Moto wawaka jengo la Ushirika, Lumumba

Wamechoma moto ofisi hizo ili kupoteza ushahidi kuhusiana na makampuni fake ya kifisadi akina ANBEN, KAGODA n.k. Maskini Tanzania inasikitisha sana inafisadiwa kila kona tena na wale wale tuliowamini na kuwapa nafasi za uongozi kumbe ni mafisadi tu!

Tazama post yako hii unaiquote post yangu ambayo haikusema kuwa brella imeunguwa, hivi huwa mnasoma hizi posts au mnakurupuka tu? au si ububu tu na upofu vilevile?
 
mngekimbilia KLHN kuona breaking news wala msingekuwa kwenye matatizo ya malumbano. Motto yetu ni "we bring the news first".. siyo speculations on the news.. kwa hili Dar-es-Salaam yuko sawa.

Tusonge mbele...
 
mngekimbilia KLHN kuona breaking news wala msingekuwa kwenye matatizo ya malumbano. Motto yetu ni "we bring the news first".. siyo speculations on the news.. kwa hili Dar-es-Salaam yuko sawa.

Tusonge mbele...

kwi kwi kwi,

unataka kusema kuwa mtetezi wa mafisadi JF (Dar es salaam) sasa hivi ni msomaji mzuri wa KLHN na ameacha kuipondea? naona vyote vimemshinda!
 
kwi kwi kwi,

unataka kusema kuwa mtetezi wa mafisadi JF (Dar es salaam) sasa hivi ni msomaji mzuri wa KLHN na ameacha kuipondea? naona vyote vimemshinda!

soma thread yangu hapo juu huo moto nimeushuhudia live. Napenda kukujuza kuwa sitetei fisadi hata siku moja. Mara nyingi nimemtetea JK afanyapo jema linaloonekana na akifanya madudu ntampaka vilevile. THATS MY PRINCIPLE "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni".
 
soma thread yangu hapo juu huo moto nimeushuhudia live. Napenda kukujuza kuwa sitetei fisadi hata siku moja. Mara nyingi nimemtetea JK afanyapo jema linaloonekana na akifanya madudu ntampaka vilevile. THATS MY PRINCIPLE "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni".

mtetezi wa mafisadi kama wewe statement zako zote ziko ndani ya quotation, yaani unasoma habari KLHN na kisha unaleta uongo hapa kuwa umeshuhudia live.... kweli Jiitu Patel anahitaji msemaji mpya hapa JF
 
mtetezi wa mafisadi kama wewe statement zako zote ziko ndani ya quotation, yaani unasoma habari KLHN na kisha unaleta uongo hapa kuwa umeshuhudia live.... kweli Jiitu Patel anahitaji msemaji mpya hapa JF

kwi wkiwiwiwiwiwiw kwwiwiwiwi pwaaaah.
ama kweli nimekubali we mwanga
 
soma thread yangu hapo juu huo moto nimeushuhudia live. Napenda kukujuza kuwa sitetei fisadi hata siku moja. Mara nyingi nimemtetea JK afanyapo jema linaloonekana na akifanya madudu ntampaka vilevile. THATS MY PRINCIPLE "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni".

......Puhleeez!. I've seen your posts.
 
Kwani kupoteza nyaraka za BRELA ni lazima kuchoma ofisi moto?

Mbona mafaili na karatasi kunyofolewa ni kawaida; na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa kwa wahusika au viongozi!
 
This one was very much predictable and waTZ deserve explanations on what measure did the govt took to safegurd her records, especialy those linked to the recent scandals. I hope BoT wont be the next one.
 
Posted Date::3/3/2008
Jengo la ghorofa 12 lanusurika kuteketezwa kwa moto Dar
James Magai na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

MOTO mkubwa uzuka na kuteketeza nusu ya sehemu ya chini jengo la Ushirika lililopo Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Ofisi zilizoteketea ni zile zinazotazamana upande na Benki ya CRDB, ambayo nayo imeponea chupuchupu kuungua.

Jengo hilo lenye gorofa 12 limepana ofisi nyingi zikiweomo za serikalia makampuni na watu binafi na pia ni Makao Makuu ya Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji nchini.

Hata hivyo, tukio hilo halikusababisha madhara kwa ofisi za kikosi hicho ambacho kipo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, baada ya askari wake kuwahi kuudhibiti moto huo usipande ghorofani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala Masindoki Masindoki, alithibitisha kutokea kwa moto huo ambao ulianza juzi saa 4.30 usiku na kuteketeza mali zote zilizokuwemo ndani ya ofisi hizo.

Masindoki alisema hadi jana, thamani ya mali ilikuwa imeteketea haikuwa imejulikana na kwamba hakuna athari zozote kwa binadamu.

Kwa upande wake, Kaimu Kamishna Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto, Mohamed Kapamba, alilisema moto huo ulianza kuwaka chini kwa chini.

Kapamba alifafanua kwamba, baada ya taarifa hizo kusambaa kuanzia saa nne ilichukua muda wa dakika nne kwa magari ya vikosi mbalimbali ikiwemo ya kikosi hicho na Jiji kufika eneo la tukio.

Alipoulizwa vipi moto huo ulichukua muda mrefu kuzimwa wakati umetokeoa Makao Makuu ya Ofisi za Zimamoto na karibu na Jiji, alijibu: Kilichochelewesha ni mfumo wa umeme, ilibidi tuanze kuwasiliana na wenzetu Tanesco (Shirika la Umeme nchini), ambao walikuja baadaye, alisisitiza Kapamba.

Kapamba aliongeza kwamba, kama kusingekuwa na tatizo la mfumo wa umeme na Tanesco wangewahi, ni dhahiri wangeweza kuudhibiti moto huo mapema.

Alitaja sababu nyingine kubwa ya pili kwamba, ofisi nyingi zilikuwa zimefungwa kwa mageti maalumu hivyo kazi ya kuvunja nayo ilichukua muda.

Ule moto awali uliwaka ndani kwa ndani, sasa hadi kujitokeza nje ulikuwa tayari umekuwa mkubwa, hadi kuvunja mageti ya milango na kuingia nayo ilichukua muda,? alisisitiza Kapamba.

Kuhusu vipi waliweza kuzuia ofisi zao za ghorofa ya nne zisiungue, alisema wakati ukiwaka askari wa kikosi hicho waliokuwa zamu walidhibiti mfumo wa umeme na kujipanga kuhakikisha moto haufiki katika ofisi zao.

Alisema lita za maji zilizotumika ni zaidi ya 30,000 kwa taarifa za awali na kuongeza kwamba bado tathimni inaendelea kufanyika.

Kwa upande wa mmoja wa askari aliyeshudia tukio hilo ambaye ni kutoka kikosi cha jiji Makao Makuu, Sud Alfan, alisema walipata taarifa za kuungua kwa jengo hilo saa 4.00 usiku na kufika eneo hilo saa 4.11 na kukuta moto mkali katika moja ya ofisi hizo.

Shuhuda huyo, alisema chanzo cha moto huo kinawezekana kikawa ni mashine ya kupozea upepo (Air Condition- AC) kwa kuwa ndiyo iliyokuwa ya kwanza kuungua.

Hatujawa na uhakika, lakini tunahisi chanzo cha moto huo ni AC ambayo iliachwa bila kuzimwa, kwani ndio kifaa cha kwanza kuungua humu. Labda kuna mfanyakazi wa ofisi hiyo ambaye alikuja ofisini jana akawasha mashine hiyo halafu akasahau kuizima na kusababisha hitilafu ya umeme, alisema Alfan.

Alfan alifafanua kwamba, ukali wa moto huo ulichochewa na aina ya malighafi zilizotumika kutengeza dari katika jengo hilo.

Dari za jengo hilo zimetengenezwa kwa majaribosi aina ya takataka za mbao na sehemu kubwa ya kuta za ofisi hizo, zilikuwa ni za mbao jambo ambalo lilisababisha moto huo kuwaka kwa nguvu sana,alisema.

Taarifa zaidi ambazo hazikuthibitishwa, zilisema askari wa wawili, Donald Ndimbo na Mohamed Mtemba, walijeruhiwa baada ya kuangukiwa na vioo wakati wakiwa katika harakati za kuzima moto huo.

Kamanda wa Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji cha Kampuni ya Nihgt Support, Kevin Lubela naye alisema, inahofiwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyotokea katika AC ndani ya ofisi moja na kwamba walifika katika eneo latukio saa 6.30 usiku wakati shughuli ya uzimaji moto huo ilikamilika saa 11 alfajiri.

Mwananchi lilifika katika eneo la tukio saa 12.30 asubuhi na kukuta vikosi hivyo vikijaribu kuzima moto huo huku wamiliki wa ofisi na mali zilizoteketea, wakilia wakiwemo mama mmoja ambaye alisema kasha lote la pesa limeteketea, bila kutaja jina lake, ofisi na kiasi hicho cha pesa kilichoteketea.

Baadhi ya wapangaji katika jengo hilo, Agness Mtiganzi, Mkurugenzi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Aglex Company Ltd, na Mama Mohamed Suleiman wa Kampuni ya Uchapaji ya Education Books Publishers, walisema mali zao nyingi ziliteketea.

Hata hivyo, wapangaji hao hawakuwa tayari kueleza thamani na aina ya mali zilizoteketea mbali ya kusisitiza mali nyingi zimeteketea.

Moto huo ulizimwa kwa ushirikiano wa Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji cha Jiji, Kikosi cha Zima Moto na Uokoaji cha Bandari, Night Support, Security Group, Ultimate Security na Kikosi cha Zima Moto cha Uwanja wa Ndege.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dares Salaam, Kamishna Alfred Tibaigana, alifika eneo la tukio na alipohojiwa na Radio Tanzania (RTD) ambayo iko chini ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), alisema inasadikiwa ukali wa moto huo, ulioteketeza ofisi za jengo hilo na ulitokana na makaratasi ambayo ni malighafi, iliyotumika kutengeneza ofisi mbalimbali katika jengo hilo.

Tukio hili ni moja ya janga kubwa kuwahi kulikumba jiji la Dar es Salaam katika siku za karibuni, ambapo la mwisho lilikuwa ni kuungua kwa Hoteli ya Sea Cliff, mwishoni mwaka jana na kusababisha hasara ya mamilioni ya shilingi.
 
Mimi nataka kujua tu kama ofisi za Brela hakiguswa na kama hazigukuswa kwa nini leo hazikufanya kazi ?Ina maana kweli ofisi kubwa namna ile inakosa umeme kisa ajali ya moto ? Je kama jengo halitakuwa na umeme kwa siku kadhaa ina maana maofisi yote jengo hilo yanafungwa ?If not Brela wana mpango upi wa kurudisha huduma kwa uharaka ?
 
Ambao tuko nje ya mji tuambieni tuelewe,ni kweli ofisi za Brela zimeungua?
 
kwi kwi kwi,

unataka kusema kuwa mtetezi wa mafisadi JF (Dar es salaam) sasa hivi ni msomaji mzuri wa KLHN na ameacha kuipondea? naona vyote vimemshinda!

..mwk,

..rejea post zetu za nyuma juu ya ndugu yetu huyu!

..kwasasa amesilimu! if u know what i mean.

..ukweli humweka mtu huru!
 
Jamani nauliza hivi?..
Ati, kweli Brela iko chini ya uongozi wa mtoto wa Mkapa?...
 
Back
Top Bottom