Moto ubungo

nami pia nilipita mida ya saa nne usiku na maduka kama saba hivi yalishaungua na moto ulikuwa ukiendelea kusambaa, hasara uenda ikiwa kubwa na vibaka walionekana kujipanga vizuri.

Nashangaa mfumo wa habari wa hapa kwetu, sijaona kama kuna gazeti lemetoa hizo habari lakini ni tukio la kusikitisha na kuonyesha tulivyokalia kaa la moto
 
Sioni cha ajabu kwenye habari hii.

Eneo hilo limekaa kihatarihatari mtupu. Kuna msongamano wa nyumba na vibanda vidogovidogo vingi. Kama unaingia dsm kwa mara ya kwanza ni ngumu kuamini kama umeshafika dsm. Hilo eneo lina msongamano sana wa nyumba na vibanda hata hamna nafasi baina ya nyumba. Ni wazi kama moto ulitokea si salama hata kwa wazima moto wenyewe, hamna sehemu ya kupita wao wala kupitisha mipira ya maji.

Watz tuache kulalama tuzingatie sheria za ujenzi. Saivi mtu anajenga popote pale anapojiskia na serikali za mtaa zinafurahia asilimia 10% ya mauzo, matokeo yake ndo kama hayo.
 
Back
Top Bottom