ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,906
- 6,909
serikali iepuke negotiations za namna hii zinatia wasiwasi. Kwa nini iwe kanisa peke yake? Memorandum ya namna hii ihusishe dini na madhehebu mengine. Serikali inaongoza wananchi siyo kanisa. Mou ya serikali ni kwa manufaa ya nchi siyo kanisa. Serikali yetu haina dini ila watu wake wana dini, wakipewa madaraka ya serikali wasi assume dogma za dini zao.kufanya hivyo ni kukaribisha mkanganyiko wa kisiasa, kiitikadi, kifalsafa na kiutawala.wenye nchi mpo!
nianze na wewe.
Nilichokielewa ni kuwa serikali haikuwa na uwezo wa kuhudumia watu wake kikamilifu. Hivyo kwa kuwa mashirika ya kidini yalikuwa na miundombinu ya kutosha, ndo wakaomba kusaidiana na mashirika ya dini ili kuhakikisha kila mtu ndani ya nchi anapata huduma zile mhimu elimu na afya bila kujali dini yake.
Kuhusiana na hiyo bilateral agreement, ni kweli serikali lazima iwatambue nchi wahsani. Kwa mfano, kuna hospital zilizojengwa na kuendeshwa na nchi wahsan kupitia makanisa yao. Sasa ili makubaliano yawe mazuri, yule mhisani kuwepo si tatizo.
Kuhusu wahindi, the aga khan ni mfano, sijui kama waliingia mkataba, lakini kama sio mkataba sidhani kama leo mie mwenye bima ya serikali ningeweza kwenda kutibiwa mahali pale. Ni mikataba hiyo inayoniwezesha mie kutibiwa hospital yoyote, bila kujali dini yangu.
Kinachowakumba ndugu zangu waisalm, hawana taasisi kubwa zinazotoa huduma hadi kuishawishi serikali kuingia nao mkataba. Kama ipo waiseme, hiyo shule au hospital ambayo ni tegemeo la watanzania wengine. Maana wenyewe hata wakijenga mfano shule watajenga mazngira ya waislam tu ndo wafike kupata huduma zao. Udini sana