Movement for Change yaingia Simanjiro....!! Ole Sendeka ahahaaa...!!

The Fixer

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
1,365
583
Kumekucha, Kamanda James Ole Millya baada ya kuufuata upepo wa Mabadiliko unauvuma vizuri tu ndani ya Tanzania na kuanza kusomba ngome ya CCM- Staminaz ndani ya Arusha,Ataingia ndani ya ngome ya Ole Sendeka,hapa Simanjiro. Vijana wapatao 3,000 ndio watakao msindikiza Kamanda wao huku Simanjiro na kuanza kazi ya kufungua matawi ya Chadema ndani ngome ya Ole Sendeka ( CCM )na kilicho kibaya zaidi ni namna Ole Sendeka anavyo hahaaa kuuzia Maandamano hayo kwa kuwatumia Polisi ! Polisi nao wamekataa kumzuia Ole Millya kwa kudai kuwa ni mzawa wa Simanjiro na ana haki kufanya lolote la kisiasa ndani ya Simanjiro ! Upepo wa Movement for Change unamtisha sana Ole Sendeka.....!
 
yaaaap! hapo hapo! na watajuta safari hii! watatumia polic n.k lakini hawataweza!!! peopleeeeeeeeees poweeeeeeeeer!
 
Hivi huyu millya si alikuwa na biofu na sendeka mpaka wakifikishana kotini? Ndo yeye? Kesi iliishaje? Nadhani sendeka aliwahi kumtishi dogo kwa bastola kama ninayo kumbukumbu.
 
Ole Sendeka, Anafahamu nguvu ya Ole Millya akiwa na vijana wake si mnakumbuka ile vita ya mwaka 2009 So Baada ya kuona jamaa anarudi na Movement for Change amepagawa ile mbayaa, Polisi baada na wao kukataa kumzui jamaa wakidai ana haki zoote kama Mtanzania ndio kabisaa amebaki kuchanganyikiwa ! Mkisikia Ole Sendeka, sukari imepanda msishangae maana kibaya zaidi atasindikizwa na Kamanda Lemma !
 
Nguvu ya Umaa aaaaaaaaa daima,watatupiga risasi na kuzimaliza lakini hatatumaliza wote Peoples Power.Karibu sana kamanda Millya kamkoboe Sendeka hana lolote
 
Millya kaona mbali, bila kutoka CCM ubunge atauota tu, na u-DC hawezi kupewa kwani hapatani na baba riziwani. so simanjiro kumekucha. kwani sendeka alipita bila kupingwa sasa kumekucha.
 
Jamani huyu ..Katibu Mwenezi wilaya Longido CCM ni nani?Nimesikia nusu nusu eti kahamia Chadema....
 
Mkuu mvt4c inaongozwa na mungu na si binadamu hata jk analijua hili hio usishangae sana tukitoka tunarudi bagamoyo ,chalinze kueleza wale watu kwanini wanaongozwa na rais kutoka huko miaka 10 wanaishia kuishi kwenye nyumba za udongo kama si laana ninini??
 
kuna dalili ya majimbo yote ya arusha kuchukuliwa na CDM
 
Hapa kuna majimbo matatu manne ya kuyapigania nayo ni
1. Longido
2. Simanjiro
3. Kiteto
4. Monduli

Haya ndo majimbo magumu yaliyo bakia ila kwa kumtumia huyu millya nina uhakika yatakubali mziki wa CHADEMA
 

Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom