MotoGP: One minute of noice in Valencia

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Tumezowea kusikia na kushiriki katika "Dakika Moja ya Ukimya" kama kumbukumbu kwa wale waliotutangulia. Lakini kutokana na kifo cha Marco Simonccelli, baba yake amewaomba washiriki katika mashindano hayo, wasimkumbuke mwanawe kwa huzuni bali kwa furaha. Simonccelli mwenye hakuwa mtu wa huzuni. Kwa hivyo kesho, badala ya kumkumbuka kwa dakika moja ya ukimya, amewata wamkumbuke kwa dakika moja ya kelele: Honda zote, vyombo vyot vya moto vitavyokuwepo uwanjani na nje ya uwanja vitarindimisha mashine na honi zao kumkumbuka Simonccelli. Ni njia nyengine ya kuyachukulia mambo! R.I.P Simonccelli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom