Movenpick sasa inaitwa Serena hotel huu ni ukwepaji kodi?

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,947
4,444
IMG_3121.JPG

Wadau hii hotel zamani ilikuwa inaitwa Sheraton wakaja wawekezaji wakachuma faida bila kulipa kodi wakabadili jina ikawa Movenpick Royal Palm wawekezaji wamechuuma weee sasa karibia miaka mitano imeisha ambapo serikali inasamehe kodi kwa mwekezaji wamekuja na jina tena jingine inaitwa Serena hivi huu mchezo wa kusamehe kodi wawekezaji wakubwa kama hawa itaisha lini au na maboss wanafaidi? Mi nimefungua kagrosali kangu TRA kila siku wanaandamana na mimi kwa siku hata kreti haliishi jamani watanzania imefika sasa kipindi tuseme enough kwa pamoja tumegeuzwa mazuzu wanawaacha makupe hawa wanao nyoja wanakuja mitaani kutukimbiza akina baba lishe inasikitisha sana.
 
wameshagawana wao kwa wao,
ngoja tusikie wadau wanasema nini.

Msamaha wa kodi miaka 5 mwekezaji anapewa wanacho fanya wao ni kucheza na majina tu msamaha unapo karibia utasikia tumeendesha kwa hasara sana
 
sasa mnapowachagua wabunge waimba kwaya na taarabu mnategemea wataweza kutunga sheria makini kweli?
 
mkuu, 2 options.
ingia msituni sasa au subiri zamu yako ikija hapo baadae
 
Movenpick was recently acquired by Serena chain of hotels of east and central africa. Serena group is owned by kenya based Tourism promotion services (tps serena) which is listed in Nairobi stock exchange. TPS is part of 96 Agha khan fund for economic developments world wide. In brief the change of name is because the hotel is now owned by kenya tps which trade under the name of serena. Serena has several hotels in kampala, mozambique, nairobi, mombasa, kigali and arusha.
 
Sawa sasa hapo unategemea Serena wataanza kulipa kodi? Moja kwa moja wataomba msamaha na watapewa wawekezaji wapya.
 
kuna tatizo kwenye sheria zetu

Jamaa wameandikisha TIC kama new project, kwani wamenunua tena nasikia kwa cash, so ahuweni ya kodi na marupurupu yake kama kuingiza gari kadhaa bila kulipa kodi, kuleta wakenya kama wataalam nk

Wanaojiita wawekezaji wanaifaidi saana hii taifa na ni sisi sisi tunawasaidia kwa ujira kidogo
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom