Moto waunguza bweni chuo cha Kilimo (MTWARA)

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,306
6,514
Kumetokea ajali ya moto katika chuo cha kilimo Mtwara(MATI-Mtwara). Moto huo umetokea majira ya saa tatu asubuhi leo hii, Umeunguza bweni la wasichana linalochukua takribani watu 70. Chanzo cha moto huo inasemekana kuwa ni hitilafu ya umeme katika mo ya chumba kilichopo kwenye bweni hilo. Vyanzo vimezidi kueleza hakuna madhara yeyote yaliyotokea kwa wanafunzi hao zaidi ya kuunguliwa na vitu vyao pamoja na magodoro yao ya kulalia. Polisi walifika chuoni hapo na kuchukua maelezo kwa mkuu wa chuo hicho ndugu Waziri mwinyi. Kikosi cha kuzima moto kilishindwa kupeleka gari chuoni hapo kwa kile kilichoelezwa kuwa ni ubovu wa gari lao, hivyo kulazimika kutumika gari la kuzima moto la bandari. Chuo cha kilimo Mtwara kipo kama kilomita kumi na nne kutoka mtwara Mjini, kinatoa kozi za kilimo kwa Ngazi ya cheti na Astashahada.
 
Back
Top Bottom