Moto wa katiba mpya.

Kulolwa

Member
Feb 12, 2011
6
0
Wana JF nawaomba tukumbushane ni kama sasa tunaelekea kutaka kupoteza na kuzima moto wa kushughulikia Katiba mpya.Kama kawaida yetu watanzania tunajidai tunajadiliana kwa muda mfupi halafu eti tunasahau mwasemaje juu ya hilo?
 
Wana JF nawaomba tukumbushane ni kama sasa tunaelekea kutaka kupoteza na kuzima moto wa kushughulikia Katiba mpya.Kama kawaida yetu watanzania tunajidai tunajadiliana kwa muda mfupi halafu eti tunasahau mwasemaje juu ya hilo?

Karibu TZ ndugu.
 
Kweli mkuu...Hata mimi nahisi kama tumeanza kuacha kuukoleza ule moto wa kudai katiba mpya!
 
inawezekana do once na sasa mabomu ya goms yamechangia kupunguza kasi.
Naamini kuwa ni kwa muda tu tunashukuru kukumbusha.

Nina hoja moja hapa ,kwa mfumo wetu wa muungano Tanzania,inapotokea Raisi ni kutoka visiwani na mambo yaliyo kwenye Muungano ni machache je ni halali kwa raisi huyo kutolea maamuzi mambo yasiyo ya muungano ?Hii ni pamoja na wizara, mfano ni mambo ya ndani ya nchi mara kadhaa inashikiliwa na wazenji kwa sasa shamsi Nahodha anaposhughukia zimamoto au magereza mambo yasiyo ya muungano inakuwaje ?
 
inawezekana do once na sasa mabomu ya goms yamechangia kupunguza kasi.
Naamini kuwa ni kwa muda tu tunashukuru kukumbusha.

Nina hoja moja hapa ,kwa mfumo wetu wa muungano Tanzania,inapotokea Raisi ni kutoka visiwani na mambo yaliyo kwenye Muungano ni machache je ni halali kwa raisi huyo kutolea maamuzi mambo yasiyo ya muungano ?Hii ni pamoja na wizara, mfano ni mambo ya ndani ya nchi mara kadhaa inashikiliwa na wazenji kwa sasa shamsi Nahodha anaposhughukia zimamoto au magereza mambo yasiyo ya muungano inakuwaje ?[/QUOTE]


Ndo maana tukasema mfumo pekee wa kuondoa tatizo hili ni serikali tatu, lakini kwa kuwa "Zi(na)dumu fikira na mawazo ya Mwalimu Nyerere, bado tunang'ang'ania mfumo huu mbovu ambapo hatujui mipaka baina ya Serikali mbili. Na sio magereza na zimamoto tu, kuna wakati wazenji wamewahi kuongoza Wizara za Mawasiliano (Maua Daftari), Habari, Utamaduni, Vijana, Michezo (Mohammed Seif), Ulinzi na JKT. Zinahusianaje na mambo ya Muungano hadi wapewe wazenji Wizara kuongoza?

Utata mwengine (ingawa hili halimo katika suala lako la msingi), kwa nini tunakuwa na duplication za wizara? Mfano, ikiwa Fedha, Ulinzi na Mambo ya Ndani ni wizara za Muungano, kwa nini Zanzibar wanakuwa na Wizara nyengine ya Fedha, Magereza, Vikosi vya serikali? Hii nchi lini itawacha madudu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom