hata nisingejiingiza kwenye mapenzi.

Ninatamani nifuate sauti ya Mungu ila ninatambua maamuzi ya Mungu ni magumu na ndio haya yanayonikumba sasa. Leo ninataka nionane nae sitapenda aondoke tukiwa hatujaelewana hili jambo litatuathiri sana na hatutaweza kuendelea na masomo na kiukweli tunapendana sana.

Nikifikiria sina cha kumwambia ninatamani niseme neno moja tu na roho yangu ipone haya maumivu ninatamani kumlaumu ninaishia kumsamehe kwa kuwa nampenda sana na pia ninatamani kuachana nae ila hofu yangu ni kuwa nitaumia sana siku za mbeleni.

Na sina mpango wa kuwa mzinzi ninatamani Mungu anibariki anipe mwanamke ambaye atakuwa wangu mimi peke yangu na asinisumbue. Inafika muda najilaumu sana kwanini nilianza mapenzi maana naumia sana. Wapendwa naombeni ushauri wenu nimwambie nini ili tuweze kuelewana na moyo wangu utulie. Na pia nifanye maamuzi yapi kuhusu sauti inayonena ndani yangu.
 
Huko kapanga kwako ndio nyumbani moyo una vyumba vingi mchagulie kimoja umuweke usimpe wote, kikawaida hapo kunakuwa hakuna makombo.
 
karibu dunia nyingine mdogo wangu bora ata wewe umeanza 19s mapenzi mimi nilianza na miaka 26 siku nilipotendwa aisehhh sijui but sasa ndo hivyo tena sijapata wa kumpenda nikishakula tu basi beib beib huisha hapo hapana kuweka urafiki na mwanamke
 
Mkuu unatambia kwa sheria za serikali na dini miaka 19 sio mtoto. Umenikumbusha wakati nina umri unaolingana na huu nilikuwa nikiwafuata walionizidi umri na kuwaeleza matatizo yanayohitaji ushauri walinipuuza ila iliniumiza sana wakati huo mpaka nilipokuwa na umri mkubwa zaidi nikatambua kwamba ni changamoto za maisha tuu. Ukifungwa mlango mmoja Mungu atakufungulia mlango mwingine, tena pengine bora zaidi.
 
Duuuhh kazi kweli kweli.

Hakuna ulevi mbaya duniani kama kulewa dini. Wewe na huyo mpenzi wako mmelewa DINI. Mtu akilewa dini ule uwezo wake wa kufikiri hukasimisha kwa wengine na yeye kubaki na kichwa kitupu.
 
YANI SIJUI NIKUAMBIE NINI...ANY WAY NAONA NI STAGE TU YA KUPITIA AU EXPERIENCE...IPO SIKU UTAJICHEKA.....NAONABADO HUJAKUMBANA NA MAMBO BADO.....USISHANGAE UKAMKUTA ANA WATU WASHAMLALA LAKINI BAADAE USIAMINI TOO MUCH....ANYTHING CAN HAPPEN
 
Pole sana kwa maumivu. Ni bora tu usikutane naye, maumivu yatapungua taratibu ila elekeza muda wako wote kwenye masomo yako ili uweze kufanya vizuri. Kila la heri na baraka kwenye masomo yako.
 
Alishatafunwa huyo. Halafu miaka hiyo unasema umempenda sana!?? Oh my God!! You are at the foolish age. You can not even ponder how sweet and how bitter your love is. You are five little boys still getting hope you love her much and noone has played the vg!!? How dare on this belief my boy? Oh shantabalalalak shantabalalalak. Sorry umenichanganya nanena kwa lugha ya kiyunani. Run away boy from that Apple
 
Dogo acha utani bint ni bikra afu were uliishajiingiza mapenzini? na nani? mbona umeanza mapenzi ukiwa ndogo? utasababisha ka dushe kako kawe kibsmia tulia usome ukimaliza chuo fanya mapenzi uwezavyo kwa sasa utaendelea kuumia na vile pesa hauna utaendelea kudanganya eti bado nina bikra
 
Mpo wanne halafu bado unasema mnapendana dogo acha hizo.

Jifunze kumuacha aende maana baada ya kuwa mtakuwa 10
 
Acha ubaguzi na itakadi za kizamani... Hii ndo dunia ya utandawazi, jichanganye ili ujue vizazi vyako vijavyo vinaendaje,,,

Kama unaona wazo lako ni jema kajichanganye interior uko uone watu wanavyoteketea kwa kukosa maarif ya kisasa.
Umenena vema mkuu.
 
Wakubwa zangu shikamoni,

Niliamua kutulia na msichana mmoja tu nikaamua nitulie nae huyo, kiukweli nampenda sana mpaka nimeamua kuwa mwaminifu kwake. Jana alinielekeza kuwa nimekuwa muwazi sana kwake na yeye ameamua kuniambia ukweli kuwa amekuwa na mahusiano na vijana wengine 3 jumla tupo wa 4. Lakini yeye bado ni bikra na hajawahi kulala na mtu yeyote.

Yeye ni mtu wa dini sana na amekuwa akihudhuria semina wiki hili na akaamua kunieleza ukweli wote na pia anasema anataka kuachana na sisi wote na atulie. Mimi nimetafakari sana Jana hiyo nikaenda kanisani muhubiri akasema ili ufanikiwe ni lazima ujitoe mahali unapodhani ni comfort zone yako nikaguswa nikajua kuwa natakiwa kuachana na mapenzi nae na nisiwe na mwanamke yoyote. Umri wangu ni miaka 19, nimefaulu na mwezi huu naanza kwenda college na yeye bado yupo shule.

Baada ya kutoka church akili yangu ilitulia na kuniambia kuwa ninataka kuwa na amani nae ninatakiwa niachane nae na nikaridhia baada ya mimi na yeye kuonana nikakumbuka mambo mengi sana tuliyopanga pamoja na ninampenda kwa kuwa anajiheshimu na ana hofu ya Mungu. Moyo unaniuma toka hapo ninafikiria mipango yangu na malengo niliyokuwa nae ninaumia sana natamani hata nisingejiingiza kwenye mapenzi.

Ninatamani nifuate sauti ya Mungu ila ninatambua maamuzi ya Mungu ni magumu na ndio haya yanayonikumba sasa. Leo ninataka nionane nae sitapenda aondoke tukiwa hatujaelewana hili jambo litatuathiri sana na hatutaweza kuendelea na masomo na kiukweli tunapendana sana.

Nikifikiria sina cha kumwambia ninatamani niseme neno moja tu na roho yangu ipone haya maumivu ninatamani kumlaumu ninaishia kumsamehe kwa kuwa nampenda sana na pia ninatamani kuachana nae ila hofu yangu ni kuwa nitaumia sana siku za mbeleni.

Na sina mpango wa kuwa mzinzi ninatamani Mungu anibariki anipe mwanamke ambaye atakuwa wangu mimi peke yangu na asinisumbue. Inafika muda najilaumu sana kwanini nilianza mapenzi maana naumia sana. Wapendwa naombeni ushauri wenu nimwambie nini ili tuweze kuelewana na moyo wangu utulie. Na pia nifanye maamuzi yapi kuhusu sauti inayonena ndani yangu.
mkuu umenishtua sana,nikajua una maradhi ya moyo kumbe mapenzi,khaaa!
ngachoka!
pole kwa mkasa!
 
Back
Top Bottom