MOU si Mkataba

Wikipedia ina define MoU hivi

A memorandum of understanding (MOU) is a
Ukienda mahakamani na madesa kutoka WIKIPEDIA utachekwa na makarani wa mahakama na utafukuziwa front lobby, wala Jaji hutamfikia. Nilidhani utatuelimisha kwa nini "makubaliano" sio "mkataba" kwa mujibu wa maudhui ya vitabu vya sheria ya Tanzania, sio WIKIPEDIA!
 
sasa kwanini waislamu wakitaka kuingia makubaliano na serikali juu ya kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi mnapiga kelele? Mnadai kodi za wananchi wote zitakuwa zinalipa watu wa imani moja! Je katika hili la taasisi hizi zinazosaidiwa na serikali hutumia kodi za wakatoliki pekee?
 
Ukienda mahakamani na madesa kutoka WIKIPEDIA utachekwa na makarani wa mahakama na utafukuziwa front lobby, wala Jaji hutamfikia. Nilidhani utatuelimisha kwa nini "makubaliano" sio "mkataba" kwa mujibu wa maudhui ya vitabu vya sheria ya Tanzania, sio WIKIPEDIA!

Hata kwenye vitabu vya sheria Memorandum of Understanding maana yake ni hiyo hiyo, kama una nyingine tofauti mkuu nielimishe.
 
Asante Mwanaukweli nimepata kitu hapo. Ndugu yangu Ngwendu leta hoja zenye nguvu ueleweke na sio kusema ungeeleza mengi lakini wakati haukuruhusu, tufanye tuelewe msingi wa manunguniko/malalamiko ya waliyoko upande huo kuhusu mou.
 
sasa kwanini waislamu wakitaka kuingia makubaliano na serikali juu ya kuanzishwa kwa mahakama ya kadhi mnapiga kelele? Mnadai kodi za wananchi wote zitakuwa zinalipa watu wa imani moja! Je katika hili la taasisi hizi zinazosaidiwa na serikali hutumia kodi za wakatoliki pekee?

operation za mabusha wanazofanyiwa waislamu pale ndanda hutokana na sadaka zao? jibu ni hapana, hakuna mkristo kwa namna yoyote anaweza kupata huduma yoyote kwenye mahakama ya kadhi, huko kodi za watanzania hazihitajiki, ni sahihi wakianzisha mahakama yao ambayo kimaudhui na vitendo inawahudumia waislamu pekee, basi waislamu peke yao waigharimie mahakama yao.
 
Memorandum of Understanding si mkataba ni makubaliano ya pande mbili ambayo hayajafikia hatua ya mkataba.

Kawaida pande mbili zinazoshirikiana katika shughuli fulani muhimu hupenda kuweka makubaliano ya ushirikiano wa shughuli zao kwa maandishi. Makubaliano hayo kawaida yanaeleza:
(1) Pande husika katika makubaliano,
(2) Mambo wanayokubaliana na malengo yake,
(3) Majukumu ya kila upande katika ushirikiano, na
(4) Saini za Wawakilishi wa pande mbili.

Ni makubaliano na si mkataba. (It is a gentlemen way of spelling out agreement).

MoU haina nguvu ya kisheria.

Wikipedia ina define MoU hivi
A memorandum of understanding (MOU) is a document describing a bilateral or multilateral agreement between parties. It expresses a convergence of will between the parties, indicating an intended common line of action. It is often used in cases where parties either do not imply a legal commitment or in situations where the parties cannot create a legally enforceable agreement. It is a more formal alternative to a gentlemen's agreement.

Memorandum of Understanding kati ya Makanisa ya Kiprotestanti na Katoliki kwa upande mmoja na Serikali, inatokana na ukweli kuwa Makanisa yamekuwa yakitoa huduma za jamii ambazo ni jukumu la msingi la Serikali. Huduma za Tiba zitolewazo na kanisa ziko zaidi katika maeneo ya vijijini ambako Serikali bado haijaweka huduma hizo. Ushirikiano huo ni msaada mkubwa kwa serikali ambayo ingepasika kuwajibika kwa raia wake wote hata hao wa vijijini kwa huduma hizo.

Vilevile wilaya nyingi zilizoanzishwa miaka ya baadaye baada ya uhuru hazikuwa na hospitali za serikali zenye hadhi ya kuwa Hospitali za wilaya na Serikali imeomba ushirikiano wa Kanisa kutumia hospitali zake kama hospitali teule za wilaya. Mfano: Nkansi, Bunda, Sumve, Rombo n.k.

Kwa haraka nimepitia Hospitali, vituo vya afya na zahanati za makanisa yaliyosaini MoU hiyo na kupata 564. Hizi karibu zote zilikuwepo wakati wa kusaini MoU hiyo.

MoU kati ya Kanisa na Serikali inaongelea suala la huduma za jamii tu, haihusiki na mengineyo.

Suala ya misaada ya fedha si kwa hospitali zote, zaidi ni zile Teule na za rufaa, ambazo Serikali inazihitaji.

Bado Makanisa yanabeba jukumu kubwa la kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati. Waumini wanajua jinsi wanavyochangishwa kwa ajili ya kuchangia ujenzi na ukarabati na wakati mwingine hata kuziendesha taasisi hizo.

Nimeweka attachment ya zahanati, vituo vya afya na Hospitali za Makanisa ili muone jinsi huduma hiyo ilivyoenea vijijini (remote areas).

Nimeweka attachment ya pili ya pdf inayoonesha kuwa Serikali ya Ujerumani inapitishia baadhi ya misaada yake ya huduma za jamii kwenye shirika la misaada la Misereor, ambalo ni la Kikatoliki. Angalia title ya mwisho "MISEREOR has strong Supporters".

Craaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaap hakuna kitu hapa, hayo yote kumbe nikutafuta justification yaku chota mabilioni ya shilingi kunufaisha kanisa kwenye shughuli zake. Ujerumani ni nchi inayoongozwa kidini kwa hiyo hata ikifanya MOU na mashirika ya dini ni sawa tu. Nilitegemea utoe mifano ya nchi zetu za Afrika Mashariki ni wapi serikali zimeingia MOU na makanisa ? Huu ulikuwa ni ufisadi mmojawapo alio ufanya EL
 
ni mkataba wa kinyonyaji uliofungwa na Lowasa. laana hii ya mkataba inamsumbua mpaka kumalizika kwa Richmond. mungu tueweke mbali na kiongozi mikataba mobovu kama hii ya MOU

utalia sana na Lowassa ila ukweli unajulikana sema hutaki kukubali. Sivyo wekeni wa kwenu
 
operation za mabusha wanazofanyiwa waislamu pale ndanda hutokana na sadaka zao? jibu ni hapana, hakuna mkristo kwa namna yoyote anaweza kupata huduma yoyote kwenye mahakama ya kadhi, huko kodi za watanzania hazihitajiki, ni sahihi wakianzisha mahakama yao ambayo kimaudhui na vitendo inawahudumia waislamu pekee, basi waislamu peke yao waigharimie mahakama yao.

Hawa jamaa wanajua lakini kuna aliyewapumbaza ufahamu! Juzi Kubenea kawawekea kila kitu ila watajifanya imeandaliwa na wakristo au waseme amenunuliwa
 
Nimefukua kaburi ili kuweka sawa Mou ya DP world ili wapinga maendeleo waelewe mkataba wa kibiashara bado haujafikia hatua yake na ukifikia hatua yake kipengele cha muda kitawekwa
 
Back
Top Bottom