Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
Moyo ulojeruhiwa, kuponywa kwake ni kazi,
Hasa ulodhulumiwa, kutwa hujaa majonzi,
Ule ulosalitiwa, hutiririka machozi,
Moyo ukijeruhiwa, huponywa kwa dawa gani?
Moyo ulojeruhiwa, daima huwa na kovu,
Kila ukishituliwa, huwa kama nyumba mbovu,
Nyumba inapovujiwa, ndivyo uzidi ubovu,

Moyo ulojeruhiwa, hauishi maumivu,
Huhisi kukataliwa, hukwepa tonesha kovu,
Hofu ya kukatiliwa, huwa kama gari bovu,

Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)