Moto walipuka chini ya mti Arusha karibu na kituo cha Sabena.

Losambo

JF-Expert Member
Nov 8, 2011
2,613
864
UPDATES;

Moto huo umeshadhibitiwa tayari kutokana na juhudi za wananchi na kikosi cha zima moto. Hadi sasa haijulikani moto huo umesababisha hasara kiasi gani.

Moto mkubwa umelipuka katikati ya jiji la Arusha na mpaka saizi umeshateketeza maduka kadhaa.

Kama ilivyo ada ya magari ya fire yamekuja bila maji na kukuta wananchi wanapambana kuzima moto. Jambo hilo lioengeza ghadhabu kwa wananchi na kushindwa kuelewa kazi ya kikosi hicho cha fire ni nini?

Stay Tunes for updates.

View attachment 51473

View attachment 51472

Vijana Wakizima Mot.JPG

Umati Ukishuhudia Moto.JPG

Umati 2.JPG
 
Last edited by a moderator:
Niko maeneo ya tukio! Lakini sishangai matukio ya moto kama haya sasa hivi jijini Arusha maeneo ya stand kuu ya mabasi Vibosho wanazinunua hizi nyumba zenye mabati ya Madebe kwa kasi sana, wakiwafuata wenye hizo nyumba wawauzie kama wakiringa tu basi muda si mrefu utasikia nyumba imewaka moto! Na sheria za mipango miji huruhusiwi kukarabati wanataka ujenge Gorofa unategemea nini kitafuata!??
 
Duh!
Ama kweli hali siyo yenyewe kabisa!
Mali za watu zinateketea pasipo na mfano.
Hali ni mbaya sana
 
Nimepita maeneo hayo nimeshangaa sijui siasa inahusikaje, maana vijana wanasema pipoooozz!!! Hii ni hatari sana
 
Nitatupa picha muda si mrefu pamoja na video clip ila watu ni wengi na moto umeshadhibitiw hakuna vurugu.
 
Niko maeneo ya tukio! Lakini sishangai matukio ya moto kama haya sasa hivi jijini Arusha maeneo ya stand kuu ya mabasi Vibosho wanazinunua hizi nyumba zenye mabati ya Madebe kwa kasi sana, wakiwafuata wenye hizo nyumba wawauzie kama wakiringa tu basi muda si mrefu utasikia nyumba imewaka moto! Na sheria za mipango miji huruhusiwi kukarabati wanataka ujenge Gorofa unategemea nini kitafuata!??

Kwa nini umetumia neno VI - bosho?
 
Hili nalo ni neno mkuu

Niko maeneo ya tukio! Lakini sishangai matukio ya moto kama haya sasa hivi jijini Arusha maeneo ya stand kuu ya mabasi Vibosho wanazinunua hizi nyumba zenye mabati ya Madebe kwa kasi sana, wakiwafuata wenye hizo nyumba wawauzie kama wakiringa tu basi muda si mrefu utasikia nyumba imewaka moto! Na sheria za mipango miji huruhusiwi kukarabati wanataka ujenge Gorofa unategemea nini kitafuata!??
 
Nimepita maeneo hayo nimeshangaa sijui siasa inahusikaje, maana vijana wanasema pipoooozz!!! Hii ni hatari sana

Duh!Hii kali.Kwahiyo hilo tukio wameshalihusisha na siasa?Haya bhana lakini hakuna tatizo tutafika tu!
 
Mara ya kwanza Fire zilikuja na maji machache zikashindwa kuuzima lakini wananchi kwa pamoja waliungana na kuuokoa msikiti uliokuwa karibu kuuanza kuungua.....sasa baada ya fire kushindwa kuzima na polisi kubaki wakishangaa wasijue la kufanya ndipo wananchi walipo shirikiana na kuuzima moto baada ya kuuzima gafla polisi wakaanza kuwasukuma wananchi ndipo wananchi wakaanza kuimba peoples Power wakiwa na maana umezimwa kwa nguvu ya umma.....wakaanda mbali kabia baada ya kuwaambia wakalete yale magari yao ya maji ya kuwasha ili yatumike kuzima moto
 
Nimepita maeneo hayo nimeshangaa sijui siasa inahusikaje, maana vijana wanasema pipoooozz!!! Hii ni hatari sana

Mkuu naskia kua kwa Arusha hyo "pipoz power" ni kauli mbiu ya kuhamasisha kufanya kazi, pia hutumika kama salaam kwa watu wanaokutana njiani..
 
Duh!Hii kali.Kwahiyo hilo tukio wameshalihusisha na siasa?Haya bhana lakini hakuna tatizo tutafika tu!
Nii baada ya vijana kushirikiana kuuzima/ kupunguza makali na kufanikiwa kuuonkoa msikiti bila kuwana zima moto hivyo swala hilo likatafathiliwa kuwa ni nguvu ya umma
 
Ama kweli Tanzania yetu bado ni giza tupu!

Lusambo!
Tunakutegemea kwa picha kwani ktk pilika hii gari yangu imegongwa na ile gari la fire nikiwa hapo.

Ntarudi after!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom